Mstari wa msingi 1Timotheo 5;15 “Kwa maana wengine
wamekwisha kugeuka nyuma na kumfuata shetani”
Mtu aliyeokolewa anaweza kugeuka
nyuma na kumfuata shetani kama hatamfahamu shetani ni nani na Fikra zake
2Wakoritho 2;11 Shetani ni adui yetu Luka 10;19 Ni adui wa watu waliookoka kama
alivyo adui wa Mungu Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili
vikuu vifuatavyo;-
·
Historia ya shetani
·
Mbinu za shetani anazozitumia kutuletea upinzani
Historia ya shetani
Shetani hapo kwanza hakuwa adui wa Mungu, Yeye
aliumbwa na Mungu kama walivyoumbwa malaika wengine, alifanywa kuwa malaika
mkuu na kupewa utukufu mwingi na Mungu. Hatimaye alikuwa na tamaa na kiburi cha
kutaka kuwa sawa na Mungu na hata kumpindua Mungu aliyemuumba. aliwashawishi
malaika wachache kupigana na majeshi ya Mungu na matokeo yake walishindwa
vibaya na kutupwa nje ya mbinguni hivyo akawa siyo malaika mkuu tena aliyekuwa
na jina Lucifer ambalo maana yake ni mwenye kutoa mwanga kama nyota ya alfajiri
na tangu wakati huo aliitwa shetani Ezekiel 28;13-19, Ufunuo 12;7-9 Isaya
14;12. Jina shetani maana yake ni Adui ,
mpinzani, mshindani mwenye kuleta vizuizi kazi zake kubwa ziko sawa na majina
yake ni adui wa watu wa Mungu ni mshindani ,huleta upinzani na vizuizi kwa watu wa Mungu hususani
waliookolewa katika hali ya chuki
kabisa ili ikiwezekana waache imani na njia ya wokovu ya kweli ya kumfikisha mtu mbinguni Yeye anaijua njia hiyo ya kweli lakini kwa
kusudi anataka kupotosha watu wamuache Yesu ambaye ndiye njia na kweli na
uzima ni shetani anaye waambia watu kuwa
hakuana wokovu na kuwa watu wanaweza
kumuona Mungu bila Yesu na kwa kutumia
udanganyifu anawakosesha wengi.Matendo 16;16-18 Shetani anamfahamu Yesu kuwa
ni mwana wa Mungu na kuwa ndiye wa kuhubiriwa na kuleta wokovu na kuwa wanaohubiri injili
ya wokovu wana nguvu kubwa na ufalme wa
Mungu unawasubiri Marko 3;11 Matendo 19;13-16.
Shetani baada ya kuasi mbinguni yeye na
malaika zake wamekwisha kuhukumiwa na mahali pao ni katika ziwa la moto wa
Milele na hawana nafasi ya kutubu tena Mathayo 25;41 Ufunuo 20;10 na kwa sababu uzuri wa mbinguni
anaufahamu anachokifanya ni kuwadanganya
watu na kushindana na watu
waliookoka ili wamfuate na kuteswa
pamoja naye katika ziwa la moto milele, anaweza kuwafanya waliookoka kuwa na
wokovu vuguvugu na hatimaye waweze kutapikwa Ufunuo 3;15-16 safari ya mbinguni
ni kama mpira wa miguu katika dunia ambapo mtu anayekwenda kufunga goli huzuiwa
kwa namna zote hata kupigwa ngwala na
viatu ilimradi tu asifanikiwe kufunga goli
Mbinu za shetani anazozitumia
kutuletea upinzani.
Ni muhimu kufahamu kuwa shetani
wakati wote haji katika njia ambayo utafahamu kuwa ni shetani kwani kwa njia hiyo watu watashituka upesi ,
Mara nyingi huja kama malaika wa nuru akiwatumia wachungaji wengine wanaosema
kuwa wameokoka au watu wanaosema kuwa
wameokoka kututoa katika kweli ya wokovu
2Wakoritho 11;14-15 baada ya kushindwa kuuzuia wokovu wako unapokuwa umeokoka
shetani kama Farao huwa hakati tama yeye na majeshi yake hujaribu tena na
tena kukurudisha nyuma kama farao alivyo
jaribu kuwafuatailia wana wa Isarael shetani atajaribu kufanya hivyo ili turudi
nyuma na kumtumikia yeye tena Kutoka 14;5-8 wakati ulipookoka shetani alishindwa vibaya
kushindana na nguvu za Yesu aliye Bwana na mwokozi wetu na akasalimu
amri Kutoka 12;30-36 kwa msingi huo shetani atatumia mbinu mbalimbali kukufanya
uache wokovu hususani ukiwa bado mchanga
katika wokovu kwani kuua kitu kichanga ni rahisi zaidi alijaribu kuwaua
Yesu na Musa katika uchanga wao Kutoka 1;15-22,2;1-10, Mathayo 2;13 mbinu zote
za shetani zinajumuishwa katika kukushawishi uuache wokovu Biblia inasema
katika 1Nyakati 21;1 “Tena shetani akasimama akamshawishi Daudi kuwahesabu
Israel “ Kushawishi ni kubadili nia ya mtu kwa kumuumbia mawazo mengine juu ya jambo kinyume na mawazo yale aliyokuwa
nayo mwanzoni kabla ya kushawishiwa
shetani atatumia mbinu mbalimbali katika
kushawishi ikiwemo
1.
Kukushawishi
yeye mwenyewe ili uache njia ya kweli
Unaweza kuona
katika akili yako kunaumbika mawazo yaliyo kinyume na wokovu ulioupokea na
hatimaye kukufanya usipige hatua yoyote ya ziada tangu ulipookolewa mawazo ya aina hii yanatokana na shetani,
endapo utayafuata mawazo hayo unakuwa umefuata mawazo ya ibilisi na mawazo yako
mwenyewe na huo ni uasi kwa Mungu Isaya
65;2 Ni lazima ukatae kuafikiana na kila wazo lililo kinyume na njia ya wokovu.
2.
Atatumia
watu kukushawishi uiache njia ya kweli
Mara baada ya
wokovu utaona watu wanaoandamana kukushawishi kurudi dhambini utashangaa
marafiki wa zamani wakikujia na
kukualika katika uvutaji wa sigara bangi na ulevi na dhambi nyinginezo watakuambia kuwa wana hela nyingi na
wahahitaji watu wa kutumia nao , utashangaa watu wanakulaumu kuwa umepotea au
kukucheka na kudharau uamuzi wa Busara ulioamua na wanaweza hata kukutenga au
kukuchukia kabisa inakupasa kuwa
mwangalifu watu wakikuvuta kurudi dhambini
usiwasikilize wala usiwajali na ujitahidi kujiepusha nao ili wasije
wakainyonya nguvu yako ya wokovu mistari
ifuatayo ni muhimu kwako Mithali 1;10-16, Torati 13;6-8 Mithali 24;1 na Hosea
7;8-9
Shetani atatumia kila njia kuhakikisha
kuwa unakosa mafundisho ili ubaki umedumaa bila kukua katika wokovu ili
hatimaye urudi nyuma na kuiacha kweli ya wokovu kwa sababu hiyo utaweza kuona siku za mafundisho ndio wageni wanakutembelea nyumbani pamoja na hayo usikubali kuacha
kwenda kanisani na kukaa na wageni kama watataka uende nao itakuwa vema.
Wakati mwingine unaweza kuona kama unafanya
biashara majira ya siku na saa za ibada ndio biashara inachanganya sana hilo
pia ni kusudi la ibilisi kukufanya utafute mapato na kukosa ibada, aidha watu
wanaweza kukushawishi na kulaumu kuwa siku hizi umekuwa bise huonekani vyovyote
iwavyo ni heri ukose kipato lakini usiikose mbingu Yohana 12;25 ni muhimu kujikana
nafsi unaweza kukutana na watu wanaokudhihaki kuwa siku hizi mbona maswala ya
ibada yanazidi au watu wanaomsema vibaya mchungaji wako au askofu wako na kutaka kukutoa katika imani jihadhari
wajibu watu hao kama nikodemu alivyowajibu wale waliokuwa wakimsema
vibaya Yesu mchungaji wetu Yohana 7;45-51 unaweza kuona pia siku za mafundisho
na ibada ndio homa zinacharuka na hali za kujisikia vibaya au kuona uvivu au
kuumwa kichwa au tumbo la kuhara n.k kemea hali hiyo na chukua hatua ya imani
kwenda ibadani utashangaa jinsi ambavyo shetani atakavyokimbia na hali hiyo
kutoweka katika dakika usiyoijua Yakobo 4;7,1Petro 5;8-9.
Usimuamini au
kumfuata mtu awaye yote ambaye anasema ameokoka lakini anakuvunja moyo kwenda
ibadani au kuendelea na wokovu au kuenda katika kanisa linalohubiri
wokovulililo tofauti na kanisa au dini yako ya kwanza isiyohubiri wokovu fahamu
kuwa huyo ni mpinzani anayetaka kukutoa kwenye kweli akiwa amekuja kama malaika
wa nuru au mtumishi wa haki 2wakoritho 11;14-15
Kwa ujumla
jihadahari na jambo lolote lile linalokunyima kuenda katika ibada bila sababu
za msingi au kukukosesha wokovu, shetani anajua kuwa ukipata mafundisho
utaimarika na kuwa askari utakayemdhibiti vilivyo
Usikubali kwenda
kwenye mikesha ambayo itakufanya kesho yake ushindwe kulisikia Neno la Mungu
vema, Neno la Mungu linauwezo wa kumbadilisha mtu wala usikubali mialiko ya
kuhubiri huku wewe ukiwa mchanga kiroho kwani kwa sasa unahitaji kujifunza neno
kwanza na kuwa na muda mrefu wa
kujifunza neno kabla ya kuhudumu 1Tomotheo 1;7 Yakobo 3;1 kila jambo
linalokuzuia kusikia au kujifunza neno likatae na kujihadhari nalo usikubali
kuiacha kweli ya wokovu kaa katika imani uliyoipokea na kudumu katika fundisho
hii ndio itakuwa siri ya kukufanya uwe mshindi na zaidi ya mshindi Warumi 8;35-37.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni