Mstari wa Msingi Wafilipi 1;29 “
Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo si kumwamini tu ila na kuteswa kwaajili yake
“
Kuchukiwa baada ya kuokoka
Baada ya kumuamini bwana Yesu na
kuanza kuukiri wokovu ulioupokea hadaharani, kutafuata kila aina ya kebehi
kutukanwa na kila namna ya kuchukiwa na ndugu walio karibu ni muhimu kuvumilia
mpaka mwisho kwani Yesu alituambia kuwa tukichukiwa kwaajili yake tuna heri Mathayo
10;22.
Katika hali ya kawaida ungefikiri kuwa ndugu mume au mke au wazazi
wangelifurahia uamuzi wako wa kuokoka lakini jambo la kushangaza ni kuwa
haitakuwa hivyo wengi wataanza kusema umeiacha imani yako ya kwanza uliyozaliwa
nayo? Au dini ya ukoo wako hali inaweza kuvuruga sana hata mahusiano yako na
mumeo yanaweza kuingia utata ni muhimu kufahamu kuwa si kila wakati watafurahia
watu uamuzi wako ndio maana Yesu alisema hakuja kuleta amani duniani Luka
12;51-53.
Wakati mwingine kwa sanbabu ya
wokovu amani itaondoka utashangaa unaweza kufanyiwa hata vikao na kuanza kutishwa au kuteswa kwaajili ya
bwana na mwokozi wako Yesu Kristo hayo yasikukatishe tamaa fahamu ya kuwa
tumepewa si kumwamini tu bali na kuteswa kwaajili yake wanaweza kukupa kila
aina ya majina hata kuitwa mchawi isikusumbue kwani hata Yesu aliitwa kuwa
anatoa pepo kwa kutumia mkuu wa pepo Mathayo 10;24-25,28 hayo yatatupata mara
baada tu ya kulikubali neno la Mungu
Fahamu kuwa wewe si wa ulimwengu
huu na hivyo ndio maana ulimwengu unakuchukia ungelikuwa wa ulimwengu huu
ulimwengu ungekupenda Yohana 17;14 kwa
msingi huo ni muhimu kuwa tayari kwa mateso ya namna yoyote ile na kuvumilia
huku tukihakikisha kuwa hayatupotezei wokovu wetu Ufunuo 3;11
Biblia inatufundisha kuwa watu
wanaokwenda mbinguni ni lazima wapitie dhiki adha na mateso mengi ndio maana mitume
waliwafundisha wanafunzi wao mapema kujua hayo Matendo 14;22 Imetupasa kuingia
katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi, aidha katika mafundisho yake
Bwana Yesu alisema Heri weri wenye kuudhiwa kwaajili ya haki maana ufalme wa
mbinguni ni wao Mathayo 5;10 yeyote
ambaye amechagua maisha ya utauwa yaani maisha ya wokovu lazima ataudhiwa soma
2Timotheo 3;12 dhiki hizi tumewekewa na
na tusifadhaishwe 1Thesalonike 3;3, Petro anasema katika 1Petro 3;14 Lakini
mjapoteswa kwaajili ya haki mna heri kwa hiyo tusiogope kutisha kwao
Mtu anayekata tamaa haraka
kwaajili ya dhiki hizi anafananishwa na mbegu zile zilizoangukia juu ya mwamba
na kwa kukosa mizizi ikitukia dhiki wanachukizwa soma Mathayo 13; 20-21,
tunapaswa kuwa wavumilivu na kamwe hatupaswi kuwajibu vibaya wala kwa
hasira kwa sababu hawajui walitendalo
wewe subiri thawabu yako ambayo ni kubwa sana Mbinguni Mathayo 5;11-12, Ni sifa kubwa mbele za Mungu kupigwa makofi kwaajili ya wema 1Petro 2;19
dhiki hizi tulizo nazo sisi ni nyepesi na za Muda tu ukilinganisha na thawabu kubwa ambayo Mungu
atakwenda kutulipa huko Mbinguni 2Wakoritho 4;17-18 inatupasa kufurahi tunaposhiriki mateso kama
Kristo ili siku akifunuliwa utukufu
mkubwa wa Mungu na roho wake anatukalia
hii ndio maana ulimwengu unatuchukia 1Petro 4;13-14 trukumbuke kuwa
yanayotupata yaliwapata pia wale waliokuwa wametutangulia na biblia inatutaka
kuchukua manabii waliotutangulia kama mfano wa kustahimili mabaya na wa
uvumilivu Yakoboo 5;10, mitume wengi waliuawa kwaajili ya Kristo katika
historia za kanisa inaonekana kuwa Petro aliuawa wakati wa mtawala aliyeitwa
Nero kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu,huko Roma Andrea alisulubiwa huko
Misri na Simon Mkananayo aliyeshurutishwa kuubeba msalaba wa Yesu naye alisulubiwa na wengine wengi walipata mateso ya namna
mbalimbali kweli ufalme wa Mungu
unapatikana kwa njia ya dhiki nyingi nasi inatupasa kuwa wavumilivu sana hata
kama kila mtu atatuchukia iwe ni kazini ama popote pale kumbuka kuwa taji kubwa
inakungoja
Kumbuka kuendelea kuwaombea wale
wanaotutesa ili kwamba Mungu awaokoe na pia wakati wote huu wa mateso
shirikisha wenzako katika Bwana ili mshirikiane katika kuomba kwani kiungo
kimoja kikiumia katika Kristo ni viungo vyote Jipe moyo kwani ushindi ni lazima
Ubarikiwe sana
Maana mmepewa kwa
ajili ya Kristo si kumwamini tu ila na kuteswa kwaajili yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni