Utangulizi;
Mara baada yakuwa Tumeokoka ni
muhimu kufahamu kuwa kuna kitu cha ziada kimetokea katika ulimwengu wa roho, Kuokoka
kwa mtu mmoja kuna thamani kubwa sana Machoni pa Mungu na malaika zake akionyesha
umuhimu wa kile kinachotokea katika ulimwengu wa roho kwa mtu kuokoka Yesu
anafundisha hivi soma (Luka 15;10 na
Luka 15;7)Hiki ndicho kinachotokea mtu anapotubu dhambi zake kwa kumaanisha
kuziacha kabisa.
Mwana mpotevu
Hata hivyo ni Muhimu kufahamu kuwa katika
Maamuzi yako haya upande wapili wa adui yaani kwa Shetani na malaika zake
hakuwezi kuwa na Furaha badala yake kutakuwa na Huzuni kubwa na mipango
madhubuti ya kuhakikisha anakurudisha nyuma ili uendelee kuwa wake na
kumtumikia katika dhambi hapa atatumia kila njia iwezekanayo kukurudisha nyuma
hivyo ni lazima uzingatie mambo ya msingi yafuatayo;-
1. Anza kufuata maagizo sahihi kutoka katika Neno la Mungu;
Wanadamu wa kawaida hasa watu wasiookoka
watatumiwa kukukatisha tamaa kuhusiana na uamuzi wako huu mpya watakuita
umepotea jambo la kushangaza sana kwani ulipokuwa dhambini hakuna mtu aliyepiga
kelele kukuonya uache lakini mara baada ya wokovu na toba na kuyaacha yote
watatokea watu kukuambia kuwa umepotea! Lazima ukabiliane na changamoto hii
ukijua ni kazi ya shetani ndani yao na
kuwahurumia kwani wao ndio wamepotea soma (2Wakoritho
4;3-4) ni lazima kwako kujifunza neno la Mungu na kujua kuwa Mungu ana mawazo
gani kwako; akieleza mtazamo wa Mungu kwa mtu aliyetubu Yesu alifundisha
yafuatayo;-
2. Wewe ulikuwa Umepotea sasa Umeonekana;
Ilivyo ni kwamba kabla ya
uamuzi wako wa toba wewe ndiye ambaye ulikuwa umepotea, ulikuwa ni mwanakondoo
mpotevu katika kundi la Kristo Hivyo Muda wote tangu uzaliwe alikuwa
akikufuatilia apate kukuokoa Wachungaji wako na viongozi wako wa dini
hawakukuambia ukweli bali walizidi kukupoteza hata ukasahau kuwa pumziko lako
ni Yesu Kristo, Yeye aliugua na kuhuzunika kwa upotevu ule akiwalaumu viongozi wako kwa kusaidia
kukupotezaa angalia (Yeremia 50;6)Yeye
Yesu alikuja duniani kwa kusudi la kutafuta na kuokoa kile kilichopotea soma (Luka 19;10).
3. Wewe ulikuwa Umekufa sasa Umefufuka;
Mtazamo wa kibiblia ni kwamba mtu awaye yote
ambaye anaishi dhambini katika hali ya kuzaliwa
yaani kwa kurithi dhambi mtu huyu ni Mfu mbele za Mungu haijalishi mbele
za wanadamu wenzake anaonekana ni
maarufu kiasi gani Mbele za Mungu hakuna cha Umaarufu kwani kama ni mtenda
dhambi kwa Mungu anakuwa ni mfu tu, Mtu yeyote anayeishi katika dunia hii
kwakufuata kawaida zake anamfuata mfalme wa uweza wa anga hili yaani shetani
ambaye hutenda kazi ndani ya wote wanaoasi maagizo ya Mungu soma (Waefeso 2;1-3),hivyo mtu anapookoka
sasa ndio anakuwa hai (Waefeso 2;4-5).
Tangu
sasa jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima.
Siku ile uliyokata shauri na kuchukua uamuzi wa kutubu na kuacha dhambi
ni siku ya wokovu wako ni siku ya kuikumbuka sana katika Maisha yako licha ya
kuwa siku ile Mbingu zilishangilia pia jina lako limeandikwa tangu siku ile
katika kitabu cha uzima Soma (Ufunuo 20;
15) Hivyo mpango wowote wa kuacha wokovu na kurudi dhambini ni kujifuta
mwenyewe kenye kitabu kile cha uzima Hivyo basi si busara kusababisha huzuni
mbinguni kwa kurudi nyuma, (Luka 15; 32).
Mtu asikutaabishe kwani kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe (Galatia 6; 5);-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni