**************************************************************
Somo; Wito wa kuwaongoza Kondoo.
Leo Tunaanza kujifunza mfululizo wa masomo yahusuyo
shule ya uongozi kwa kujifunza somo hili la msingi “Wito wa kuwaongoza kondoo”Tutajifunza
Somo hili kwa kuligawa katika vipengele vitano vifuatavyo;-
·
Watu
waliookoka huitwa Kondoo
·
Mungu
ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo
·
Wachungaji
wanadamu
·
Jinsi
isivyowezekana Mchungaji kuongoza kondoo peke yake
* Watu
waliookoka Huitwa Kondoo.
Watu waliookoka huitwa kondoo (zaburi 79;13;100;3;Yohana10;27-28)Kwanini wanaitwa kondoo,Kondoo ni
wanyama wasioweza kufanya lolote bila kuongozwa au kupewa msaada wa Kiroho,wao
hutembea wakitazama chini na kuiangalia miguu ya kiongozi wao yaani Mchungaji
wao Kondoo wanahitaji Malisho na kunyweshwa maji (Mwanzo 29;7,Yohana 10;2-4).Kondoo
watatulia mahali Fulani wakingoja Maelekezo ya Kiongozi wao tofauti na Mbuzi au
wanyama wengine na kutafuta Malisho
wenyewe nk.Siyo hilo tu kondoo ni rahisi sana kuvamiwa na wanyama wengine
wakali na kuuawa bila kujitetea kwa lolote
hawana mbio kama wengine wala viungo vya kujitetea kama pembe kali
nk.hivyo maisha ya kondoo yanahitaji
sana Mchungaji au kiongozi Kadiri mchungaji
wao alivyo shujaa ndivyo wanavyo faidika, mchungaji akiwa mtu mbaya nao
pia Hudhurika (1Samuel 17;34-35, Yohana
10;11-12)Hivyo maisha ya watu waliookoka yanatutegemea sana sisi viongozi
Tukiwa wema kondoo wataishi maisha Mazuri ya kupendeza(Yeremia 50;6;Ezekiel 34;5-6)
Kilio cha kondoo wakati woote ni kupata kiongozi wa kuwaongoza wao
Hulia
wakati wote wakisema ni nani atakayeniongoza hata Edom(zaburi108;10)Bila kiongozi
watu waliookoka wanaweza kufanya yaliyo mema machoni pao wenyewe na
kumhuzunisha Mungu. (waamuzi 21;25).
* Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa Kondoo.
Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo
ambao pia ndio kanisa ni kondoo zake kanisa ni mali yake (Waebrania 13;20;1Petro 5;4;Zaburi 23;1-3).Mungu kama mchungaji mkuu
wa kondoo,Yeye ndie Kiongozi mkuu wa kondoo wake na maongozi yoote ya Kondoo
hutokana na neno lake(Kutoka
13;17;Yohana8;47;Zaburi 119;9)hata hivyo ingawa Mungu ndiye Mchungaji mkuu
wa kondoo katika mpango wake wa Uongozi ameweka wachungaji wanadamu ambao
hufanya kazi pamoja na Mungu(1Koritho
3;9).
*
Wachungaji wanadamu.
Katika
mpango wake Mungu anawaongoza kondoo wake kwa kuwatumia wachungaji wanadamu(zaburi 78;70-72;2Samuel 5;1-2, Zaburi 77;20
Kutoka 15;22 Hesabu 27;15-21 Yohana
21;15-17).Mungu huwatumia wachungaji wanadamu hawa kufanya kazi ya
kuwaongoza kondoo kwa maelekezo ya neno lake(Kutoka 32;34)Hata hivyo uongozi wa wachungaji hao wanadamu wanadamu hufikia mpaka wanapokuwa na
kundi kubwa la kondoo nao huitaji wanadamu hawa wengine wengi wa kutenda kazi
pamoja nao
* Jinsi isivyowezekana Mchungaji kuongoza
kondoo Peke yake.
Kadiri
kanisa linavyoongezeka kunakuwa na kundi kubwa la kondoo wanahohitaji
uongozi.kiongozi mmoja hata angekuwa na
uwezo Mkubwa namna gani huelemewa na kushindwa kukidhi mahitaji ya uongozi wa
kondoo wengi, matokeo yake kondoo wengi hujisikia upweke kwa kukosa msaada wa
uongozi na matokeo yake hutawanyika na kuliacha kanisa hilo na kutafuta mahali
Pengine wanapoweza kupata uongozi wa maisha yao lakini wengine kwa kukosa
uongozi hurudi nyuma na kuacha wokovu(Waamuzi 18;1,30-31). Kiongozi Musa alipokuwa amewaacha kondoo bila kiongozi
,pale alipopanda mlimani Sinai kupokea amri kumi za Mungu huku nyuma kondoo walipoona hawana kiongozi maana kiongozi wao amekawia
kurudi walirudi nyuma na kuacha wokovu na kufanya machukizo makubwa mbele za Mungu.(Kutoka 32;1-8,15-24).Ufumbuzi wa Tatizo la watu waliookoka kurudi nyuma na kuacha
wokovu ni kuwa na viongozi wengi
wanaomsaidia Mchungaji.Kadiri tunavyokusudia kanisa letu kuwa na watu wengi
zaidi ndivyo inavyotupasa kuwa na viongozi wengi zaidi wa kumsaidia Mchungaji
kuliongoza kanisa,Viongozi hawa watakuwa wanashughulikia matatizo madogomadogo
ya kondoo na kuyapatia ufumbuzi na yale makubwa tu ndiyo yatakuwa yanapelekwa
kwa Mchungaji, Bila kufuata mpango huu Kanisa litadumaa na haliwezi kuongezeka
kiimani na kiidadi, Hata kama watu wengi watakuwa wanakata shauri,hawataendelea
katika zizi la kondoo kwa kukosa uongozi.Musa na watu wake waliukubali na
kuufuata mpango huu wa Mungu na matokeo yake walifanikiwa (Kutoka 18;13-26) Bwana amusaidie kila mmoja wetu ili tusiwe
kwazo la kukua na kuongezeka kwa kanisa.
*Wito wa Kuwaongoza kondoo.
Kilio
cha watu wa Mungu humfikia Mungu (Kutoka
2;23;Mwanzo 18;20-21,Yakobo 5;4)
Kondoo wa Mungu wanaohitaji uongozi
wanapolia wakisema nina atakayetupeleka
hata mji wenye Boma?ni nani atakaye tuongoza hata edomu (Zaburi 108;10).Kilio hiki humfikia Mungu,Kondoo hawa wana wasi wasi
wa kulala Porini na kuwa katika hali ya kushambuliwa na mbwa mwitu au simba
wanataka kiongozi atakaye wapeleka kwenye mji wenye Boma (yaani zizi la
kondoo).Kondoo hawa pia wanalia wakihitaji mtu wa kuwaongoza hata wafike Edomu nchi yenye
malisho mengi na maji mengi(Hesabu
20;14-19).Ndivyo kondoo wa Mungu wanavyolia pia,wanahitaji viongozi
watakaohakikisha wokovu wao unadumu na hawawezwi na shetani samba aungurumaye
na tena wanahitaji viongozi wa
kuwahakikishia wanapata malisho na kuangaliwa na kutunzwa ili wafurahie raha ya
Wokovu. Kilio hiki cha kondoo kikimfikia Mungu ,Mungu nae anatoa wito kwa watu
wake akitaka wajitoe kuwaongoza Kondoo yaani kiongozi wa kanisa,Mungu anauliza
Hapana hata mmoja wa Kumshika mkono? Miongoni mwa wana wote aliowalea(Isaya 51;18) Kwa sababu hiyo mungu anauliza
ni nani atakaye kwenda kwa ajili yetu?-Isaya 6;8 Isaya alisema Mimi hapa, sisi
nasi hatupaswi kumuachia mchungaji pekee kuifanya kazi hii peke yake na hivyo
tunapaswa kushirikiana nae katika kulitunza Kundi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni