Somo la Tisa
Vijana na Hatari ya ugonjwa wa ukimwi
Ukimwi uligundulika kwa mara ya
kwanza nchini Tanzania mwaka 1983,ambapo wagonjwa watatu waligundulika katika
hospitali ya Ndolage mkoani kagera,Mwaka
1984 wagonjwa zaidi walionekana mkoani kilimanjarommoja,na tabora wawili,1985
mikoa nane kati ya 20 iliripotiwa kuwa na wagonjwa hivyo kulikuwa na wagonjwa
kati ya 404 amabao kati ya hao 322 walikua mkoani Kagera;1986mikoa yoote ya
Tanzania iliripotiwa kuwa na wagonjwa hadi mwaka 2001 december wagonjwa wapatao
144,498 waliripotiwa wagonjwa hao ni wale walioripoti mahospitalini na
inakisiwa kitaalamu kuwa kati ya wagonjwa (5) Watano ni mmoja tu anayeripoti
hospitali,Umri wa wagonjwa hao ni kati ya 20-49,kiwango kikubwa zaidi ni 25-34
na 30-39 hivyo unaweza kuona kuwa kundi kubwa la wanaoshambuliwa ni
vijana.ukimwi sasa umesambaa mara dufu zaidi na karibu kila familia imewahi
kuona machungu ya ugonjwa huu Hivyo kama kanisa hatuwezi kuacha
kuzungumzia swala hili Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo
manne yafuatayo;-
- Maana ya ugonjwa wa Ukimwi.
- Njia kuu za maambukizi ya ukimwi.
- Athari za ugonjwa wa ukimwi.
- Wajibu wa kanisa katika kukabiliana na tatizo la Ukimwi.
Maana ya ugonjwa wa ukimwi.
Neno ukimwi ni kifupi cha maneno matatu
yafuatayo ambayo ni Ukosefu wa Kinga,Mwilini kwa kiingereza AIDS yaani “ A Human Immune Deficiency
Syndrome”Ugonjwa huu husababishwa na
vijidudu vidogo sana kuliko bacteria ambavyo huitwa Virisi Vya Ukimwi (V.V.U) kwa kiingereza (H.I.V) yaani Human Immunodeficiency
virus. Vijidudu hivi hushambulia chembechembe nyeupe zilizopo katika mwili
ambazo ni kinga au askari wa mwili kwa watu wa duniani ni ugonjwa mpya lakini
kwa watu wa biblia huu sio Ugonjwa mpya Magonjwa kama ukimwi yaliahidiwa katika
biblia kwa watu watakaoishi kinyume na kanuni za kimungu (Kumbu 28;15,27,35,58-61),kinga ya mwili ilianza kuharibika mara tu
baada ya anguko la mwanadamu katika Bustani ya Edeni,mungu alimuumba mwanadamu
aishi milele lakini mungu alimuhakikishia kifo Adamu endapo angeishi kinyume na
kanuni zake na kwa kutokutii kwake na kuula mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2;15-17) Ni tangu wakati huu
basi kinga ya mwili wa binadamu iliharibika wanadamu walianza kuzeeka,kupatwa
na magonjwa,kupunguziwa siku za kuishi kula kwa jasho kuzaa kwa uchungu na
taabu za kila namna hivyo mtu awe na ukimwi au asiwe nao kufa atakufa tu,Mwili
hauna tena uwezo wa kumfanya mtu asiwe na uwezo wa kupatwa na magonjwa (2Koritho 5;1-4) Mauti ni matokeo ya
dhambi, na kwa kweli Mungu ataihukumu kila aina ya dhambi tuifanyayo iko ahadi
ya adhabu kwa waasherati(Ebrania 13;4),hapa
hatuukumu kuwa kila mtu aliye au anayeugua ukimwi ameipata kwa zinaa hapana
wala wao sio wakosaji wakubwa lakini mkazo hapa ni kuwa dhambi yoyote aifanyayo
mwanadamu mshahara wake ni mauti (Warumi
6;23)watu woote wanaofanya dhambi zaidi ya zinaa wanahakikishiwa
kutokuurithi ufalme wa Mungu (wagalatia
5;19-21 Wakoritho 6;9-10).
Njia
kuu za Maambukizi ya Ukimwi.
Njia kuu za maambukizi ya
ugonjwa huu wa Ukimwizilizofanyiwa
utafiti Tangu ukimwi ulipoanza ni kama ifuatavyo kulingana na viwango vya juu
mpaka vya chini
- Tendo la Ngono au kujamiiana
- Kuongezewa damu
- Maambuklizi ya watoto wakati wa kuzaliwa
- vitu vyenye ncha kali.
Hizo
ndio njia kuu za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,Hata hivyo kwa mujibu wa
utafiti ambao umefanywa kwa jamii kuhusu maambukizi umebaini kuwa waathirika
zaidi wa ugonjwa huu ni wana ndoa wakifuatiwa na makundi mengine hizi ni
takwimu za mwaka 2000 takwimu hizi ni kama ifuatavyo;-
- Watu walio na ndoa waliongoza kwa asilimia 48%
- Watu walioishi bila ndoa (Mabachela,Singles n.k) 32%
- Watu waliooana na kuachana 6%
- Watu waliotengana 5%
- Watu ambao hawajaoa wala kuolewa lakini wanafanya ngono ni 2%.
Takwimu
hizi ni sahihi Kiroho tunaweza kusema ukimwi unawashambilia zaidi watu walioko
katika ndoa kwa nini huenda ni kwa sababu ya matendo ya kutokuwa waaminifu
katika ndoa zetu.
Tabia ya Virusi vya ukimwi
katika Picha.
Kirusi Chembechembe
Virusi vipya baada
Nyeupe ya
niezi mitatu
Pichani juu kirusi kipya kinapoingia mwilini
huishambulia chembechembe nyeupe ya uhai katika damu ambayo ni ngumu sana
kushambuliwa lakini kirusi huishambulia na kuifanya chakula kasha baada ya
miezi mitatu kirusi huzaliana kwa wingi zaidi na kila kimoja hutafuta
chembechembe nyeupe nyingine ili kuishambulia Virusi vimekuwa vikiwasumbua
wanasayansi kwani ni kidogo sana na hujibanza kwenyekinga ya mwili hivyo kupata
dawa ya kukishambulia bila kuidhuru chembechembe nyeupe ni ngumu kwani huishi
ndani yake,pia vina tabia ya kubadilika badilika na kinajitengenezea kinga
gamba gumu,Kadiri mtu anavyofanya zinaa ndivyo anavyojiongezea maambukizi zaidi
ya virusi vipya vyenye tabia mpya na kujiweka katikahatari ya kufa kwa haraka
ni vizuri kujilinda kwa Mungu.
Athari za ugonjwa wa ukimwi.
Kupungua
kwa wastani wa umri wa kuishi.
Kupungua kwa wastani wa umri wa
kuishi ni moja ya athari zitokanazo na ukimwi,na ni swala la
kimaandiko,Maandiko yanatufundisha jinsi
ambavyo mtu anaweza kuishi siku nyingi pale anapomcha Mungu (Mithali 10;27),Mungu alipunguza miaka
ya kuishi kwa mwanadamu kadiri uasi ulivyokua ukiongezeka,Babu zetu tangu Adamu
waliishi zaidi ya miaka mia tisa hivi 900,(Mwanzo
5;5,8,11,n.k.) Baada ya uovu kuongezeka umri wa kuishi ulipunguzwa kufikia
miaka 120 (Mwanzo 6;1-3),Wakati wa
Musa Mungu alimfunulia Musa kuwa amepunguza umri wa kuishi mwanadamu mpaka
miaka 70 na kama ana nguvu 80 (Zaburi
90;10).Baada ya miaka michache hii ukimwi umezifanya nchi nyingi za kusini
mwa sahara zikiwemo Afrika kusini,Zimbabwe,Angola n.k kuwa na wastani wa kuishi
kati ya miaka 45-30 hivi.
Ongezeko
la watu Tegemezi (Yatima na Wajane).
Mtu awaye yoote asiyepiga vita
ukimwi haelewi analolitenda,Ukimwi umeiathiri kila familia,ukoo,na
jamii,umefika wakati ambapo jukumu la kutunza Wajane na Yatima limekuwa kubwa
kiasi ambacho hatutaweza kukwepa kutunza Wadogo zetu,watoto wa kaka zetu,Dada
zetu,wajomba zetu,shangazi zetu,binamu zetu,mama zetu wakubwa,mama zetu wadogo,
baba zetu wakubwa,Baba zetu,wadogo, n.k.Lazima tuwatunze na kuwapa elimu ya
kutosha kwa kipato cha Afrika hili ni jukumu Kubwa sana na endapo hatutawapa
elimu ya kutosha tutakuwa na kanisa jinga,na Taifa jinga,fgamilia jinga Jukumu
la kuwatunza yatima na wajane kibiblia
ni jukumu la wakristo wa kweli (Yakobo
1;27)
Kupungua
kwa watenda kazi
Ukimwi unaua wataalamu
wengi,wakulima,wafanya biashara,wazalishaji viwandani,na unadhoofisha utendaji
makanisani nk.Mtu mwenye ugonjwa wa ukimwi huugua mara kwa mara ,hivyo
wanaweza wasiwepo kazini mara kwa
mara,hali kadhalika kanisani ,mashuleni n.k Jaribu kuwaza Mwalimu mwenye ukimwi
au mwanajeshi mwenye ukimwi anawezaje kuwajibika na kulipigania taifa Hali ya uchumi ni dhahiri pia kuwa itadidimia
Kuongezeka
kwa gharama za matibabu
(Kwa sababu ya kuugua kwa Muda mrefu) Kama
tunavyofahamu tabiya na mwenendo wa ukimwi Tangu mtu anapogundulika kuwa ana
virusi vya ukimwi na hasa cd4s zinapokuwa chini anatakiwa aanze tiba bila
kukosa na kwa tabia ya ukimwi watu hawa huugua kwa Muda mrefu jambo hili
linapelekea kuongezeka kwa gherama za matibabu na lishe.Aidha kutakuweko wimbi
la kuongezeka kwa watu waliokosa Matumaini,walioathirika
kisaikolojia,kusambaratika kwa familia,ukiwa,upweke,misiba na huzuni,shutuma
mauaji na visasi au ulevi wa kupindukia pia kuongezeka kwa tatizo la Unyanyapaa
nk .Hizi zoote ni athari za Kuwepo kwa ugonjwa wa ukimwi.
Wajibu
wa kanisa katika kukabiliana na tatizo la Ukimwi
Ni
muhimu kufahamu kuwa kanisa linawajibika na swala zima la tatizo la ukimwi
Mchungaji na washirika amabao wanadhani
wako salama na wanaufurahia wokovu wakifikiri kuwa wao hawana ukimwi
wanajidanganya,suluhisho la tatizo la ukimwi haliko nje ya taasisi yoyote ile
wala dini yoyotre ile wala serikali yoyote Macho ya mungu yanaliangalia kanisa
kama chombo chenye majibu ya kutosha kwa swala zima la ukimwi ni Biblia pekee
yenye majibu ya kutosha ,matumaini ya kutosha ,kinga ya kutosha na matibabu ya kutosha kuhusiana na swala la
ukimwi Kumbuka kuwa wanaoathirika sasa wengi wao hukimbilia kanisani wakihitaji
msaada wa kiroho sasa kama kanisa litakwepa wajibu huu na kujikita katika kunyanya
paa wakati kanisa ndilo lenye majibu ya kimaadili,ya waliochanganyikiwa,ya
waliokata tama,ya walio na wasiwasi,ya waliona mashaka na tukasimama kuhukumu
na kushutumu Je watu hawa wa Mungu wakimbilie wapi? Kule Rwanda wakati wa
mauaji ya kimbari watu wengi walikimbilia makanisani wakifikiri wangekuwa
salama lakini kwa kuwa kanisa lilikuwa limeshindwa kusimama katika nafasi yake
na dhambi ya kibaguzi ilikuwa imewatafuna hukohuko walikokimbilia watu ndiko
waliko uawa Ukimwi unalipa kanisa wajibu mzito sana ni wajibu ambao ni zaidi ya
kuhubiri injili,Kanisa linawajibika kuwaonya watu,kufundisha ,kutoa
matumaini,kufariji,kupinga vitendo vya unyanyasaji dhidi ya waathirika,kutoa
jibu mbadala zaidi ya kondom ambayo ndiyo majibu ya mkato ya dunia hii,Kuwa na
miujiza ya uponyaji ili kwa maombezi wagonjwa hao wapone na endapo hawatapona
wajiandae kufa kishujaa wakiwa wamejaa matumaini na kuwa tayari kukabiliana
mauti wakimuamini Mungu. Wakiwa na ushuhuda wa huduma juhudi na bidii ya kanisa
Dhidi yao. Ni kwa msingi huu kanisa linawajibika
- Kutoa majibu ya Yaliyoshindikana kwa Dunia
Mungu anayo majibu ya
yaliyoshindikana kwa dunia na serikali,majibu haya hayapatikani kokote
isipokuwa katika neno lake kupitia kanisa,hata kama hatujasikia kokote kua
Mungu anaponya ukimwi kanisa ni lazima liwe na majibu ya jinsi kama hii Kuwa
Mungu anaponya Elisha hakuwahi kusikia au kusoma popote kuwa ukoma unapona
lakini pale serikali iliposhindwa kutoa majibu ya uponyaji kwa ukoma Eilsha
alikuwa tayari kutoa majibu ya swala lililoshindikana soma (Wafalme 5;4-14)
- Kondomu sio suluhisho la kujikinga na ukimwi.
Kanisa linaposimama katika zamu yake ni lazima lisimame kama nabii kuonya na kuonyesha njia dunia
inapoamini kuwa ,lazima mtu abakie na mpenzi mmoja muaminifu lazima tutoe
majibu kuwa hakuna mtu anaweza kuwa muaminifu bila kukutana na Yesu kristo hivyo ni lazima
tumuonyeshe Kristo kuwa ni njia na kweli na uzima,Mtu kuwa na mpenzi mmoja
maana yake ni lazima awe mke halali na
Mume halali Kanisa lazima lionyeshe kuwa huwezi kuwa na mpenzi mmoja muaminifu
nje ya Kristo na ndoa ya kikristo,Ndoa zozote zenye kuruhusu wake zaidi ya moja
kwa sasa hazina soko tena sera ya kibiblia ya mke moja mume moja inauzika kwa
sasa,Dunia inaposema ikishindikana tumia kondom kanisa ni lazima lionyeshe
kivitendo kupingana na dhana kwa sababu
ni lazima tujiulize kwanini ukimwi haupungui hata pamoja na kuwepo kwa
matangazo ya kutosha kuhusu ukimwi na matumizi ya kondom,Kwanini uwezo wa
kondom kuzuia ukimwi unapewa asilimia 70 tu,Kwanini ziwepo za viwango tofauti
na bei tofauti lazima tuonyeshe jibu la kweli kuwa kondom si salama
ikilinganishwa na nguvu ya utendaji wa mwili na tama zake,kimsingi kondom
ziligunduliwa zamani zaidi kabla ya ukimwi kwa kusudi la kupanga uzazi kama
kondom haina uwezo wa kuzuia kwa asilimia 100 ni wazi kuwa si kinga kamili
Kanisa
ni lazima lisimame katika zamu yake.
Kanisa kama nabii ni lazima lionye na
kukemea na kuonyesha njia iliyo sahihi (Ezekiel
3;16-19) Lazima tuchukue tahadhari ya kutosha katika kuwashauri na
kuwaandaa maharusi huku wakipimwa kabla ya ndoa,
Kanisa kama Mchungaji lazima liwajibike
kufariji Ezekiel alikuwa nabii aliyetoa maonyo sana juu ya Yuda kwenda utumwani
Babeli lakini ilipotokea kuwa watu wamekwenda utumwani hakutoa tena maonyo
badala yake alisimama kuwafariji,hata kama tunakemea uovu hatuwezi kuacha
kuwapokea walojeruhiwa na kuendelea kuwahukumu bali tunapaswa kuwaganga(Ezekiel 34;1-10,371)
Kanisa kama Mwalimu lazima liwafundishe watu
hususani vijana kusubiri na kungoja wakati halali wa kufanya mapenzi, lazima
lifundishe maadili na usafi wa ndoa ya kweli ya mke moja na mume moja waaminifu,
lazima tufundishe kujali na kutokuwanyanyapaa waathirika ila wajisikie wako
katika mikono salama ya wakristo
Kanisa kama wainjilisti tunawajibu wa
kuwakaribisha waathirika na kuwaonyesha njia ya halali nay a kweli ya kuishi
kwa matumaini
Mwisho kanisa ni lazima lipambanena tabia ya
unyanyapaa tukumbuke kuwa wakati watu waliwatenga wenye ukoma nyakati za biblia
Yesu aliwagusa (Luka 5;12-13) Wakati
dunia inakataa kukaa na wenye ukimwi na kuchochea kifo cha haraka cha watu hawa
ama kuwaona kuwa ni wenye dhambi sana kanisa lazima litambue kuwa wanahitaji
upendo wetu,faraja,kujali na kuwa ni wakristo pekee wanao weza kuonyesha hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni