Jumatatu, 1 Februari 2016

Simba aliye wa kabila la Yuda!


Ufunuo 5:1-5 Biblia inasema hivi  “1. Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. 2. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 3. Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 4. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 5. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba”


Mungu ni wa ajabu sana nilipokuwa najisomea Biblia na kufika katika Mstari wa tano nikayaona maneno hayo Simba aliye wa Kabila la Yuda!  Maneno hayo yalinishangaza sana ni wazi kuwa Simba anayetajwa hapo ni Yesu Kristo hilo halina mjadala,  ni wazi kuwa Yesu ni Masihi na masihi alikuja kupitia ukoo wa Yuda hilo pia halina mjadala, Daudi pia alitokea ukoo huu wa kabila la Yuda hilo halikuwa na mjadala, Jambo kubwa lililovuta hisia kwangu ni kutajwa kwa Yuda mwenyewe hapa ndipo penye mjadala


Yuda wanaotajwa katika biblia wanaweza kuwa wengi, lakini walio maarufu ni watatu 1. Ni Yuda Iskariote umaarufu wake umekuja kutokana na tendo lake la kumsaliti Bwana Yesu, 2 Yuda ndugu yake Yakobo hawa ndi ndugu wa kunyonya wa Yesu Kristo na waandishi wa nyaraka za Yakobo na ule waraka wa Yuda, hawa wako katika agano jipya, Yuda anayetajwa akiunganishwa na Masihi ni Yuda wa agano la Kale huyu ni mtu wa namna gani?

Yuda alikuwa miongoni mwa watoto wa kiume wa Israel au Yakobo, alipata umaarufu sana kuliko ndugu zake, Kabla kidogo ya kuondoka ulimwenguni Yakobo ambaye ndiye Israel alitoa unabii kuhusu maswala ya maisha ya wanae ya baadaye, alimtabiria mema sana Yuda Mwanzo 49:8-12 moja ya maswala hayo muhimu ni kuja kwa Masihi kupitia kabila la Yuda

Yakobo alikuwa na wana 12 lakini swali la kujiuliza kwa nini Yuda awe maarufuna wa muhimu labda zaidi kuliko wengine? Kwa nini ni kama amebarikiwa zaidi, kwa nini aunganishwe na ubaba wa kuja kwa Masihi kwa nini Yesu aitwe SIMBA ALIYE WA KABILA LA YUDA? Ni lazima kuna maswala ya kujifunza kumhusu Yuda 

Ni wazi kuwa tunaelewa kuwa Mungu alinmtumia Yuda kutimiza mpango wake, Mungu katika hekima yake iliyo ya ajabu kuliko ya wanadamu, huwatumia wanadamu kwa makusudi yake na kwa neema yake na rehema, “1Koritho 1:26-29” si lazima uwe maalumu sana au utoke katika ukoo muhimu sana au uwe na tabia maalumu sana ndipo Mungu akutumie Hapana ! unapomchunguza Yuda utagundua ni kwa neema na rehema na wala si kwa matendo tunastahili Baraka za Mungu

Matatizo ya Yuda
Mwanzo 37:26 Yuda alihusika kwa kiwango kikubwa pia katika miakakati na mipango ya kumuuza Yusufu ndugu yake, ilikuwa ni kama ana huruma na ujanja wa kumuokoa Yusufu asiuawe, lakini Bado anawajibika kwa mkiwango kikubwa katika uovu wa kumuuza ndugu yake wa Damu awe mtumwa.

Mwanzo 37:31-35 Yuda na ndugu zake, wakiwa wamejikausha walishiriki wazi katika kusema uongo kwa baba yao kuhusu Yusufu, kumbuka wote walikubaliana waseme ameliwa na mnyama mkali,kumbuka zilikuwa ni habari za msiba wa kuumiza kwa Israel Baba yao, Yuda alishiriki utayari wa kumuaminisha Israel kuwa mwanae amekufa na kunyamaza na uongo huo kwa miaka zaidi ya 13, huku mzee akilalamika kupoteza mwana mpendwa, Kama amri ya kuwaheshimu wazazi ili upate heri na miaka mingi duniani Yuda alikuwa amaeharibu tayari

Mwanzo 38:1 Yuda huyuhuyu ulipofika wakati wa kuoa, Yeye aliamua kuoa mwanamke mkanaani , hii ilikuwa kinyume na tamaduni za Israel na Isaka na hata Ibrahimu, wote wliona umuhimu wa kuoa kwao lakini yeye hakuona umuhimu huo kwake mwanamke ni mwanamke tu alioa mkanaani
Mwanzo 38:7-10 Yuda kupitia mwanamke huyu mkanaani alipata watoto, wa kiume, lakini wawili kati yao mungu aliwaua mapema kwa sababu walikuwa waovu mbele za Bwana bila shaka unakumbuka Eri  na Onani, Unadhani nani anawajibika na uovu wa watoto hao? Utasema ni mwanamke mkanaani sawa lakini nani aliyemuoa? Na wanapouawa wanao unaowategemea nani anapitia uchungu?

Mwanzo 38:12-16 Yuda alikuwa ni mtu aliyeshindwa kuutawala mwili, aliongozwa na tamaa ya mwili, alifiwa na mkewe sawa , lakini anakwenda njiani anaona mwanamke kahaba anaingia kwake akifikiri ni kahaba, hakuwa na muda wala hata umakini wa kuangalia mwanamke huyo ni nani alitimiza tamaa yake na kuondoka zake

Mwanzo 38:24-30 Yuda alukuwa na moyo wa Kuhukumu, angalia kuwa analipogundua mkwewe Tamari ana mimba, hata pamoja na kuwa ndiye aliyemwekea mtego kwa kujifanya kahaba kwa sababu hakumpa haki zake, Yuda anawajibika kwa matendo yake ya hukumu akiamuru apigwe kwa mawe huku akiwa amesahau kuwa na Yeye ni mzinifu tu, ashukuriwe Mungu kuwa Tamari alimtaja mtu aliyempa mimba na kuonyesha ushahidi, na kupitia uhusiano huu wa kijinga na wa aibu kunazaliwa Mapacha  na mmoja anaingia katika mstari wa kutuletea Masihi Mathayo 1:3

Unamwangaliaje Yuda? Je ni kama asiyefaa kabisa kutumiwa na Mungu? Angelikuweko leo katika makanisa yanayojiita ya kiroho angetengwa na kufungwa kwa siku kadhaa, au anagefukuzwa kanisani na maadiko yangetumika kuwa hizi ni nyakati za agano jipya ni tofauti na zamani za ujinga? Na ingesahaulika kuwa mwanadamu ni yuleyule kihistoria, Ukweli kwa Mungu unabaki palepale Mungu alikuwa ana mpango naye, Mungu alikuwa anashughulika naye amfanye kuwa Baraka kwa wengine Mwanzo 49:8-12 

Yuda alikuwa kama pande la Mti usiofaa na Mungu alikuwa na Mpango wa kuuchonga ufae kwa kazi zake, Kama ni mwanafunzi mzuri wa Biblia utagundua kwa haraka kuwa wako wengi waliotumiwa na Mungu kwa namna na viwango vya kipekee, lakini maisha yao yakiwa yamepitia katika mpango mbaya wa kusikitisha na kuumiza

Rahabu aliyekuwa kahaba wa kutupwa katika mji wa Yeriko alimjua Mungu na akawa miongoni mwa hao waliomleta masihi (Joshua 2:1 Mathayo 1:5)
Ruth aliyekuwa mpagani na kutokea kabila la madui wa Israel alimjua Mungu na kuingia katika mstari wa waliomzaa Yesu

Daudi wa ukoo huo huo wa Yuda aliyezini na kuua kupitia Bathsheba anamzaa Sulemani ambao wote wanaingia katika Mababa waliomleta Yesu Kristo
Mathayo aliyekuwa Mtoza ushuru, aliyeajiriwa na serikali ya kirumi, watoza ushuru walijulikana kama wezi, waongo, na wadhalimu, wasaliti, Mungu alumuokoa na kumtumia kwa utukuifu wake ikiwamo kuandika injili Mathayo 10;3 akawa miongoni mwa Mitume
Paulo mtume akishuhudia yeye mwenyewe kwamba alikuwa mwenye dhambi, mtukanaji na muongo Itimotheo 1:12-15 na Matendo 26:9-11

Je ninani nanastahili kuwa Muhudumu wa Agano jipya? Paulo mtume anasema Mungu ndiye atustahilihishaye 2Wakoritho 3:5

Ndugu zangu Mabadiliko ni Mchakato, tunapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi katika maisha yetu uhalisia wa maisha hugawanyika katika maeneo makuu matatu, kuna mabadiliko ambayo utayapokea mara moja Instant na mengine utaanza kukamilishwa taratibu na hatimaye utakamilika katika kifo, Instant Sanctification, Progressive sanctification and Perfect Sanctification !

Mwanzo 43: 1-9 Maisha ya Yuda baada ya miaka yalikuwa yamebadilika kabisa, Yuda aliyekuwa na Ubinafsi,Uasherati, Umimi choyo na kuhukumu sasa ameacha kabisa kujifikiri mwenyewe

Anafikiri kuhusu Familia yake yote anajua kuwa wanahitaji chakula ili waishi, anafikiri kuhusu Familia yao na maisha yao ya baadaye watakuwaje

Anafikiri kuhusu Ndugu yake Simeon ambaye amefungwa na Yusufu anafikiri namna atakavyomrudisha nyumbani lakini sasa ni lazima waende na Benjamin

Yuda amabye alikuwa hafikiri sawasawa sasa  amekuwa na ushawishi yuko tayari kuyatoa maisha yake kwa  Usalama wa Simeon, Benjamin, Baba yake na Familia nzima, yuko tayari kubeba lawama za wote milele kama hatathibitisha uaminifu kwa baba yake Yuda sasa Amekuwa amekomaa
Mungu hutumia majaribu na mapito kadhaa katika maisha kutubadilisha kitabia Yakobo 1:12, 1Petro 6-7
Mungu wakati wote ana mpango wa kukamilisha ndoto zetu na makusudi yake katika maisha yetu yuko tayari kugharimika kwa namna yoyote katika kuhakikisha kuwa kusudi lake ndani yetu linatimia uisnihukumu, nisikuhukumu, tusihukumiane kabla ya wakati Mungu ni Mfinyanzi na sisi tu Udongo maadamu tuko mikononi mwake atatugeuza kokote apendako Yeremia 18:1-6

Yuda yuko tayari kuwa Mtumwa kwa aajili ya Ndugu yake na Baba yake mzazi ndugu Yakobo wasiumizwe Mwanzo 44:33, Yuda alikuwa mwenye moyo wa toba sasa na mwenye kuamini katika hukumu za Mungu na kisasi cha Bwana Mwanzo 44;16

Mungu atatutumia kwa kiwango cha juu na kutufanya Baraka tutakapofikia katika badiliko kuu ambalo yeye amelikusudia Wagalatia 4:1-5 tusikubali kubaki kama watoto wadogo tuliodumaa Mungu anatutaka tukue na kubadilika 1Petro 2;2 2Petro 3;18 Waebrania 5:11-61 Biblia inatutaka tukue

Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote.

Maoni 1 :

Unknown alisema ...

Hoja hapa ni kwa nini alistahili kuzivunja zile muhuri saba? Zili muhuri saba ni nini?