Osama
Bin Laden ni mmoja wa matajiri wakubwa sana aliyeishi uhamishoni baada ya
kuikimbia nchi yake ya Saud Arabia. Ndiye anayeaminika kuwa anahusika na mashambulizi ya kigaidi Ya September 11
huko Marekani Mwaka 2001 ambapo katika tukio hilo watu Elfu tatu waliuawa
(3,000) Ni mtu aliyekuwa na chuki kubwa sana dhidi ya Marekani, akiwa na
usahawishi mkubwa miongoni mwa ulimwengu wa kiislamu,Osama alihusikka na
mashambulizi mengine madogomadogo kuihusu marekani akiwa nchi ya ukimbizini
yaani Afghanstan
Osama Bin Laden Moja ya watu wenye akili sana Duniani ambazo shetani alizitumia
Osama Bin Laden alizaliwa Mwaka 1957 Huko Saud Arabia
Ni miliomnea mkubwa sana duniani ambaye pia ni mwanzilishi wa kundi la ugaidi
liitwalo Al-Qaida ambao ni mtanadao mkubwa sana wa kigaidi unaohusika na
shambulizi baya la kigaidi lillilo fanyika Saeptember 11 mwaka 2001 huko
Marekani, ugaidi uliofanyika kwa kusudi la kuishambulia Marekani, Pia alihusika
na mashambulizi mengine yenye uhusiano na kuiudhi marekani yaliyofanyika Mwaka
wa 1999, kulingana na uchunguzi wa shirika la utafiti la kimarekani federal
Bureau of Investigation (F.B.I.) unathibitisha kuwa Osama alihusika na
mashambulizi ya kigaidi ya kuzishambulia
Balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya
mwaka 1998, Wengi hawagahamu mengi kuhusu maisha ya Osama Bin Laden hasa
watu wa mataifa ya Magharibi, Ingawa alirithi utajiri mkubwa sana kutoka kwa
baba yake ambaye alikuwa na kampuni ya ujenzi iliyofanikiwa sana kutoka na na
ukaribu wake na familia ya kifalme ya Saudia.
Bin Laden alianza kupata umaarufu kimataifa kuanzia miaka ya mapema ya
1980 nchini Afaghanstan kwaajili ya umahiri wake katika kupambana na Majeshi ya
Kisoviet akiwa Afaghanstan, Jamuhuri ya Kisoviet ilikuwa imaivamia Afaghan
mmnamo mwaka 1979. Akiwa kijana mdogo
alipataq mafundisho ya msingi ya Kiislamu na aliamini kuwa uvamizi wa kisoviet
kuwa ni dhambi isiyosameheka kwa katika ardhi ya Kiislamu, Bin Laden alisaidia
kifedha na kwa kutoa msaada wa aina mbalimbali, alijenga Kambi za mafunzo ya
kijeshi na Barabara na vyombo vya habari, Pia alifadhili usafiri wa wanajeshi
mbalimbali waliosafiri kuja kujitoa wakitokea mataifa mbalimbali ya
kiarabu.Wakati huo Marekani pia iliwasaidia wale waliokija kuipiga Urusi
Jamuhusi ya Kisoviet wakati huo kwa uvamizi wake dhidi ya Afaghan. Mwishoni mwa
mwaka 1988 Baada ya vita kuisha, Bin Laden alianzisha kundi la kigaidi liitwalo
Al-Qaida ambalo maana yake ni “Arabic for the Base” maana yake “Waarabu kwa
Maswala uya Msingi” hili ni kundi ambalo kwa madai ya maafisa wa kimarekani
kimsingi linadaiwa kuhusika na kupanga uanzishwaji na uendeshwaji wa makundi
mengine ya kigaidi yenye msimamo wa imani kali za kiislamu duniani kote.
Mwaka 1989 baada ya vita vya Afghan Bin
laden alirudi Saud Arabia na mwaka uliofuata Kuwait Ilivamiwa na Iraq na
Marekani ilionyesha mwitikio kwa kuunganisha majeshi ya washirika na kuivamia
Iraq katika vita vya ghuba ya uajemi, na kuanzia wakati huu Ufalme wa Saud
Uliruhusu majeshi haya ya wavamizi kuitumia Ardhi ya Saudia na Bin Laden aliudhishwa sana na kitendo
hicho kwani aliona kuwa maadui wa Kiislamu wanaikanyaga Ardhi Takatifu Karibu
na Mecca na Madina na ndipo alipoanza kuwakosoa viongozi hao Jambo lililopelekea
miaka miwili baadaye 1992 kufutiwa uraia wa Saudia aliondoka huko na Kuelekea
Sudan ambako wakati huo Uislamu wenye misimamo mikali ulikuwa uimepata nguvu,
miaka miwili baadaye Sudan ilimuondolea uraia wake na kutaifisha mali zake huko Saudia.
Wengi wa wapiganaji wenye asili ya
Kiarabu wa vita vya Afaghan walijiunga na Osama huko Sudani ambako alianzisha
biashara za aina mbalimbali, huku akimiliki kampuni mbalimbali za ujenzi na
kufadhili ujenzi wa barabara na huko alianzisha vituo vya mafunzo na kuwasaidia
mtandao wake wa kigaidi wa Al-Qaeda akisaidiwa na waarabu wenye asili ya
Kiafghan, Mwaka 1996 kwaajili ya msukumo wa Kimarekani na sertikali ya Saudia
Sudan walimfukuza Bin Laden na akaenda kuishi mafichoni huko Afghanstan
Mwaka 1996 alitoa wito wa kwanza kabisa wa
kutangaza vita takatifu Jihad dhidi ya Marekani na uwepo wake katika inchi
nyingine na kwa mujibvu wa maafisa wa kimarekani tangu wakati huo alianza
kuchukizwa na uwepo wa Marekani katika nchui za Kiarabu, huku akichukizwa na
jinsi wanavyoiunga mkono Israel na kuiona Marekani kama inaendeleza vita
takatifu ya Kikristo Crusades na akiamni kuwa Wakristo wa Magharibi wana mpango
wa kuivamia ardhi ya waislam. Inaaminika kuwa ni kundi hili la Al-Qaeda
linalosaidia kiuchumi vikundi vingi vya kigaidi ulimwenguni
Bin Laden anaamini kuwa shughuli za Wamarekani
katika mashariki ya kati zina uhusiano na
vita takatifu ya kikristo kwa mfano uongozi vibaraka huko Kuwait, kuiunga
mkono Israel Al-Qaeda walikiri mara ya kwanza kabisa kuhusika na shambulizi la
Bomu mwaka 1995 wakati wa muungano wa Saudia na Amerika katika mafunzo ya
kijeshi huko Riyadh mji mkuu wa Saudia, ambapo watu watano waliuawa
Mwaka 1998 walishambulia ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania na Kenya na tukio la shambulizi dhidi ya Manoari ya
Amerika mwaka 2000, na bin Laden alihusishwa na mashambulizi hayo, Mwaka 2001
Ndege ziliongozwa kushambulia jumba la kituo kikuu cha kijeshi nchini Marekani
maarufu kama Pentagoni na baadaye ndege mbili kuiga na kushambulia minara mikubwa miwili ya kituo kikuu cha
kibiashara cha kimataifa na kwa kufuatia matukio hayao U.S.A iliivamia Afghan
na kuiondoa madarakani serikali ya
Kitaliban ambayo ilikuwa ikimkumbatia na kumuunga mkono Bin Laden na kundi la
Al-Qaeda, mwaka 2002 Bin Laden alitoa kanda inayothibitisha kuhusika na tukio
la September 11
World trade center Mahali magaidi walishambulia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 3000
Mwaka 2004 Kabla kidogo ya Uchaguzi wa
rais nchini Marekani Bin Laden alitoa kanda tena kupitia kituo maarufu cha
habar Al Jazeera ambapo ndani yake Bin Laden aliwaonya watu wa Marekani kuwa
kama “mtachezea hali ya amani yetu tutachezea hali ya amani yenu” Bin Laden
aliongeza kuwa kilichompelekea kuishambulia
Marekani na kuishambulia kigaidi
kitendo chao cha tukio la mwaka 1982 ambapo Israel iliivamia Lebanon na
nilipoangalia minara na magorofa ya Lebanon ikiangushwa chini nilijisikia kuwa
hawa wasio haki wanapaswa kuteseka kama ilivyokuwa Lebanon yaani minara au
magorofa marefu huko Marekani ni laimz iangushwe ili nao waonje maumivu ya
kuangusha ya wengine na kuacha kuwaua watoto wetu na wanawake wetu”
Marekani ilipeleka majeshi yake nchini Afaghanstan na kuayashambulia majeshi na ngome
kubwa ya ugaidi duniani kwa muda mrefu na wakati mwingine wakifanyiwa mashambulizi
ya kushitukiza hata hivyo mnamo tarehe 2 Asubuhi vyombo vya habari vilitangaza
kuwa Osama bin Laden ambaye kwa muda mrefu alikuwa mafichoni kuwa ameuawa Osama
aliuawa na majeshi ya Marekani usiku wa kuamkia 2nd May 2011 Huko Pakstan ambapo Raisi wa Marekani
Barack Obama alitarajiwa kuutangazia ulimwengu kuwa kiongozi huyo mkubwa wa
mtandao wa ugaidi duniani siku zake zimekoma za kuweko duniani Hakuna marefu
yasiyo na mwisho.Hata hivyo utata ulijitokeza kati ya nchi ya pakstai na
Marekani kuwa ilikuwaje Osama ajifiche nchini humo bila Pakstan kuwa na
taarifa, Pakstan walikiri kuwa hawakuwa na taarifa ya kuwa gaidi Huyo aliishi
nchini humo.
Rais Barack
Obama
Barack Obama alikuwa Seneta wa jimbo la Illinois nchini Marekani mnamo
mwaka 2004, Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2008 kwa tiketi ya chama
cha Democratic Katika kipindi cha utawala wake alipunguza kwa kiwango kikubwa
majeshi ya Marekani nchini Iraq lakini aliongeza nguvu nchini Afaghan kwa
kuzingatia kuwa ndio kituo kikuu cha uzalishaji magaidi Duniani kuongezwa kwa
wanajeshi nchini huko kumeleta matokeo Mazuri ya kusambaratika kwa ngome kubwa
za kigaidi ikiwemo kuuawa kwa Osama wengi walipongeza kuuawa kwa mjahidina huyo
aliyeua wengi duniani kweli aushikaye upanga ataangamia kwa upanga.wengi
walifikiri kuwa atakuwa mwenye msimamo Baridi kuhusu maswala ya wenye siasa
kali duniani lakini sasa watu wamekubali ule usemi kuwa Paka ni paka tu hata
akiwa mweusi Raisi Jakaya Kikwete
wa Tanzania alipongeza kuuawa kwa bin
Laden na kusema ni ushindi mkubwa kwa vita dhidi ya ugaidi alisema kuwa ingawa
si vema kushangilia kifo ca mwanadamu yeyote hata kama ni adui yako lakini
kuuawa kwake ni nafuu kwa vita dhidi ya ugaidi alisema kikwete
UFAHAMU
KUHUSU AL-QAEDA
Al-Qaeda ni moja
ya mtandao mkubwa wa kimataifa wa kigaidi ulioanzishwa na Osama Bin Laden
uitwao al-qaeda ambao una makusudi ya
kushambulia nchi za magharibi kama sehemu ya kulipiza kisasi kwa nchi
hizo zinzofikiriwa kuwa kinyume na uislamu na hususani Marekani, Mtandao huu
unashikilia misimamo mikali ya sharia za kiislamu. Jina Al- qaeda maana yake ni
“Waarabu kwa maswala ya Msingi”wao ni wana mapinduzi wa kiislamu ambao wako
tayari kupambana katika kuhakikisha kuwa wanatetea maslahi ya kiislamu
ulimwenguni
Al-qaeda pia wanahusika na tukio la
September 11,2001 ambapo kituo kikuu cha kimataifa cha biashara kilichoko New
York City na Kituo cha kijeshi Pentagon kilichoko Arlington,Virginia Karibu na
mto Potomac Karibu na mji mkuu wa Marekani Washingtone katika siku hiyohiyo,
Magaidi wapatao 19 waliongoza ndege iliyokuwa na abiria wengine wane mara baada
ya kuruka toka uwanja wa Boston,Massachusetts,Newark,New Jersey na Washingtone,
Ndege mbili pia ziliruka na kushambulia minara mikubwa miwili ya kituo kikuu
cha biashara kama ilivyoonyeshwa katika picha hapo juu jumla uya watu waliouawa
kutokana na mashambulizi hayo ni 30,000.
Al-qaida walihusika na shambulizi za
ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania tukio ambalo lilitokea 1998, matukio mengine ni pamoja na
lile la Manoari ya Marekani huko Aden Yemen, Kulipuliwa kwa mabomu huko Madrid
Hispania mwezi March 2004 na watu 190 waliuawa na 1400 kujeruhiwa, hotel ya
Paradise mjini Mombasa ambapo wayahudi kadhaa waliuawa kwa bomu la kujitoa
muhanga.
KAZI
KUBWA YA AL-QAEDA
Al-Qaeda kwa ujumla wanapigana
vita takatifu ulimwenguni iitwayo Jihad kama tulivyojifunza na wanafikiri kuwa
wao ndio watetezi wa kubwa wa tamaduni mila na dini ya kiarabu na mpango wao
mkubwa ni kutawala dunia na kuifanya dini ya kiislamu kuwa dini itakayotawala ulimwengu
ili kwamba ulimwengu uweze kuongozwa kwa mujibu wa Shariya (Sheriaza kiislamu)
Al-qaeda wanaiona Marekani na nchi
nyingine za magharibi kuwa ndio kizuizi kikubwa cha mpango wao kwa sababu wana
uhusiano na nchi nyingi sana ambazo al-qaeda wanaziona kuwa ni za kikafiri
Al-qaeda wanaamini kuwa kuweko kwa majeshi
ya Marekani huko Saudia ni aibu kwa ulimwengu wa kiislamu kwa sababu nchi hiyo
ina misikiti mikubwa miwili iliyo mitakatifu ukiwemo ule wa Mecca na Medina,
Bin - Laden amekwisha toa wito mara mbili (Fatwa) wa kuwaondoa wamarekani
katika ardhi hiyo takatifu, Fatwa ya kwanza
ilitangazwa mwaka 1998 kupigana jihadi kwaajili ya Wayahudi na Crusaders na
ikitangazwa pia kuhusika na kuwaua wamarekani na kuainishwa kuwa ni wajibu wa
waislamu kuwashughulikia watu hao kokote waliko, aidha tukio la kigaidi
linahusishwa na ulipaji kisasi kwa uvamizi wa maeneo mbalimbali ya kiislamu
ikiwa ni pamoja na Bosnia, Chechnya, Timor ya Mashariki, Philippines, Sudan na
Somalia.
Baada ya tukio la September 11 Rais wa
Marekani wakati huo George W. Bush aliamuru majeshi kuivamia Afaghan na kufanikiwa kusambaratisha kambi ya mafunzo
ya magaidi, na makao makuu ya kijeshi katika inchi hiyo, maelfu ya watu
waliuawa pamoja na viongozi wakubwa wa ugaidi ingawaje al-Qaeda wameendelea
kuonyesha uwezo wao wa kuendelea na mashambulizi ya kigaidi kupitia vikundi
mbalimbali ulimwenguni
Mwaka 2002 kwa mfano al-qaeda walihusika
na matukio ya mauaji huko Tunisia, Pakstan, Jordan, Indonesia, Kuwait,
Philippines, Yemen na Kenya katika mipango yao hujumuisha kuwashambulia
Australia, Ujerumani, na Israel, wengine ni wahandisi wa kifaransa na
wanaubalozi wa kimarekani wakati mwingine hujihusisha na utekaji nyara wa watu
kama waandishi n.k.
MTANDAO
WA AL-QAEDA DUNIANI
Kwa mujibu wa uchunguzi wa ndani
sana kuhusu watu kadhaa waliokamatwa kwa kuhusika na ulipuaji wa balozi za
Marekani nchini Kenya na Tanzania inaaminika kuwa al-qaeda wana mtandao mkubwa
wenye mawasiliano kutoka ngazi ya juu hadi ya chini na kwa kina na marefu huku Osama
Bin Laden akiaminika kuwa ndie Jemedari mkuu wa Mtandao huu yeye kama amiri
jeshi wa mtandao kazi yake ni kushughulika Kiroho,kimipango na muongozo na
mbinu za mikakati ya kutekeleza maswala ya kigaidi hivyo anaheshimika sana na
ndio mwenye kutoa mipango na amri za utekelezaji wa kigaidi hata kwa makundi
mengine ( Meillis al – shura) Mtoa ushauri wenye kujenga.Vikundi vingi sana vya
kigaidi hata vinavyoitwa kwa majina mengine vinafanya kazi chini ya Mtandao huu
wa Al-qaeda.
ASILI
YA AL-QAEDA
Vita vya Afghan na soviet
Pichani chini Mujahideen
(Wapiganaji wa kiislamu) wakiwa wamesimama juu ya Helcopter waliyoiangusha
chini huko Afghan mwaka 1979 Mwana milionea wa Saud Bin Laden alisaidia kifedha
kujengwa kwa makambi ya mafunzo ya Mujahedeen waliopigana kinyume na majeshi ya
Kisoviet walipoivamia Afghan na walikuwa wakifunzwa kutoka majeshi ya Marekani
kupitia shirika la kijasusi la kimarekani Central Inteligence Agence (C.I.A),
Maelfu ya wapiganaji hawa walijiunga na Al-Qaeda baada ya vita na Soviet na kuwa mtandao mkubwa wa
kigaidi duniani,
Al-Qaeda
kwa asili walianza mwaka 1979 mara baada ya uvamizi wa majeshi ya kisoviet
Union of Soviet Socialist Republic (USSR) Bin Laden alikuwa miongoni mwa maelfu
ya wanajeshi wa kiislamu waliojitoa
kuikomboa Afaghanstan ili kuwafukuza wavamizi wa kisovieti Bin ladeni
mwana wa mwana milionea wa Saud Arabia
alikuwa miongoni mwa maelfu wa vijana wa kiislamu waliojitoa kwenda kuikomboa Afghan alijistawisha kama mlezi mkuu wa wana jihad wapiganaji wa vita
takatifu wengine ni pamoja na shekh Abdullah Azzam mwanzilishi wa jumuiya ya
Makhtab al-khidamat MAK (Yaani Ofisi ya huduma) ilikuwa mwaka 1984 ambayo
ilihusika na uandaaji wa makamanda wa kijeshi wa kimataifa watakaoipigania
Afghan inasemekana ofisi hii iliandaa na kufundisha na kuwalipa fedha mujahedeen kati ya 10,000 na 50,000 ambao
walitokea inchi mbalimbali zipatazo 50 karibu nusu ya wanachama wa MAK
walitokea Saud na wengine walitokea Algeria,Misri, na katika inchi za kiislamu kama Yemen, Pakistan, na Sudan na kutokana na uwezo mkubwa wa Bin Laden na
ushawishi wake na umaarufu na utajiri wengi walimsikiliza na kumtii kama
kamanda mkuu. Mwishoni mwa vita vya Afghan Bin Laden na Azzam waligombana kama
kundi lake liendelee kufanya kazi ya ukombozi kwaajili ya Afghan aui kwaajili
ya ulimwengu mzima , Lakini Bin laden alipata nguvu kubwa kwa sababu ya kuwa na
imani kali ya kiislamu na theolojia aliyokuwa nayo iliyochangiwa na ushawishi
wa Sayyid
Qutb, mwanzilishi wa kundi la Muslim
Brotherhood huko Misri na Maulana Sayed Abdul A’la Maudoodi mzaliwa wa
India na mwandishi wa habari mwenye
akili sana aliyehamia toka Pakstani 1947 ambao mafundisho yao yalikazia kuhusu
Jihad kama swala Binafsi linalo takiwa kutekelezwa na kila Muislamu wa kweli na
kuwa kamwe Uislamu hauwezi kutenganishwa na utawala wa kiserikali na kuwa
mataifa ya magharibi ni mataifa adui wakubwa wa Uislamu. Na ingawaje al-qaeda
ilianza kupata sura kati ya mwaka 1987 na 1988 ni baada ya Azzan kuuawa mwaka
1989 ndipo al-qaeda walijitenga na MAK na kuwa Wana jihad mpaka sasa na mwaka
huohuo majeshi ya soviet yalijitoa Afghan na ndipo al-qaeda walipata nguvu
kubwa miongoni mwa inchi za kiislamu huku Bin laden akiwa na umuhimu mkubwa na
matukio ya kusambaratika kwa USSR yalifuatia na Ndipo Bin Laden alisema kuwa
sasa USA nayo ni lazima iondoke katika inchi za kiarabu na ulimwengu wa
kiislamu na kuuondoa umagharibi katyika inchi zao.
KUKUA KWA AL-QAEDA.
Mwaka
1989 Bin Laden alirudi SaudArabia na kupinga vikali kuweko kwa majeshi ya
Marekani nchini saud na 1991 wakati wa vita vya ghuba ya uajemi aliushutumu
vikali hadharani utawala wa kifalme kwa kuwakaribisha makafiri kutumia ardhi
yake na april 1991 Vita ilipomalizika Bin Laden alikwenda Paksatan, 1992
alikwenda Sudan ambapo alikaribishwa na utawala National Islamic Front na
kiongozi wake Hassan al-turabi ambaye alistawisha uislamu wenye msimamo mkali
dhidi ya shariya
Mwaka 1991 mpaka 1996 Bin Laden alikuwa
kimya akijishughulisha na kuimarisha mtanadao wa al-qaeda kimataifa na
kufanikiwa kuwa na matawi katika inchi kama 45 huku wakifadhiliwa sio tu na
Osama mwenyewe bali pia na vyanzo vingine vya kifedha vinavyojihusisha na
uchangiaji wa jihadi
TUKIO LA
SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA SEPTEMBER 11.
Hili hapo juu ndilo tukio halisi
la September 11 2001, timu ya magaidi wapatao 19 wakiwa na mpango wa kujitoa
muhanga walifanya shambulizi la kihistoria na kuua watu 3000 pichani ndege
zilivyoweza kushambulia majengo ya minara miwili ya kituo cha kibiashara cha
kimataifa katika picha ya pili na picha kwanza ni majengi hayo yalivyokuwa yakionekana
kabla ya shambulizi Picha kwa hisani ya maktaba ya mchungaji Innocent Kamote
Ingawa haijulikani ni wapi mpango
wa shambulizi la September 11 lilipangwa lakini inavyoonekana mpango wa
kuyashambulia kwa ndege majengo haya kule new York na Washington DC, ulipangwa
mwishini mwa 1999 wakati wa Mohamed Atta kiongozi wa kigaidi ambaye pia alikuwa
ni Pilot aliyechagua ndege mbili ambazo zingetumika kwa shambulizi hilo
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya shirika la kijasusi la Marekani CIA
inasemekana kuwa Pilot aliyeongoza ndege hizo hakuwa na sifa
ya kazi hiyo, wala wazo la kuwa angeuawa hii ni kwa mujibu wa mkurugezi
wa shirika hilo George Tenet magaidi walihakikisha kuwa hakuna mtu anafahamu
mpango huo na kuhakikisha kuwa habari za mpango huo wa mauaji haujulikani na
mtu Bin Laden aliamini kwa kufanikiwa
kwa mpango huo kungepelekea Marekani kuporomoka kiuchumi na kuwatishia sana
raia wa marekani na serikali yake, Bin Laden aliita Marekani kuwa ni chui wa
makaratasi na kuwa pigo hilo lingebadilisha msimamo wa Marekani kuhusu mataifa
ya kigeni katika wizara yake ya mambo ya nje
na kuwa lengo la al-qaeda lingefanikiwa ikiwa ni pamoja na majeshi ya
Marekani kuondoka Saud na Israel na kuwa Marekani ingeacha shughuli zake za
kibiashara katika ulimwengu wa Nchi za Kiarabu
MATOKEO YA SHAMBULIZI LA AL-QAEDA LA SEPTEMBER 11.
Kinyume
na matarajio ya al- qaeda Marekani ilipokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo
la kigaidi na kutangaza vita vya kidunia dhidi ya matukio ya kigaidi na
magaidi.Na kampeni kubwa za kijeshi za kushughulikia magaidi zilianza na
October 7 Mwaka 2001 Mashambulizi makali yalianza dhidi ya kityuo kikuu cha
kigaidi huko afghan na serikali ya Kitaliban kuondolewa madarakani na Novembr
2001 serikali ya kitaliban ilishindwa vibaya na kuondolewa madarakani, al-qaeda
wote walisambaratishwa vibaya na kuondolewa kabisa katika ngome yao huko afghan
ingawaje Bin laden na watu wake wa Karibu kama Ayman Muhamad Rabi al-Zawahin
walikimbia kukamatwa
Marekani
na washirika wake walifanikiwa kuzuia vyanzo vya kifedha vyote vyenye kusaidia
makunfdi mbalimbali ya kigaidi , sheria na miswada mbalimbali ya kupambana na
ugaidi zilipitishwa na kila taifa na kupelekea magaidi wengi kukamatwa zaidi ya
Mgaidi 1000 waliokuwa na uhusiano na al-qaeda walikamatwa katika inchi
mbalimbali na mpaka mwishoni mwa 2003 magaidi wapatao 3000 walikamatawa na huku
viongozi wengi wa mitandao ya kigaidi wakiuawa au kukamatwa mmoja wa watu
waliofanikiwa kukamatwa ni Khalid Shaikh Muhamad ambaye alikuwa ni moja ya
viongozi wa ngazi ya juu sana wa mtandao wa al-qaeda ambaye alisaidia kuongoza
tukio la September 11 huko Pakstan.
Ingawaje
al-qaeda wamedhoofishwa kwa kiasi kikubwa bado waliendelea na matukio ya
kigaidi ambapo mwaka 2002 walifanya shambulizi huko Tunisia, Kuwait na Kenya na
2004 walifanya shambulizi huko Spain wakijitutumua kuwa bado hawajasambaratika
hata hivyo inaaminika kuwa mashambulizi mengi yalikuwa yamekwisha kukusudiwa
zamani hata kabla ya tukio la September 11.
HALI YA BAADAYE YA AL-QAEDA.
Mkanda
wa sauti inayosadikiwa kuwa ya Bin Laden uliorushwa katika vyombo vya habari
November 2002 uliokuwa ukiwasifiwa wote wanaopingana na desturi za kimagharibi
baada ya kushindwa 2002 ulionya kuongeza vitosho kwa mashambulizi zaidi ya
kigaidi, wakati huu Bin Laden alionekana kuitishia Australia,
Beligium,Uingereza ,Ufaransa, Ujerumani na Hispania nchi zote ambazo zilijihusisha na muitikio wa kuishambulia
al-qaeda na kuisaidia Marekani katika vita dhidi ya ugaidi
Mwezi
April 2004 alitoa mkanda mwengine ukiwaelekeza al-qaeda kuhakikisha kuwa
wanaichana Marekani vipande vipande na washirika wake ulaya na ilitoa onyo kwa
watu wa ulaya kuacha kuushambulia Uislamu na nchi za kiislamu au kuingilia
maswala yake na alisema ukweli utathibitika pale ambapo askari wa mwiosho
ataondoka katika nchi hizo ikiwemo Afghan
na Iraq, kwani Marekani na washirika wake waliiondoa serikali ya
kitaliban mnamo 2001 na Kumuondoa Madarakani Rais Saddam Hussein mwezi April
2003
Kuachiliwa
kwa mkanda huo kulifuatia tukio la mashambulizi ya mji wa Madrid Huko Hispania
mwezi March 11 2004 ambapo watu 190 waliuawa na 1400 kujeruhiwa, na serikali ya
Spain iliwakamata baadhi ya washukiwa wanaohusiana na mtandao wa al-qaeda Jaji wa kihispania alithibitisha mtandao huo
kuhusika kufuatia Spain kujiunga na majeshi ya washirika na Marekani
na kupeleka vikosi vyake huko Iraq na hivyo kuzilzzimisha inchi za ulaya
kujiondoa katika mpango wake wa kuisaidia marekani, Spain baada ya kupeleka
kikosi cha askari 1300 baadaye kulitokea shambulizi linguine jambo
lilolopelekea serikali iliyofuata ya Spain kuondoa vikosi vyake toka Iraq Hata
hivyo inchi nyingi za Ulaya zilikataa mpango huo na kusema kamwe hawawezi
kukubaliana na Magaidi
Maswala
mengi kuhusu tukio la September yalieleweka vema bada ya uvamizi wa Marekani
kwa Iraq ambapo ilibainika wazi kuwa Iraq haikuwa na uhusiano na kundi hilo
hususani baada ya kuondolewa madarakani kwa serikali ya Saddam Hussein, Baadaye
al-qaeda walijaribu kujihusisha na matukio ya uchaguzi wa Rais wa Marekani
mnamo 2004 Laden alitoa mkanda akiwaonya
waamerika kuwa usalama wao haumo mikononi mwa chama cha Democratic cha mgombea
John Kerry, wala Bush au al-qaeda
usalama wao uko katika mikono yao ingawaje uchunguzi ulibaini kuwa mkanda huo
unakosa sifa za Osama mwenyewe kwani nhakuwa anazungumza kama Osama mwenyewe
mwenye jazaba na kejeli nyingi na kubainika kuwa ulitengenezwa tu na waarabu wanaopinga sera za marekani kwa mashariki ya
kati ,Baadaye mkanda mwingine wa video wa Osama ulifuatiwa na ule wa
Zawahiri na huende ulirekodiwa kabla ya
uchaguzi ambapo bwana al- Zawahiri
alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Marekani hauna tija kwetu mpigie kura
yeyote unayetaka Bush, au Kerry au Shetani mwenyewe hili halituhusu
linalotuhusu sisi ni kukaliwa kwa ardhi yetu na makafiri, mnamo 2004 CIA
walihisi kuwa huenda al-qaeda wana lengo la kum iliki nyuklia kufuataia
kuhisiwa kuwa engineer wa kipakistan mmoja kutoa taaluma kwao kuhusu silaha
hizo.
Ndugu
msomaji wangu vyovyote vile iwavyo huu ndio msimamo wa mafundisho ya Quran
ulivyo na unaopelekea kuweko kwa
amakundi ya kigaidi duniani hivyo pamoja
na jitihada za kimarekani na washirika wake kupambana nao ni muhimu kufahamu
kuwa fundisho la ugaidi liko kwenye Quran
na ugaidi unaweza kuendelea kuweko maadamu uislamu uko na Quran iko
ndugu mpendwa hii ni changamoto kubwa ulimwenguni hata kwa waislamu wenyewe
kuhakikisha kuwa wanakuwa na tafasiri sahii ya Quran hasa kwa kuisoma injili
inayosisitiza upendo na kuachana na mitazamo ya kizamani inayopelekea kuuawa
kwa watu wengi wasio na hatia unajua kwa nini ugaidi unaruhusu kuua hata
waislamu wenzako ambao wanaonekana kuwa na misimamo ya wastani na ndio maana
nasema kuwa hata waislamu wana changamoto kubwa la tafasiri sahii isiyo na
unafiki kuhusu Quran.
Nilipotembelea Marekani Mwezi Juni 2014 na wanafunzi wangu Tulifika mahali Yalipokuwepo Magorofa ya World Trade Center Mahali hapa sasa panaitwa Zero Ground na pana visima na majina ya watu zaidi ya 3000 waliouawa kwa misigi ya tofauti za kiitikadi (Katika picha kutoka Kushoto Yohana Komba, Onstard Mashauri, Herbeth Gumbo, Imani Peter Mngazija, Willium Biniventure Kifutumo, Mimi Rev. Innocent Kamote na Author Chikoka Picha na Maelezo kwa Hisani ya Mwandishi wa Makala hii Rev. Innocent Kamote)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni