******************************************************************
Somo;
Kuigwa kwa kiongozi wa Kanisa
Hakuna furaha kubwa kwa baba yetu wa
Mbinguni anayoipata kuliko anayoipata
anapowaona watoto wake wanaitikia wito wa kuwaongoza kondoo wake.kuitikia wito
wa kuwaongoza kondoo ni moja ya hatua zinazodhihirisha kukua kwa mtu aliyeokoka.katika
hali ya asili Mzazi asingependa kumuona mtoto wake anabaki mchanga tu siku zote
na hakui, Furaha ya mzazi hutimia anapoona moja ya watoto wake akiwaongoza
wadogo zake na kusaidia kufanya majukumu ya mzazi katika hali kama hiyo Mungu
hufurahi anapoona mtu aliyeokoka anakua na kuifikia hatua ya kuwaongoza wengine
Lakini ni muhimu kuufahamu mapema kuwa wale ambao tumekubali kuwaongoza huwa
wanaiga sana Tabia zetu hivyo ni muhimu kujifunza somo hili “kuigwa kwa
kiongozi wa kanisa” tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu;-
Jinsi
kondoo wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa.
Wajibu
wa kiongozi wa kanisa kuwa kielelezo
Kiongozi
wa kanisa ni mwakilishi wa Mchungaji
Jinsi kondoo
wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa
Watoto
wa kike huwaangalia kwa makini mama zao wanapopika chakula katika hali ambayo
wakati mwingine ni vigumu hata mama kujua kinachoendelea na hatimaye utaona nao
wanatafuta vyombo vya kitoto vinavyofanana na kuanza kuwaiga jinsi ya kupika
kumbe watoto ndivyo walivyo ni kwa msingi huu watoto wakiroho huwaiga wale
wanaowaongoza au waliowatangulia katika wokovu kwa jambo lolote lile liwe jema
au baya. Kuna usemi mmoja unaosema “ukitaka kufahamu tabia ya kiongozi
waangalie wale anaowaongoza” Kiongozi kamwe hapaswi kuwaambia watu fuateni
yale ninayosema na si yale ninayotenda kiongozi huyo hajui analolisema, Kuigwa
kwa kiongozi katika Matendo yao ni kanuni iliyoandikwa mioyoni mwa watu na haiwezi kuepukika Biblia ina mifano mingi ya jinsi watu
wanaooongozwa wanavyowaiga wale waliowaongoza angalia mifano hiyo katika 1Falme 22;51-53, 2Nyakati 22;1-4, Yeremia
9;14, Amosi 2;4, 2 Nyakati 17;3-4,26;3-4, 2Tomotheo 1;5.Biblia inaonyesha
kuwa Simeon Petro aliandaliwa mapema kuwa kiongozi wa kanisa Luka 22;31-32,Matendo 1;15,2;14. Simeon
Petro wakati mmoja kama kiongozi wa kanisa aliamua kuacha majukumu yake ya
kiutumishi na kuamua kwenda kuvua samaki wanafunzi wengine walipomuona waliamua
kujiunga na kiongozi wao kuvua samaki Yohana
21;7.Yesu alipowakuta wao Baharini Petro alifahamu kuwa ameonyesha mfano
mbaya hususani kwa wanafunzi wale wengine akajuta na kujitupa baharini Yohana 21;7 sisi na si kama Viongozi
tunawajibu mkubwa wa kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kufahamu kuwa kuishi
maisha ambayo si kielelezo ni sawa na kuisaidia kazi ya shetani, Viongozi
wataigwa na wale wanaokuja nyuma yao kwa kila kitu kama tunawahi ibada, ni
waombaji, tuna bidii,tunatii neno la Mungu na kulitetemekea tunatii wachungaji
n.k watu wanaoongozwa humtazama kiongozi wao kwa kila jambo hata kama ni baya
kama uvivu, ulegevu, uzembe n.k kwa msingi huo ni muhimu kuwa makini tunapokuwa
tumeingia katika ngazio ya maongozi.
Petro alimwangaluia sana kiongozi wake
Yesu jinsi alivyokuwa anafanya maombi ya kufufuka wafu naye akaiga vilevile
kabla ya kufanya maombi ya kufufuka wafu
kumbuka kuwa Yesu aliwatoa watu nje
na Petro akaiga vilevile Linganisha Marko
5;39-42 na Matendo 9;39-41 sisi
nasi tukiwa kama Viongozi wa kanisa tunaangaliwa katika kila jambo. Waebrania 13;7 Nyakati za kanisa la
kwanza waliwaiga Viongozi wao katika kila jambo walichofanya Viongozi ni
kuwasihi wauchunguze mwisho wa mwenendo wa Viongozi wao.
Wajibu wa kiongozi wa
kanisa kuwa kielelezo
Mpaka hapo tumeona jinsi kiongozi wa
kanisa anavyoweza kujenga ufalme wa Mungu au kuubomoa,kiongozi wa kanisa
akafanya vema atawafanya wanaomuongoza nao kufanya vema ni kwa sababu hii ndio
maana Mungu huwaheshimu sana Viongozi wa kanisa na ndio maana anataka Viongozi
wa kanisa wawe vielelezo Neno la Mungu linatoa wito na wajibu kwa Viongozi wa
kanisa kuwa vielelezo 1Timotheo4;12,16
Tito 2;7;1Petro 5;2-4.Viongozi
Nyakati za kanisa la kwanza walijitahidi sana kuwa vielelezo na ndio maana
ufalme wa Mungu ulijengeka kwa kasi sana na kwa namna ya kipekee katika wakati
wao 1Koritho 11;1, 4;16,Wafilipi
3;17,4;9,1Thesalonike 2;10,2Thesalonike 3;7,9, Mungu hana upendeleo Neema
ya Mungu iko kwa kila kiongozi
kutusaidia kuwa kielelezo kwa ajili ya kujenga ufalme wake Bwana ampe
neema kila mmoja wetu kuwa kielelezo katika jina la Yesu Kristo.
Kiongozi wa kanisa ni
mwakilishi wa Mchungaji.
Ni
muhimu kuufahamu kuwa mtu anapoteuliwa kuwa kiongozi katika sehemu yoyote iwe
kanisa au cell au makanisa ya nyumbani au vijana au kina mama au maombi au
kikundi chochote yeye ni ana kuwa ni
mwakilishi wa Mchungaji katika eneo husika ina maana ya kuwa kiongozi huyo
huongoza eneo lake hilo kwa niaba ya Mchungaji hivyo unafanya kile ambacho
Mchungaji angekifanya katika sehemu hiyo
Luka 10;1, hivyo anayemsikiliza
kiongozi anamsikiliza Mchungaji anayekataa hamkatai Mchungaji tu bali na yeye
aliyewatuma Luka 10;16,Kwa msingi
huo ingawa Viongozi hawa hawaitwi wachungaji Lakini ni wachungaji wa maeneo yao
waliyopewa kuyasimamia hivyo kila unapofanya jambo jiulize kuwa hiki
ninachikifanya je Mchungaji angekifanya? Kwa msingi huo wewe kama kiongozi ni
muhimu kukumbuka kuwa uko karibu na watu kusaidia huduma ya kichungaji na hivyo
maisha yako kama kielelezo yatasaidia kujenga au kubomoa ufalme wa Mungu na
kanisa lake kwa nia moja kabisa tukatae kutumiwa na ibilisi kuliharibu kanisa
la Mungu na chini ya neema ya Mungu tuseme kama Paulo mtume “MNIFUATE MIMI, KAMA
MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni