*******************************************************************
Somo;
Majukumu ya kiongozi wa kanisa
Kufahamu
majukumu ya kazi za kiongozi katika kanisa ni mojawapo ya Jukumu muhimu kwa
kiongozi wa kanisa, Mara nyingi imetokea Viongozi wengi wa makanisa ya kiroho
hawajui majukumu yao na hii inachangia kwa kiasi Fulani kutokuyafikia malengo. Tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia mambo mawili yafuatayo
Viongozi
wa kanisa ni wachungaji.
Majukumu
ya kichungaji ya kiongozi wa kanisa
Viongozi wa kanisa ni
wachungaji.
Viongozi wa makanisa ya nyumbani au cells na
Viongozi wengine woote na wasaidizi wao woote ni wachungaji wa kondoo wa Mungu,
Hawa ni wachungaji wanaotenda kazi chini ya Mchungaji hata ingawa hawaitwi kwa
jina hili, lakini majukumu yao wanayoyafanya ni ya kichungaji, katika mpango wa
Mungu kila mtu ana husika katika utendaji kama makuhani wa Mungu Ufunuo 1;5-6,
1Petro 2;5,9 kama ikiwa kila mtu aliyeokoka Maandiko yanamuita kuhani ni zaidi
sana mtu anapokuwa kiongozi katika kanisa Viongozi katika kanisa ni wachungaji
wanaotenda kazi chini ya Mchungaji na kumsaidia katika huduma za kichungaji
Majukumu ya kichungaji
ya kiongozi wa kanisa.
Viongozi wa kanisa kama ilivyo kwa
Mchungaji wana wajibika kufanya kazi ya uiunjilisti uchungaji na ualimu katika
eneo lao walilopewa na Mungu leo tutachukua Muda kujifunza majukumu mbalimbali ya kiongozi wa yanayohusiana na uinjilisti na ualimu na
uongozi kwa ujumla wake
- Kuwafahamu Kondoo kwa sura na majina Yohana 10; 2-3.
Ni wajibu wa kiongozi katika kanisa
kuwafahamu kondoo wake kwa majina na sura, kadiri kanisa linavyokua na
kuongezeka lazima kanisa liwe na mfumo unaoruhusu watu kujulikana kama kuwa na
makanisa ya nyumbani ambapo kiongozi anapaswa kuwatambua kwa sura na majina ,watu
hupenda kutambulika na hujisikia salama pale
anapokuwa anatambukiwa Kanisani hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwatambua
watu wake, na kutokana na kuwafahamu kwa majina na sura inakuwa rahisi kuwaombea kwa kuwataja majina
yao Viongozi wanapaswa kuwafahamu wale Viongozi wengine walio chini yao pia tunapaswa kujua mahudhurio yao katika
ibada zote za mafundisho siku ya bwana na kadhalika
- Kuhubiri na kufanya uinjilisti Marko 1;38-39;Matendo 20;27.
Kiongozi yeyote wa kanisa kwa ngazi
yoyote ni lazima awe muhubiri na
anawajibika kuwahamasisha watu walio chini yake kuwa na furaha ya kuona watu
wakiokolewa na kuongezeka katika kanisa
tuhakikishe kuwa tunawahubiri watu na wageni wanaokuja katika kanisa
letu na kuwaaalika katika ibada mbalimbali za kanisa ,aidha kama ni kuiongozi
wa cell au kanisa la nyumbani hakikisha kuwa unalihubiri eneo lote
linalokuzunguka na kuhamasisha watu kuhudhuria ibada zote aidha tunapofahamu kuwa Fulani na Fulani
hawakuhudhuria ibada ni muhimu kuwatembelea na kujua ni kwanini
hakuhudhuria na kutoa msaada unao
hitajika kwa pia kufanya ufuatiliaji kwa
washirika wachanga kiroho na kuwalisha kwa neno na mafundisho,kiongozi anapaswa
kukumbuka kuwa mfano au kielelezo kwa watu aliopewa kuwaongoza.
- Kufundisha au kulilisha kanisa. Matendo 20;28.
Lisha kondoo zangu huu ni wito kwa kila kiongozi wa kanisa kwa msingi
huo ni wajibu wa kiongozi wa kanisa la nyumbani n.k kujiandaa na kujitayarisha
mapema kwa habari ya somo atakalolifundisha
kila siku ya ibada za makanisa ya nyumbani au katika vipindi vya ibada
za idara n.k. Masomo yanayopaswa kufundishwa ni yale yaliyo maalumu kwa ajili
hiyo au yale yanayofundishwa Kanisani ni hatia kuleta mafundisho mageni 2Yohana
1;9-11,Tito 1;9 kufundisha kwetu hakuna budi kuwe na malengo ya kuondoa au
kurekebisha matatizo yaliyopo katika
sehemu zetu za maongozi tabia kama masengenyo, kuchelewa ibada au kutohudhuria
n.k kumbuyjka kuwa inahitaji maombi na maandalizi ya kutosha kabla ya kufundisha somo au siyo kondoo
watajkuwa hawashibi na matokeo yake
hawatavutiwa kuendelea kuja katika
katika kipindi husika.
- Kuwatunza kondoo.
Ni wajibu wa kiongozi kufanya kazi
ya msamaria katika kutunza kondoo wake Luka 10;30-37 ni lazima kuwatafuta
waliopetea na kujua kuwa ni kwanini hawaji katika ibada,lazima tumuombe Mungu
atupe karama na vipawa ili kuwahudumia
watu wake kuomba kwa ajili ya uponyaji kwa ajili ya wote wenye shida za magonjwa
na kuwafungua waliovunjika moyo kwa kuwapa neno la Mungu la kuwaita moyo
Ezekiel 34;1-2,4-6.
- Kuwatembelea washirika na kujua hali zao za kimwili na kiroho.
Yeremia 23;1-2 matendo 15;36.
Kiongozi yeyote wa kanisa anatakiwa kuifahamu kila nyumbay a mshirika
wake na kuwatembelea mara kwa mara na
waqkati mwingine kwa kushtukiza ili ajue hali ya kimwili na kiroho ya washirika,
bila matembezi ya jinsi hii ni rahisi
kumkuta kondoo amejerihiwa iwapo kuna
taarifa ya tabia mbaya ya mshirika awaye yoote
zifanyiwe uchunguzi wa kina na wa haki kisha zitafutwe njia za kumsaidia
kiroho endapo liko juu ya uwezo wako likabidhio kwa Mchungaji kumbuka katika
kuwatembelea washirika pia ni muhimu kuweka kipaumbele kwa wale walio wachanga
,wageni na wenye kuugua au waliopatwa na misiba na matatizo mbalimbali haita
kuwa busara sana kwa mshirika aliyekomaa kiriho kuwa na madai ya kutembelewa na
badala yake wao nao washirikiane na Viongozi katika kuifanya kazi ya
kuwatenbelea washirika na kuwaita moyo.
- Kutoa ushauri kwa kondoo. Mithali 20;18;12;15.
Mengi tunayoletewa na kondoo kutaka
ushauri mara nyingi ni yale yaliyo mepesi kuyatolea ushauri hata hivyo Mengine
huwa magumu na mtu unapoletewa tu ni rahisi kuona moyoni kuwa hili limenizidi
kimo katika mazingira kama hayo hilo
lipeleke kwa kiongozi wako wa juu na katika kanuni za kutoa ushauri ni vizuri
uwe mwepesi wa kusikia kuliko kusema Yakobo 1;19 Roho wa Mungu hudondosha
ushauri kwetu tunapokuwa watu wa kusikia au katika hali hii ya utulivu, na wakati huo huo zingatia kuwa ni Kinyume na
mapenzi ya Mungu kutoa siri za matatizo ya mtu aliyekuomba umpe ushauri Mithali
25;2,9.
- Kumlinda Mchungaji 1 Samuel 26;16
Viongozi katika kanisa ni wawakilishi wa Mchungaji na wana wajibu wa
kumlinda Mchungaji na kuhakikisha kuwa kila roho ya uasi inayoinuka kinyume na Mchungaji
inashughulikiwa ipaswavyo na kuitolea taarifa lazima kiongozi wa kanisa awe na
moyo wa kiuchungaji Isaya 40;11,1Thesalonike 2;7 Bila moyo huu utendaji wetu wa
kazi utaingia dosari.lolote linalopungua katika karama hii ya kumtumikia Mungu
tumuombe Mungu atupe karama hizo za kutuwezesha kuifanya kazi yake aidha sivibaya kuwatumia wale ambao Mungu
amewapa karama hizo kutusaidia katika
kuwahudumia wale tunao waongoza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni