Waamuzi
7:13 – 14
Moja ya waamuzi wanaotajwa kama
mashujaa wa Imani katika agano jipya, Gideon ni mmoja wao, anatajwa kama moja
ya watu waliotiwa nguvu na kufanywa kuwa Hodari na kukimbiza Majeshi ya wageni Waebrania
11:32-35, Lakini tunaposoma Habari ya Gideoni na kuchunguza kwa kina
tutagundua kuwa siri ya ushindi wa Gideoni ilitokana na imani yake ndogo kwa
Mungu na utayari wa kuyatii maagizo ya Mungu, leo tutachukua Muda kuangalia kwa
undani nini kilizunguka maisha ya Gideoni na ninini kilimpa Ushindi mkubwa?
Gideon na watu 300 walitakiwa kupiga tarumbeta na kuangaza kwa mwenge wakati wa usiku na Mungu aliwapa ushindi
Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
maswala kadhaa yafuatayo:-
1.
Hali mbaya ya wana wa Isarael wakati
wa Gideoni
2.
Hali ya Gideoni na wito kutoka kwa
Mungu
3.
Kushinda vita kwa mkate wa Shayiri
Hali mbaya ya wana wa Israel wakati wa Gideoni
Katika wakati wa Gideoni Israel
walikuwa wanapitia moja ya aina ya ukoloni uliokuwa mbaya zaidi, wote
tunakumbuka kuwa Israel waliwahi kuwa watumwa huko Misri, na kuwa Mungu
aliwakomboa kutoka Utumwani kupitia Musa na kuwaleta Katika nchi ya Kanaani,
wote tunafahamu kuwa utumwa wa kuelekea Misri ulitokana na wao kuishi miaka
mingi huko, Lakini sasa Mungu alikuwa amewapa nchi yao na walikuwa Taifa huru,
Hata hivyo Israel wanajikuta sasa wanatawaliwa na Wamidian, ukoloni wa kimidian
ulikuwa ni wa tofauti, wao waliwatisha sana na kusababisha waishi chini ya
mashimi na mahandaki, mapango na ngome za milimani, waliteka nyara kila kitu na
kuharibu chakula hivyo hata kula yao ilikuwa ya shida, waliwapokonya mifugo na
walikuja wakiwa wengi kama nzige kwa mujibu wa Biblia Waamuzi 6:1-6, hali iliyopelekea wana wa Israel kumlilia Bwana.
Africa na Asia na America wanafahamu
sana hali ya ukoloni, Ukoloni ni hali ya taifa moja kuvuka mipaka yake na
kwenda kulitawala lingine Kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni,
Pia uko ukoloni mamboleo, ambapo
ukoloni huu ni taifa moja au zaidi au kikundi cha watu kuzitawala nchi nyingine
kinyemela kwa kuziwekea vikwazo nchi nyingine au kuzifanya ziwe na Uchumi
tegemezi, kwa faida ya mataifa yanayotegemewa
Zamani sana aina za ukoloni
zilitofautiana Wakaldayo, waoa walikuwa waliwachukua watu na kuwahamishia
katika nchi zao kama watumwa na kuwatumia kwa faida yao, Warumi au watu wa
Ulaya walianzisha aina hii ya ukoloni wa inchi moja kubwa kwenda kutawala nchi
nyingine kwa faida yao palepale walipo, Israel imepitia aina zote za utumwa,
lakini utumwa uliombaya zaidi ni kumuonea mtu katika nchi yake mwenyewe
palepale alipo, Hii ilikuwa inawaumiza sana wana wa Israel, na kwa wamidian sio
walikuwa wakiwatawala lakini waliwapokonya Israel kila walichokuwa nacho, mpaka
chakula na kuwafanya waishi kwa hofu kwenye mashimo hali hii ilimuuma sana
Gideon Moyoni pia Waamuzi 6:11-13 Gideon
alihesabu hali hii kama kutupwa na Mungu. Kwa vile wana wa Isarael walikuwa
wamemlilia Mungu aliamua kumtumia Gideon ili kuwakomboa dhidi ya Jeshi lile
kubwa.
Hali ya Gideoni na wito kutoka kwa Mungu
Mungu aliamua kumtumia Gideon kwa
sababu kadhaa lakini ukweli Gideoni alikuwa tayari amezaliwa katika Mazingira
ya hofu kubwa aliogopa kila kilichomzunguka na Mungu alifahamu hilo, lakini
mtazamo wa Mungu kwa Gideoni ilikuwa Mungu anamuona Gideon kama shujaa Waamuzi 6:12, Malaika alimuita shujaa,
Inagwa ukweli ilikuwa hakukuwa na mtu muoga aliyepata kutumiwa na Mungu kama Gideon,
Mungu alimtazama akaona uko uwezo ndani ya Gideon na Mungu alitaka kumtia moyo Waamuzi 6:14 - 16, Gideoni alitiwa Moyo
na alianza kwa kubomoa madhabahu ya miungu ya Baba yake na kuanza kumuabudu
Mungu aliye hai, Gideoni alitaka uthibitisho kutoka kwa Mungu endapo Mungu
atamtumia Waamuzi 6:33-40
Gideoni ni wazi kuwa alikuwa muoga
hata hivyo, na Mungu aliifahamu hali yake, aliita jeshi kubwa la wanaume
wapatao 32,000 lakini hawa wote
walikuwa waoga sana na Mungu aliona hata wakishinda watajisifu kwa sababu ya
wingi wao hivyo waoga walipunguzwa na 22,000,
walirejea nyumbani na kumi elfu wakabaki na Gideon Bwana akasema hawa pia ni
wengi na alimwambia Gideoni awachje kwa kuwaleta kunywa maji, waliokunywa kwa
kiganja cha mkono ndio walioweza kupita nao walikuwa 300 tu Waamuzi 7:1-7, Hata
hivyo Gideon bado alikuwa muoga hata hakuweza kutembea peke yake
Kushinda vita kwa mkate wa shayiri
Mungu alitafuta namna ya kumtia
Nguvu Gideon Waamuzi 7:9-14 na
kupitia ndoto hii ya mkate wa shayiri Gideoni alitiwa nguvu na waliwapiga
vibaya wamidian na kuwaua wafalme wao wawili na kusambaratisha jeshi zima Waamuzi 7:15-25, Kwa nini Mungu alimpa
ushindi Gideon
1.
Alichukizwa na hali ya mateso dhidi
ya taifa lake
2.
Alikuwa mwenye kumuabudu Mungu, alivunja
madhabau ya baba yake na kumuamini Mungu aliye hai
3.
Ingawa alikuwa muoga sana alitii
kile Mungu alichokuwa akimuelekeza
4.
Alitiwa nguvu na ndoto ya mkate wa
shayiri mkate huu ulianguka kutoka Mbinguni na kuipiga hema ya wamidian na
kuisambaratisha vibaya, aliabudu.
5.
Gideon alihitaji kupandishwa imani
na kuamini kuwa Mungu atamsaidia
6.
Gideon alikubali kwenda uwanja wa
vita.
7.
Imani ndogo tuliyonayo katika Kristo
ambaye ni mkate ushukao kutoka Mbinguni itakupa ushindi katika maisha yako, Yesu
ndio Mkate wa ngano aliouona Gideon siri ya kushinda vita vya aina yoyote
duniani inayotukumba watu wa Mungu, ni kumwamini Yesu ni kujitia nguvu kwa huyo
yeye ndio kimbilio letu, aliye dhaifu na asemi mimi ni Hodari.
Ushundi wa Maisha yetu na mapambano ya aina mbalimbali
utategemea na kiasi cha imani kitakachotutia nguvu kutoka mbinguni ni wazi kuwa
Gideon alitiwa nguvu sana aliposikia tafasiri ya ndoto ya mkate wa shayiri,
mkate huu ulioshuka kutoka mbinguni ulikuwa unamwakilisha Yesu Kristo kiasi
chochote cha imani tulicho nacho katika Kristo hata kama ni kidogo kiasi gani
kitatupa ushindi dhidi ya adui, hatihitaji silaha wala ujuzi wa vita tunahitaji
utayari na kukubali kuelekezwa na Mungu na kisha kutiwa Nguvu Gideon alitiwa
nguvu na Mungu kupitia ndoto ya mkate wa shayiri uliotoka Juu. Mungumape kila
mmoja wetu ushindi kwa mkate wa Shayiri katika Jina la Yesu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni