Jumanne, 16 Februari 2016

Kwani mmemuokotea wapi huyu ?



Nilimuokotea kituoni.........

Si kila mahali ni  Mahali sahii kuanzisha mahusiano bila kumjua mwezio kwa kina


Naomba nikiri kwamba katika mbilinge zangu za kuwania mabinti ujanani nilipata misukosuko mingi sana kiasi kwamba kila nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe. Namuomba Mwenye Enzi Mungu, wanangu wasije wakarithi hiki kipaji changu.

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1990, wakati huo nikiwa ni kijana barubaru. Nilikuwa natokea kwa Kaka yangu Sinza naelekea Mwenge kwa shangazi yangu nilipokuwa nikiishi.

Nikiwa kituoni, ndipo nilipokutana na binti huyu. Huyu binti alionekana mchangamfu na muongeaji sana. Alinisalimia kama vile ananifahamu kwa kuniuliza habari za nyumbani na kama wazazi hawajambo. Alikuwa ni mweusi na mzuri kwa sura na umbo. Huwa napenda sana mabinti weusi, mwenyewe huwa nawaita Black Beauty.
 
Pia alikuwa na macho fulani ya kulegea kama vile amekula kungu, Alionekana kuwa msomi maana alikuwa anaongea Kiswahili huku akichanganya na kiingereza. Kwa kuwa na mimi nilikuwa napenda sana kuongea kiingereza, japo sikuwa nakijua vizuri, nilijitahidi kuongea naye huku nikiweka manjonjo ya Kimarekani.

Mbele ya mtoto ambaye anaonekana yuko vizuri upstairs lazima ujue kuweka mapozi japo kidogo. Kwa kuwa nilikuwa mbovu wa macho na nilikuwa natumia miwani ya macho aina ya photo Chromic ilinifanya nionekane kuwa ni msomi wa Chuo Kikuu wakati niliangukia pua kidato cha nne kwa kupata ziro. Lakini hata hivyo nashukuru hizi English Course zilinitioa kimasomaso nisionekane kilaza mbele ya binti mrembo kama huyu.

Nilijaribu kufikiria nilipokutana naye bila mafanikio. Lakini alinivutia kwa ucheshi wake na tabasamu lake. Basi pale kituoni tuliongea kidogo na basi lilipowasili tulipanda wote ambapo alinilipia nauli ingawa nilijifaragua kutaka kumlipia wakati nauli ya kumlipia sikuwa nayo.


Tulipofika Mwenge tuliachana ambapo alipanda mabasi ya Kawe alipokuwa akiishi kama alivyoniambia, lakini tulikubaliana tukutane wiki inayofuata pale Mwenge kituoni.

Ni kweli wiki iliyofuata tulikutana pale kituoni Mwenge, alikuwa mchangamfu sana safari hii ikiwa ni mara mbili zaidi. Alikuwa amevaa pedo nyeupe ambayo ilikuwa imembana na kuacha mahips yake yakiwa yametokelezea, juu alikuwa amevaa kitopu chekundu.

Basi tulitafuta mahali tulivu tukapata chipsi kuku, na baada ya kumshawishi kufanya mapenzi wala hakuwa mbishi, tukaenda katika Gesti ya TURUNYA iliyoko pale Mwenye Mlalakuwa na kufanya tendo, ambapo gharama zote alilipa yeye. Hata hivyo kwenye ushiriki wa tendo niliogopa kidogo, kwani alikuwa anafanya vituko vya aina nyingi.

Lakini nilijua huenda mdadi wa masuala ya mapenzi. Lakini, kwa kweli, labda kile tunachoita kupenda ni upofu, ndicho kilichonifanya nisione ukweli mkubwa zaidi. Tulizoeana na huyu binti haraka sana lakini vituko vyake vilikuwa vinazidi kila siku. Kuna siku niliamua kumpeleka nyumbani kwa shangazi yangu nilipokuwa nikiishi. Shangazi yangu alishangazwa na uchakaramu wake.

Mara anakwenda kuwasha Music System iliyokuwa pale sebuleni na kuanza kucheza mziki Kimarekani, mara atoe hela zikanunuliwe soda, wakati yeye ndiye mgeni pale nyumbani, ili mradi alikuwa na vituko vingi tu na uchakaramu uliopitiliza.

Shangazi aliniuliza kama namfahamu yule binti vizuri na nilimdanganya kwa kumwambia napafahamu hadi kwao. Ukweli ni kwamba huyu binti alikuwa akiniambia mara anaishi Kawe, mara Msasani, mara Masaki na wakati mwingine Kinondoni, ilimradi hakuwa anaeleweka.

Ilikuwa kila tukikutana alikuwa analipa gharama zote za mtoko mpaka malipo ya Guest tuliyokuwa tukikutana na kufanya tendo. Lakini pia matumizi yake ya fedha yalikuwa ni ya fujo. Aliniambia kwamba alisoma nchini Marekani na baba yake ni mtu mkubwa sana serikalini.
Siku moja huyu binti aliniambia angependa kunipeleka kwao, ilibidi nimwambie tupange siku. Nilitaka kuwachukua marafiki zangu wa pale mtaani kwenda nao kwao, kwani kwa kule kutokuwa na msimamo kwake kwamba, kwao hasa ni wapi, nilikuwa nimemwogopa kidogo.

Siku tuliyokubaliana kwamba, angenipeleka kwao ilifika. Niliwachukua rafiki zangu watatu na kwenda nao. Ni kweli yule binti alitupeleka kwao. Ilikuwa ni Kawe. Ile kufika tu tukaona watu wa familia wametulaki kwa njia ya ajabu.

Afadhali tunashukuru sana. Kwani mmemuokotea wapi? Ni mwezi mzima sasa tunamtafuta. Aliondoka na shilingi laki saba hapa…” Mama yake alisema na sisi tukashikwa na butwaa.

“…..Kwani …… kwani ….. Alipotea?” Niliuliza nikiwa na kigugumizi. Mama yake alisema, Mwanangu masikini ana tatizo la kiakili karibu mwaka wa tatu sasa………..”

Nilihisi nikiwa nimechoka, hata kusimama nilishindwa. Nilijikuta nikikaa chini. Wale marafiki zangu walinitazama tu. Nataka niwe mkweli, katika kipindi nilichokuwa nikijivinjari na huyu binti, nilikuwa nawaringishia sana hawa marafiki zangu, kwa kujidai kwamba nimeopoa binti wa Kimarekani.

Tuliaga na kuondoka huku wenzangu wakijifanya kunipa moyo. Nasema walijifanya kwa sababu, wao ndiyo walitangaza kila mahali pale mtaani kuhusu jambo hili. Walinikera sana
…..

Kwa mwenzi mzima, nikawa natoka ndani usiku tu
……….

Hakuna maoni: