UTANGULIZI.
Shule
ya watenda kazi ni shule maalumu inayoandaa na kuweka tayari watu
waliookoka kuwa tayari kumtumikia Mungu
au kufanya kazi Pamoja na Mungu Huwezi kutenganisha wokovu na kumtumikia Mungu
Tumeokolewa ili Tumtumikie Mungu, Mungu alipo waokoa wana wa Israel Kutoka
katika Nchi ya utumwa alirudia mara kwa mara kusudi la kuwaokoa kuwa ni ili wamtumikie
fuatilia mistari hii (Kutoka 7;15-16.
8;1,20.9;1,13,10;3) Kumtumikia Mungu ni jukumu letu kuu kwa sababu sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu (1Koritho 3;9a) Hivyo mungu anatutegemea kama sisi nasi
tunavyomtegemea.
Mapenzi ya mungu ni kuwaona watu
wanaokolewa kwa wingi na kuacha maovu jukumu hili ametupa (Ezekiel 33;11,18;23,32.Timotheo 2;4,2Petro 3;9) Bwanawetu Yesu
alikuja kufanya mapenzi ya Mungu (Yohana
5;20,4,34).Pia alihubiri na kufundisha kila mmoja wetu kufanya mapenzi ya
Mungu (Mathayo 7;21,12;50,2;28-31,Luka
12;47-48).
Ni wajibu wa kila mtu aliyeokolewa
kubeba mzigo wa kuona watu wanaokolewa na wanadumu katika imani,hili ni jukumu
la kujivunia sana ,Mungu katika hekima yake hakuwapa malaika kazi hii alitupa
sisi wanadamu kwani sisi tunao ushuhuda,Malaika wanaitamani sana lakini Mungu
kwa heshima kubwa ametupa sisi jukumu hili (Mathayo 28;19-20).Yeye
Mungu hufanya kazi siku zoote na hufanya kazi kuliko sisi,yeye kama baba yetu
ni muhimu sisi tukifanya kazi pamoja nae (Marko16;20,Matendo
8;1,4;29-35,11;19-21) Wenzetu nyakati za kanisa la kwanza walikuwa hodari katika kulitimiza kusudi hili
loa kumtumikia Mungu
Hivyo basi kila mtu aliyeokoka ana jukumu
la kufanya kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu huduma ya kiinjilisti kwa gharama
yoyote bila kukwepa (Mithali
24;11-12,Yakobo 5;19-20),Hili si
jukumu la wachungaji peke yao ni jukumu la kila mmoja wetu,Tunapoendelea
kujifunza shule hii ya uinjilisti au shule ya watenda kazi tutajifunza masomo
maalumu yatakayotupa hekima katika kuzivuta roho za watu shule hii itakufanya
utoke katika hatua moja ya ukristo na kuingia katika heshima ya kufanya kazi na
mungu hivyo kila anayehitimu shule hii tunamtegemea atakuwa mtu mwenye uewzo wa
kuwaleta watu kwa yesu na kusimamia kuendelea kwa watu waliookoka kukulia
wokovu hivyo unakua ni mtenda kazi pamoja na mungu na pia ni mtenda kazi pamoja
na watumishi wa mungu shambani mwake ,Hivyo unapohitimu shule hii wewe si
mkristo wa kawaida bali ni Mtenda kazi katika Shamba la Bwana (2koritho 8;2324) watu hawa wanapaswa
kuonyeshwa upendo na heshima kwani watakuwa wkitaabika kwa ajili ya watu wa
Mungu kwa ajili ya kutenda kazi kwao
katika kanisa watu hawa ni washirika wa karibu na Mtumishi wa Mungu kwani
kuchapa kazi kwao kunaweka nafasi kubwa katika kutoa nafasi kwa mtumishi
kuutafuta uso wa mungu na kulihudumia lile neno na kufanya maombezi kwa ajili
ya Kondoo woote kwa ujumla na kushauri wale wanaokuja kwa ajili ya ushauri na
maombezi kazi hii ni pana na inahitaji watenda kazi wengi,Mungu akubariki kwa
kupata neema ya kuingia katika shule hii au kupata muhktasari wa masomo haya na
kujisomea na kuyafanyia kazi yoote yaliyomo katika masomo haya wako katika
Utumishi Mchungaji Innocent Kamote.
Mungu ataipima Kazi ya kila mmoja wetu Duniani
Somo maalum shule ya watenda
kazi
Somo; KUPIMWA KWA KAZI YA KILA MTU
Ni muhimu kufahamu kuwa watu tuliuookolewa
tumeokolewa ili tumtumikie mungu,na kuna thawabu kubwa tutakazizipata mbele za
Mungu kwa kumtumikia,Thawabu hizi zitatolewa kulingana na utendaji kazi wa
mtu,kwa hivyo kazi kazi ya kila mkristo itapimwa tutajifunza spmo hili kwa
kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-
·
Kusudi
la kuokolewa
·
Utumishi
aliopewa kila Mtu aliyeokoka
·
Kupimwa
kwa kazi ya kila mtu
·
Baraka
ya kufanya kazi ya mungu kwa hiyari
·
Faida
za kuitenda kazi ya Mungu.
Kusudi la kuokolewa.
Hatuna
budi kufahamu tene na tena kuwa mara baada ya kuokolewa kwa kumkiri Yesu Kristo
kama bwana na mwokozi wetu,sio mwisho wa kila jambo bali tumekubali kuwa
wayumwa wake naye ni mtawala wetu,kwa sababu ametununua kwa damu ya thamani
hivyo tunao wajibu wa kumtumikia,Kusudi letu la kumtumikia Mungu halitofautiani
na lile Bwana alilokazia alipokuwa akiwaokoa Waisrael kule Misri (Kutoka 7;16) Kwa msingi huo katika maisha yetu ya wokovu ni muhimu sana
kutumika Kutumika sit u kuna thawabu bali kunatusaidia kukua kiroho na kukomaa
katika utumishi na pia kunaendelea kututakasa,Mungu ameweka mkazo katioka swala
zima la kumtumikia (Kutoka 8;1,20;9;1,13)
jambo hili kwa jinsi mungu alivyolikazia lilipelekea hata farao kutambua kusudi la Waisrael kuitwa
na Mungu wao (Kutoka 10;11,10;26),
Na mataifa pia yalitambua kuwa Mungu wa Israel ni Mungu wa pekee aliye wapenda
) makanisa mengi sana leo yako nyuma na hayaongezeki kiidadi kwa sababu
wameacha kutilia mkazo swala la
kumtumikia Mungu na kuwaachia wachungaji peke yao (Matendo
2;18,8;1,4,2Timotheo 2;2)
Utumishi aliopewa kila Mtu
aliyeokoka.
Kila
mtu aliyeokoka ni mtumishi na amepewa utumishi na analazimika kuhubiri na
kufundsisha ,hata kama ana umri mdogo (Yeremia
1;4-8) Mungu huweza kutuita hata tuikiwa katika umri mdogo kama apendavyo
kwa ajili ya kazi yake (marko 16;15),Licha
ya kuwa tumeagizwa kuihubiri injili ,kila mtu aliyeokoka ni tawi la mzabibu
ambaye ni Yesu hivyo Bwana anatutarajia tuzae matunda (Yohana 15,2,6) Hivyo kuna hatari ya kutupwa nje kama hatumzalii
Bwana matunda, Kadiri tunavyomtumikia Mungu ndivyo na kuzaa sana ndivyo
Anavyotukuzwa (Yohana 15;8,Luka 15;10,7)
Yesu alihakikisha alipokuwa duniani baba yake anatukuzwa,ni namna gani tunaweza
kumtukuza Mungu ni kwa kuhubiri injili na kuwafuatilia waliookoka kuwafundisha
ili waukulie wokovu na kudumu kazi hii ndiyo inadhihirisha kuwa Tunampenda sana Bwana (Yohana
21;15-17) neno lisha humaanisha kufundisha na chunga ni kutoa huduma za
kichungaji kwa kondoo wa Mungu wenye mahitaji mbalimbali, Bwana atupe neema ya
kumtumikia.
Kupimwa kwa kazi ya kila mtu.
Pamoja na kuwa tumeokolewa ni muhimu
kufahamu kuwa watu waliookoka watahukumiwa kulingana na matendo yao,kazi ya
kila mtu itapimwa,na kila mmoja atakuwa na utukufu wa tofauti mbinguni kwa sababu ya utumishi wale waongozao wengi
katika kutenda haki watang’aa kama Mwangaza wa anga (Daniel 12;3,Mithali 11;30). Woote
tunaweza kuingia mbinguni lakini kutakuwa na madaraja tofauti kulingana na kazi
mungu ni mwenye haki (1Timotheo 3;13)
kwa msingi huu basi kazi ya kila mmoja itapimwa ili kuamua kwa haki nani
anastahili nini (1Samuel 2;3.1Koritho
3;11-15 Warumi 14;12) kwa msingi
huo basi itakuwa aibu kuifanya kazi ya mungu kilegevu(Warumi 12;11,) na ni lazima kukamilisha kazi(Yohana 4;34),Makanisa mengi hufanya kazi kubwa nay a gharama
yakuwaleta watu kwa Yesu kasha hubakia kufurahia idadi ya watu waliookoka na
kufurahia bila kukamilisha kazi kwa kuwalea watu wa Mungu waliookoka kwa
kuwafuatilia na kuwafundisha ili wadumu katika Imani tusipofanya hivyo kazi
yoote tuliyoifanya inakuwa ni Bure au kazi isiyokamilika (1Lonike 3;5)
Baraka ya kufanya kazi ya Mungu
kwa hiyari.
Mungu atatupa ujira au ijara kwa ajili ya kazi
hii tuifanyayo (2Nyakati 15;7),hata
hivyo hatuna budi kuifanya kazi hii kwa hiyari,Mungu huwabariki watu
wanaoifanya kazi yake kwa hiyari na si kwa kusukumwasukumwa(1Nyakati 29;14-18,6),Ni muhimu
tukitumika huku tunajua yakuwa kazi hii tunayoifanya ni ya Mungu na sio ya
mwanadamu (1Koritho 9;16-17),kuna
tofauti kuifanya kazi hii kwa hiari au kwa sharti kwa hiyari inathwabu kubwa
sana sisi tumeitwa kuifanya kazi hii kwa hiyari
Faida za kuitenda kazi ya
Mungu.
Wanafunzi wa Yesu walimuuliza kuwa baada
ya kuwa wameifanya kazi hii watapata nini basi? Kuna malipo makubwa kabisa
Heshima ya kumtumikia Baba itatuweka pale Kristo atakapokuwa (Yohana 12;26,Kutoka 23;25-27) Tutapata
mema mengi hapa duniani na mbinguni ziko ahadi nyingi sana kwa watu woote
wanaomtumikiaMungu,ataondoa magonjwa ,hapatakuwa na aliye tasa na mbinguni
tutalipwa mara mia (Mathayo 19;27-29)
Somo maalum shule ya watenda
kazi.
Somo: UMUHIMU WA KUFANYA
UFUATILIAJI.
Upo umuhimu mkubwa sana wa kufanya
ufuatiliaji kwa ajili ya kuwafuatilia watoto wachanga wa Kiroho ,Kazi hii ni ya
muhimu kuliko tunavyofikiri (Matendo
15;36), Makanisa mengi na watumishi wengi wa Mungu hufanya kazi nzuri ya
kuhubiria watu injili ya wokovu na watu wanaokolewa kwa wingi,Hata hivyo kazi
hii haiwezi kuwa kamili kama utaondoa ufuatiliaji Ni makusudi basi ya Roho wa
mungu kutufundisha somo hili ili kazi tunazozifanya za kuhubiri injili ziweze
kuwa kamili.Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-
- Urahisi wa kuua kiumbe katika wakati wa uchanga
- Jinsi ya kuwaficha watoto wachanga wa kiroho
- Sababu zinazopelekea watoto wachanga wa kiroho kuuawa.
- Jinsi inavyochukiza Mbele za Mungu mmoja apotee.
- Umuhimu wa kufanya ufuatiliaji.
Urahisi wa kuua kiumbe katika
wakati wa uchanga.
Ni muhimu kufahamu kuwa ni rahisi kuua kitu
katika uchanga kuliko kikiwa kimekomaa,Mmea mchanga unaweza kuuawa kirahisi
unapokuwa mchanga hata kwa kukanyagwa na
kuku tu , Takwimu nyingi zinaonyesha kuwa Barani Afrika vifo vingi vya watoto
vinavyotokea ni vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitani mapaka
sifuri,Mtoto mdogo aweza kufa hata kwa kumlalia vibaya tu (1Falme 13;16-19),katika malezi watoto wanahitaji uangalifu mkubwa
sana,kinga zao zinakuwa bado hazijaweza kustahimili magonjwa ya dunia,watu
waovu wenye tabia ya kupenda kutoa mamba hupendelea kutoa mamba ikiwa changa
kuliko ile iliyokomaa Kwa ufahamu huu kuwa ni rahisi kuua kitu katika uchanga
wake shetani hupendelea kuwaua watoto wachanga wa kiroho kabla
hawajakomaa,mpango wa Shetani kumuangamiza Yesu au Musa ulifanywa na shetani mapema katika uchanga
wao (Kutoka 1;15-18,22,2;1-6,Math
2;13-16) Mtu nanapookoka hata kam ni mzee katika hatua zake za mwanzoni za
wokovu ni mtoto mchanga kiroho (1Petro
2;2).
Jinsi ya kuwaficha watoto
wachanga wa kiroho
Ni muhimu basi kanisa likawa na mkakati
kabla hata ya mikutano ya injili kuwaandaa watenda kazi ambao watakuwa tayari
kuwafuatilia watoto wachanga kiroho,aidha kanisa ni muhimu likafahamun kuwa
baada ya mkutano kwisha sio ndio muda wa mapumziko umewadia hapana ndio kwanza
kumekucha na kazi inaanza,katika wakati huu watu wengine maalumu watakuwa
wakiwaomea watoto hao wachanga kiroho,na watenda kazi wakifanya ufuatiliaji
haraka sana mara baada ya kuokolewa kwa
watoto hao kabla ya saa ishirini na nne (IThesalonoke
3;5,2Koritho11;3) ni Vema basi tukaanza kuwanyonyesha mara moja wanapokuwa
wamezaliwa hakuna mama anayezaa kasha akaanza kunyonyesha siku ya tatu au ya nne,Tuwaombee na kuanza
ufuatiliaji mara moja.
Sababu zinazopelekea watoto
wachanga wa kiroho kuuawa.
Kwa nini Watoto wengi wa kiroho
hawaendelei na wokovu mara wanapokuwa wameokoka,moja ya sababu ni kuwa Shetani
hakati tama wala hapumziki Yeye hufanya ufuatiliaji haraka kabla mtendakazi
hajafanya ufuatiliaji woote tunakumbuka siku wana wa Israel walipotoka Misri
kuwa farao alifanya uamuzi wa kuwafuatilia kabla hata hawajafika kokote ili
awarejeze tena utumwani ndani ya masaa 24 (Kutoka
14;9-10,Ebrania 5;13-14,2Koritho 11;3)
Mtoto mchanga kiroho ni rahisi kuuawa kwa sababu hawajui sana neno la haki
nirahisi kudanganywa hata kwa maneno ya kawaida na kukata tama bado hawana
silaha zote za mungu za kuwasaidia kupambana (Efeso 10-18) kwa hiyo katika uchanga wake hajui vita vya kiroho
wala namna ya kutumia silaha,Mungu alipowaokoa wana wa Israel alitaka wajue
vita (Kutoka 13;17-18).
1. Wavae kweli yaani neno la Mungu
(Yohana 8;12)
2. Wavae dirii ya haki ,matendo ya
haki (Matendo 22;25-29)
3. Wawe na ngao ya Imani (warumi 1;17)
4. Wavae chepeo ya wokovu yaani
wawe na hakika ya wokovu ( Zaburi 103;12)
5. Awe na upanga war oho kujua
namna ya kulitumia neno (mathayo 4;4-11)
6. Ajue kuomba na kujaa roho
kunena kwa lugha
Watoto
wachanga wa kiroho wakifikia hatua ya kuyajua hayo wanakuwa na nafasi nzuri ya
kuendelea mbele,Mambo hayo hayawezi kufanyika kwa wiki moja tu yanahitaji muda
Jinsi inavyochukiza Mbele za
Mungu mmoja apotee.
Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali anataka
watu woote wafikie toba (2Petro 3;9.Marth 18;14,1Falme 20;39-40,Ebrania
2;13) Ikiwa Mungu anachukizwa kwa mmoja kupotea kama watenda kazi
tunapokuwa tumekabidhiwa watoto wachanga wa kiroho na kuwafuatilia Mungu
anakuwa ametukabidhi ili tuwalee kwa niaba yake (Math 25;33-40) na
tunapowaacha hata wakafa kiroho bila kuonyesha jitihada zozote Damu yao
itatakwa mikononi mwetu (Ezekiel 3;17-19)
Umuhimu wa kufanya ufuatiliaji.
Katika hali ya kawaida mama aliyezaa
atahakikisha anamtunza mtotop aliyemzaa kwa gharama yoyote (Wagalatia 4;1-2,4;19-20,1Thesalonike 3;5),Hakuna
jambo muhimu wakati wa mavuno kama ufuatiliaji,Lazima tuhakikishe
tunawafuatilia kwa ukaribu na kujua mahitaji yao na kuanza kuwafundisha neno la
Mungu ,tusikubali kuridhika na semina za kanisani pekee mwalimu wa ufuatiliaji
anapaswa kuwa makini kuwa mtoto wake wakiroho anapitia mazingira gani kasha
kumfundisha masomo ya mwanzo ya wokovu ambayo ni maziwa yasiyoghoshiwa,huku
tukikwepa kuwafundisha vitu vigumu kama kupunguza wake zake iwapo ana wake
zaidi ya mmoja n.k.Wakati wa ufuatiliaji ni wakati wa kujikana nafsi kwani
iakulazimu kupanga ratiba na mwanafunzi wako na hivyo itakulazimuni wakati
mwingine kukutana saa ambazo umetoka kazini,wanafunzi hao wa kiroho wanahitaji
uvumilivu mkubwa kwani wengine watakuwa bado wanakwenda katika makanisa yao ya zamani,na wengine
ukuaji wao ni wa taratibu sana na wengine haraka,wengine itakulazimu kuwasaidia
kazi ndogondogo n.k. somo lifuatalo
Somo maalum shule ya watenda
kazi
Somo: GHARAMA ZA KUFANYA
UFUATILIAJI.
Katika hali ya kawaida mtu anapojifungua
mtoto pamoja na furaha ya kuzaliwa kwa mtoto huyo kutakuweko Gharama za malezi
ya mtoto huyo mapaka pale atakapoweza kujitegemea,Mambo hayo yanafanana na mabo
ya rohoni ,Watu wanapookolewa kunakuwa
na Gharama za kuwalea mpaka waweze kujitegemea kiroho ni kwa msingi huu Roho wa
mungu anataka tujifunze somo hili sasa gharama za ufuatiliaji tutajifunza somo
hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-
·
Gharama
kubwa huambatana na chochote chenye faida
·
Ulinganifu
wa malezi ya watoto wa changa kiroho na
kimwili
Gharama kubwa huambatana na
chochote chenye faida
Kama tulivyogusia katika utangulizi kuwa
katika hali ya kawaida wazazi watakuwa na furaha ya kuzaliwa kwa mtoto, lakini
swala la kugharimika kwa malezi liko palepale,Kadhalika katika hali ya kiroho,
baada ya watu kuokolewa hatupaswi tu kushangilia mavuno pekee bali tunapaswa
kufahamu kuwa tunawajibu wa kuwalea au kuwafuatilia katika wakati huu tutagharimika kwa mambo mengi kama
kuwafuatilia ,kujikana nafsi kuwa na muda nao,ili kuwafundisha ,kujitoa kwa
nauli au kuwatolea nauli ili waje kanisani,kuwatolea kopi za masomo ya mwanzo
ya wokovu,kuwaombea,nk.kwa ujumla ufuatiliaji unagharama,Lakini kugharimika
wketu si bure ,Kuna heshima kubwa sana ,Wakati wa kunyakuliwa tutakuwa kama
kuku anayeambatana na Vifaranga vyake,wale woote ambao tuliwasaidia kusimama
katika wokovu watatuzunguka (2Timotheo
2;6).Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa kitu chochote chenye Thamani
kina gharama kubwa sana (2Samuel
24;21-25) Tunapopata taabu kwa ajili ya kazi ya bwana tutakuwa wa kwnza kupata matunda(2Timotheo 2;6,Zaburi 126;1-3,5-6;Yohana
16;21-22,2Thesalonike 2;19-20).
Ulinganifu wa malezi ya watoto
wa changa kiroho na kimwili
Watoto wachanga wa kimwili wanahitaji
maangalizi ya karibu na watoto wa kiroho, pia tunapaswa kuwaangalia sana,
Chakula cha watoto wa kimwili ni maziwa na chakula cha watoto wachanga wa
kiroho pia ni maziwa ni lazima tuwe
waangalifu tusizungumzie mambo magumu kwao kama ubatizo,utatu,malipizi ya
ndoa,n.k. Kama ilivyo kwa vyakula vya watoto wachanga nivya gharama na watoto
wa kiroho tutagharimika kuwafundisha na kuwahudumia mara kwa mara hata masomo
ya ziada yanayotatua matatizo yaliyonayo,Watoto wadogo ni rahisi kudanganywa
kadhalika watoto wa kiroho pia wahitaji kufundishwa masomo ya kinga kuwalinda
na imani potofu,Watoto hawajui thamani ya vitu (2Koritho 12;14-15,17-18) matoto mchanga ni rahisi kutoa ahadi
lakini ikawa ni vigumu kuitekeleza,Tusijali wala tusi wahukumu,wanahitaji
uvumilivu (Luka 8;15)Itatupasa kuwavumilia katika maeneo mengi hata kiama unamkuta
anacheza dansi usimhukumu kwa haraka,Tunapaswa kujua wanalielewa vipi neno la
Mungu n.k.Watoto huwa hawaridhiki na chakula cha nyumbani kadhalika watoto wa
kiroho wanaweza kurudi katika mapokeo yao tuendelee kusoma nao neno na
kuwafuatilia bila kukata tama wakati mwingine inaweza kukugharimu miezi hata
sita kumfuatilia mtu mmoja kabla hajaonyesha muelekeo,Bwana atupe kuzaa matunda
kwa uvumilivu mwingi.
Somo maalum shule ya watenda
kazi
SOMO: NJAA NA KIU YA KULIONA
KANISA LIKIONGEZEKA.
Mtu awaye yote anapokuwa ameokolewa na
kuifahamu kweli ana paswa sasa kutulia na kuanza kumtumikia Mungu bila
kutangatanga isipokuwa kwa sababu maalumu tu sizizoweza kuzuilika,Pamoja na
kuwa Yesu Kristo ametuweka huru bado hakuna uhuru usio na mipaka ,Lazima
tutulie katika sehemu moja na kuanza kuujenga ufalme wa mungu tuikiwa na njaa
na kiu ya kuliona kanisa tunaloabudu
linaongezeka kwa msingi huo tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia vipengele vinne vifuatavyo;-
·
Njaa
na kiu ya haki.
·
Kuumbika kwa Kristo ndani yetu.
·
Njaa na kiu ya kuliona kanisa linaongezeka.
·
Jinsi ya kufanya ili kanisa liongezeke.
Njaa na kiu ya haki.
(Mathayo
5;6),kuwa na haki ni kuwa na sifa ambazo Mungu anataka uwe nazo,kiu au njaa
ni uhitaji wa nuhimu anaokuwa nao mtu,Mungu kwa kawaida hampi mtu kitu
asichokuwa na haja nacho,chochote tunachokihitaji kutoka kwa mungu lazima
kitanguliwe na kiu na njaa,Watoto wanapotaka kitu kutoka kwa wazazi wao kwa
kawaida huomba na wakati mwingine hulia na kugaragara ,Tunapokuwa na uhitaji
wowote kutoka kwa mungu ni muhimu kwetu kuomba na kumlilia chochote iwe ni
mtoto,Nyumba,Gari, mchumba na karama za rohoni vinapatikana kwa maombi, hii ni
hali halisi katika ulimwengu war oho kuwa lazima tuombe yale tunayotaka
yafanyike katika kanisa letu.Wako watu wengine ambao ni vigumu kuwapata katika
ufalme wa mungu bila miujiza na uponyaji wa aina mbalimbali ni lazima tumuombe
Mungu awatumie watumishi wake kwa vipawa na karama mbalimbali ili wale
wasioamini wapate kuamini kwa neno au kwa tendo(1Koritho 2;4),Hivyo hatuna budi kumuomba Mungu kwa bidii kwa ajili
ya yale yoote ambayo tunataka kuyaona au kuyafanya katika kanisa letu (1Koritho 12;31;4;1).Ni muhimu kumuomba
Mungu na kuugua na kulia kwa ajili ya kukua na kuongezeka kwa kanisa letu.
Kuumbika
kwa Kristo ndani yetu.
Kristo
kuumbika ndani yetu ni jambo la msingi sana ,tunaweza kuwa tumeokolewa Muda
mrefu lakini Kristo akawa hajaumbika
ndani yetu (Galatia 4;19) Kristo
anapoumbika ndani yetu tunakomaa kiasi cha kufikia kuwaza,kusema na kutenda
katika tabia na mwenendo kama Kristo mwenyewe alivyo,Mtu anaweza kufikia hata
ngazi ya utumishi lakini kristo akawa hajaumbika kwa wingi ndani yake Kristo
akiumbika ndani yetu tutakuwa na shauku hamu kiu na njaa kama ile iliyokuwamo
ndani yake.
Njaa
na kiu ya kuliona kanisa linaongezeka.
Mtenda kazi
ambaye Kristo ameumbika ndani yake kwa wingi atakuwa na njaa na kiu ya kuyaleta
mavuno katika ufalme wa Mungu (Yohana
44;6-8,9-15,31-35).Kila siku njaa ya Yesu Kristo ilikuwa ni kumuona mmoja
akiokolewa,kama Kristo ameumbika ndani yetu tutakuwa na hamu ya kumuona mwenye dhambi mmoja akitubu na
kumwamini Yesu (Yohana 1;37-45,Isaya
60;22a,Luka 15,10,7,2Petro 3;9) Kama Kristo ameumbika ndani yetu
hatutapenda Mtu yeyeote apotee,Nyakati za kanisa la kwanza wenzetu walikuwa na
njaa na kiu ya kuona kanisa likiongezeka (Matendo
2;41,4;4,5;14,9;31;12,24,17;4.13;1),
Kanisa la Antiokia kwa mujibu wa waandishi wa karne ya kwanza lilikuwa na watu
laki tano (500,000),walioabudu
sehemu moja nab ado hawakuridhika kuwa na hao tu,ni lazima tusikubali
kuwapoteza watoto wachanga wa kiroho (Yohana
17;12) wala tusiridhike kuwa na watu wacheche,Hili litawezekana kama tu
tutakuwa na watendakazi ambao Kristo ameumbika ndani yao;
Jinsi ya kufanya ili kanisa
liongezeke.
Ø
Ni
lazima tufahamu kuwa wajibu wa kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu sio wa
wachungaji pekee
Ø
Lazima
tumuombe Mungu kila saa na kila siku kwamba Kristo aumbike ndani yetu
Ø
Tumuombe
Mungu awaokoe Ndug,jamaa,marafiki,majirani na wengineo
Ø
Wakati
mwingine tuwaalike kuja kanisani na watakutana na neno hukohuko.
Ø
Tuwashuhudie
katika uinjilisti wetu Binafsi na kuwakaribisha katika makanisa ya Nyumbani au cells
Ø
Tusikubali
kuridhika kuona watu wachache kanisani wakati wa ibada,tuwapitie kuja nao
ibadani huku tukiwasaidia kazi zinazowazuia kuja kwa haraka au kuwafanya
kutolea udhuru.
Ø
Tuwatumie
wale ambao ni wachanga na hawajadumu sana
katika neno wawaalike wengine na kuwaleta kwa Yesu au kanisani (Yohana 1;40-42;4;28-39).
Ø
Tukubali
kuwa katika hali zoote ili tuwapate isipokuwa dhambi
Ø
Tumuombe
Mungu kuumbiwa mzigo wa kuhudhuria Ibada zoote huku tukiwapitia wageni wakiwa
peke yao
wanajisikia kukata tama
Ø
Funga
na kuomba kwa uzito mkubwa kwa ajili yao
na wengine ili Mungu awalete wale waliookoka kwa kumaanisha
Ø
Kama tumewqaalika watu tumuombe Mungu awaokoe wale
woote tuliowaalika.
Ø
Tujitahidi
kuwa nuru ili kuwavuta wale wasiookolewa kama
taa ivutiavyo wadudu
Ø
Tutumie
mbinu zozote tutakazofunuliwa na Roho wa Mungu ili kuwaleta kwake kwa gaharama
yoyote.
Somo maalum shule ya watenda
kazi.
SOMO: MTENDA
KAZI KAMA TAI.
Tai ni miongoni mwa ndege hadari sana ambao sifa zao
zimejaa kwa wingi sana katika Neno la Mungu,Roho mtakatifu huwafananisha
watendakazi hodari na ndege huyu tai,tutajifunza somo hili mtendakazi kama tai
kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-
·
Mtenda
kazi kama tai.
·
Mambo
yatupasayo kufanya
Mtenda kazi kama
tai.
Watu wanaotenda kazi kwa moyo ndio
wanaoitwa wanao mngoja Bwana (Isaya 40;30-31),Waatendakazi ambao wanafanya kazi ya Mungu kwa uhodari
wanafananishwa na tai,Mungu anatarajia kuwaona watenda kazi wakiwa kama tai
wakifanya kazi yake kwa uhodari na si kwa ulegevu (Yeremia 48;10,Warumi 12;11),Juhudi nyingi sana zinahitajika katika
kati ya Mungu kuliko hata ya kaisari,Watuwe ngi hufanya kazi za kaisari kwa
bidii kwa sababu wanaogopa kufukuzwa kazi,lakini kazi ya Mungu huifanya kwa
kusukumwasukumwa, bila juhudi zozote katika roho zao,Nyakati za biblia mtu au
kitu hadari kilifananishwa na tai (Yeremia
4;13) tai hupenda kuishi juu kwa kuyaangalia yaliyo juu,watendakazi nao
wanapaswa kuyaangalia yaliyo juu (2Koritho
4;16-18) Paulo mtume alikuwa mtume hodari yeye alifanya kazi kuliko mitume
woote kwa Muda alioitwa na Roho mtakatifu kufanya hivyo,utu wake wa nje
ulichakaa lakini alifanya kazi sana . Ni muhimu kufahamu kuwa sisi nasi hatuna
budi kufahamu kuwa dhiki zitaambatana nasi katika kazi ya Mungu kwa namna isiyo
ya kawaida, Hata hivyo dhiki hii ni nyepesi ukilinganisha na malipo atakayotupa
Mungu na mambo ya milele.
Waalimu wa ufuatiliaji na watendakazi
kwa ujumla wanatakiwa kuwa wepesi kama tai (Maombolezo 4;19) Tai huwa wepesi sana katika kujua na kufuatilia
mizoga hata bila kupewa taarifa (Luka
17;37),Mizoga ni watu ambao bado hawajaokolewa ambao kwa mujibu wa biblia
wamekufa kwa ajili ya dhambi zao (Efeso
2;1-2).Kuja kwa Bwana kunakaribia hivyo sisi kama tai tutakusanyika naye
siku ile (Luka 17;37,Yuda 1;14,Zekaria 14;4,Ufunuo 19;17-18) hii
maana yake ni muhimu kuwakaribu kihuduma wakati wowote wanapokuwepo wenye
dhambi ili waokolewe iwe ni katika mikutani ya injili au huduma za maombezi na
za kiinjili za ndani (Mathayo
9;35-38,Matendo 13;2).
Roho mtakatifu ndiye Bwana wa mavuno na
ndiye anayehusika katika kuwapeleka watenda kazi katika katika shamba lake
ambao ni sawa na watunzaji wa shamba la mizabibu (Luka 13;6-9,19;13).Kufanya uinjilisti ni sawa na kufanya Biashara (Wimbo uliobora 1;6 1Koritho 3;9;Rumi 10;13-15).Mungu hutenda kazi Pamoja
na wanadamu (Efeso 4;30) Lakini
tunaweza kumhuzunisha na kumkatisha
tama.tunakuwa marafiki na Roho mtakatifu pale ambapo hatutaaacha kukusanyika siku za uinjilisti wetu,Kule kuwa
tayari kwetu humfanya Roho mtakatifu afanye kazi pamoja nasi kama kuokoa na
kuponya na pale ambapo hatutaacha mtu apotee (Mathayo 18;14) .Uamsho katika kanisa unaletwa na upepo yaani Roho
mtakatifu (kutoka 14;21;Yohana
3;6-8,Hesabu 11;31).Upepo ni
Roho mtakatifu. (IThesalonike 5;19).Tunaweza
kumhuzunisha na pia kumzimisha (Zaburi 2;8)Hivyo ni muhimu kumuomba
Roho Mtakatifu ili asituache na huku tukizidi kuwa hodari kama tai.
Mambo yatupasayo kufanya.
Ni muhimu kufahamu kuwa kuokoka au
kuokolewa ndio muujiza mkubwa sana tena ndio wa kwanza kuliko yote, hivyo sisi
kama tai hatuna budi kufurahia mizoga yaani kufurahi na kushangilia pale watu
wanapoamua kuokoka ni lazima tuwafuatilie na kuwatia moyo na kuwaeleza kuwa
uamuzi waliofanya ni wa muhimu na bora na wa busara.Tuwatie moyo kuendelea
mbele na kuhudhuria ibada katika kanisa kuu na makanisa ya nyumbani bila kukosa
kwa gharama yoyote.mungu na atubariki tukiyatenda.
Somo maalum shule ya watenda
kazi.
SOMO: MISINGI YA UFUATILIAJI
Katika
ufuatiliaji iko misingi ya muhimu ambayo tunapaswa kuizingatia kama watendakazi
na waalimu wa ufuatiliaji, Bwana atupe neema ya kuizingatia Misingi hiyo na
kuzidi katika jina la Yesu.Tutajifunza somo hili misingi ya ufuatiliaji kwa
kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-
- Madhara ya mwalimu wa kwanza
- Yatupasayo kufanya kabla ya kufanya ufuatiliaji.
- Umuhimu wa ufuatiliaji katika saa ishirini na nne (24).
- Umuhimu wa kufanya utafiti wa mwanzo.
- Kuzaa matunda kwa uvumilivu.
Madhara ya mwalimu wa kwanza
Wengi wetu tuko hivi tulivyo kutokana na
mwalimu wetu wa kwanza,Kama wazazi wetu wanazungumza lugha Fulani lugha hiyo itapandikizwa katika hatua za
mwanzoni.katika hatua za mwanzoni ni rahisi kupandikiza chochote iwe ni kitu kibaya au kizuri ,mwalimu wa
kwanza anauwezo wa kupandikiza tabia yoyote na kuipandikiza ndani yetu (Ezekiel 16;44-45) Mwalimu wa kwanza ana
nafasi ya tabia yake kuigwa na wale anaowafundisha ,Mfano kama mwalimu wa
darasa la kwanza atakuwa na mwandiko mbaya
upo uwezekano wa wanafunzi wake kuwa na mwandiko mbaya na ndio maana ni
vizuri kuumba mwandiko,Inchi nyingi za Afrika zimeiga tabia ya inchi zile ambazo zili tutawala.Mambo hayo ndivyo
yalivyo katika ulimwengu wa kiroho mwalimu wa kwanza wa kiroho anaweza
kuwaambukiza hata sauti yake au lolote katika tabia usemi na mwenendo n.k.
Mwalimu wa kwnza ana nafasi ya kubwa ya
kuleta madhara makubwa kwani kama vile
alivyo ndivyo na mtoto wake wa kiroho
atakuwa vilevile (2Timoth 1;5),Hata imani ya mtu hutokana na
wazazi au waalimu wa kwanza ndio maaana maandiko ya natuonya kuwa kielelezo kwa
waaminio kwani mwalimu wa kwanza wa ufuatiliaji ana uwezo wa kusaidia kujenga
kanisa zuri au kuliua (Rumi 11;16),Tunapokuwa waalimu wa
ufuatiliaji tunakuwa tumetumwa na Roho
mtakatifu,Hivyo ni muhimu kuepuka
kuwa kikwazo kwa tunaowafuatilia,ikiwa hatutakuwa
kielelezo na kuwa mbali na dunia
tunaweza kuwa kwazo,Haki yetu inapaswa izidi ile haki ya mafarisayo (Math 5;20,1Tomoth 4;12) ni muhimu kuwa
kielelezo katika usemi,mwenendo imani na
usafi,ikiwa tutawakwaza mojawapo ya wadogo hawa
Damu yao itatakwa mikononi mwetu.Bwana ampe neema kila mtendakazi kuwa na hekima na kuifanya kazi hii
tuliyouitiwa na kuzidi katika jina la Yesu.
Yatupasayo kufanya kabla ya
kufanya ufuatiliaji.
(1Thesalonike 3;10) Hatuna budi kuomba
usiku na mchana ili wale tunao wafuatilia wasimame katika imani,kuomba ni sawa
na kumwagilia maji (1Koritho 3;6,Luka
22;31-32) Bila maombi ya kutosha
watoto wetu wachanga kiroho hawataweza kubadilishwa (Converted) na hatimaye
wataiacha imani.Hivyo maombi ni muhimu sana .
Umuhimu wa ufuatiliaji katika saa
ishirini na nne (24).
Kama tulivyogusia katika masomo mengine
ya awali shetani adui wa Mungu na watu wake hatafurahia kuona mtu aliyeokolewa
akiendelea na kudumu katika wokovu,hivyo yeye huanza ufuatiliaji katika masaa
24 tu mara baada ya mtu kuokoka hii ni kama vile farao alivyowafuatilia wana wa
Israel walipotoka Misri kwa wokovu ndani ya saa 24 tu (Kutoka 14;5-7,9-10) siku ileile shetani atataka kumrudisha nyuma
mtu aliyeokoka Kwa msingi huo tusipo mfuatilia
mtoto mchanga kiroho katika kipindi cha saa 24baada ya kuokolewa
tunakuwa tumempa nafasi shetani kufanya kazi kubwa ndani ya saa hizo na
kuwarejesha nyuma au kuifanya kazi ya ufuatiliaji kuwa ngumu.Kwa msingi huu ni
muhimu kulifuatilia hili na kuwatia moyo na kuwafundisha masomo ya mwanzo ya
wokovu yale yaliyo muhimu.
Umuhimu wa kufanya utafiti wa
mwanzo.
Ni muhimu kuwa na hekima katika hatua za
mwanzoni kabisa za ufuatiliaji ili tupate matokeo mazuri.Kwa msingi huo utafiti
wa mwanzo kwa mtu tunayemfuatilia ni wa Muhimu,ni lazima tujue kuwa mtu huyu tunaemfuatilia Je amezaliwa
mara ya pili? Na tunaweza kumfahamu mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa kuzingatia
vigezo vifuatavyo
Ø
Mtu
aliyezaliwa mara ya pili huonyesha furaha, kulipenda neno la Mungu na
kutokuonea haya wokovu,atawekewa ndani yake kuchukia dhambi (1Koritho 2;14). kwa kawaida mtoto wa
Ibilisi hapendi neno la Mungu.(1Yohana
4;8)
Ø
Roho
wa Mungu atashuhudia ndani yake kuwa ameokoka na amekuwa mwana wa Mungu (Rumi 8;1,16,Luka 1;77,1Yohana 2;6-27).Ni
muhimu pia kufanya utafiti wa kimwili mkuwa mtu tunayemfuatilia yukoje
Anacheo,Msomi,Tajiri,Umri mkubwa kuliko wako,n.k.Endapo utagundua hayo ni
vizuri kutafuta mtu wa aina kama yak wake ili waweze kuendana kifikira kihali
na kijinsi na umri ili wasionyeshe dharau kwetu,kama ni wasomi ni muhimu
akifuatiliwa na msomi mwenzie (Amosi
3;3).
Kuzaa matunda kwa uvumilivu.
(Luka 8;15) Wakati mwingine itatulazimu
kuvumilia tunapofanya ufuatiliaji,watoto wengine wa kiroho huchukua muda mrefu
sana kukua Mchungaji mmoja Jimmy Sakuye wa FGBF Arusha wakati akiwa
mshirika alimfuatilia mtu mmoja kwa miezi sita kwa shida sana kwani wakati mwingine mtu huyu
alikuwa akienda kwenye dini yake ya mapokeo Sakuye alivumilia na kuendelea
kumfuatilia mtu huyo sasa ni Askofu wa
jimbo Mwanza FGBF David Chamoto hii inatufundisha kuwa Nyakati nyingine
itatugharimu kwani watoto wengine hukua
kwa shida sana inatupasa kuwa wavumilivu,Kuna kuwaombea kuwavumilia
wanapoonyesha mambo ya kidunia au kusakata dansi kupiga wake zao n.k hayo yoote
yanahitaji uvumilivu mkubwa na upeo mkubwa wa Kiroho. Bwana ampe kila mmoja
wetu neema ya kuzaa matunda kwa uvumilivu katika jina la Yesu Kristo amen.
Somo maalum shule
ya watenda kazi.
Somo: HEKIMA NA MAARIFA YA
UFUATILIAJI.
Katika
kuwafuatilia watoto wachanga kiroho kunahitajika hekima na maarifa namna ya
kuingia na kutoka mbele zao ili kusudi tusiweze kuharibu kazi na mpango mzima
wa Roho Mtakatifu wakati wa ufuatiliaji tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vinne vifuatavyo;-
- Hekima ya kuwafuatilia waliotaka maombezi tu.
- Hekima ya kuwalea watoto wachanga wa kiroho.
- Mpangilio wa masomo ya mwanzo ya wokovu
- Jinsi na namna ya kuwafundisha.
Hekima ya kuwafuatilia
waliotaka maombezi tu.
Ni muhimu kufahamu kuwa wako watu wengine amabao wanakuja kwenye
mahubiri kwa lengo la kuombewa tu,hata watu wanapoalikwa kuokoka anaweza kuwa miongoni mwao lakini nia yake ni
maombezi tu ,watu hawa hawako mbali na ufalme wa Mungu (Marko 12;34,Zaburi 119;67,71) Wakati mwingine Mungu huruhusu mateso
yawapate ili watu wapate kumjua yeye na wengine ni vigumu kuokoka mpaka wabanwe
kwenye kona kidogo (Yohana 4;52-53,11;45).Watu
wengine humwamini mungu baada ya kufanyiwa muujiza (Yohana 12;9-11) aidha Mungu huwaponya wengine ili wamwamini(Luka 8;1-4)Mfano Mariam Magdalene
aliyekuwa kahaba na kutolewa pepo aliponywa na akawa anamtumikia Mungu.Kwa
msingi huu tunapofanya utafiti mwanzoni na kugundua kuwa mtu huyu alifuata
maombezi akaponywa tunamfuatilia kwa kumjenga jinsi ya kuutunza muujiza wake
ambako kwa usalama ni kuokoka,Pili kama alifuatilia maombezi na hakuponywa tunapaswa kumfundisha jinsi ya kung’ang’ania
na kuupata muujiza wake ambapo ni kuendelea kuja ibadani,aidha kwa kuwa watenda
kazi pia huenda kwa niaba ya Yesu Kristo unaweza kuomba nao kuwaombea kuwawekea
mikono na hatimaye Bwana atawaponya na wataokolewa Hivyo tusiwapuuzie watu
wanaofuata maombezi(Luka 10;1,17)
wakati mwingine majaribu hutupata ili tuwasaidie wale watakaojaribiwa (Waebrania 2;18).
Hekima ya kuwalea watoto
wachanga wa kiroho.
Biblia inasema wenye hekima huvuta roho
za watu (Mithali 11;30) Watoto
wachanga kiroho ni wale waliookoka hivi
karibuni,Hata hivyo Mtu anaweza kuwa kuwa ameokoka siku nyingi lakini akawa ni
mchanga bado (Waebrania 5;11-14)Hwa
wa muda mrefu ni wale waliodumaa kiroho wanahitaji tiba lakini wale wachanga
kabisa wanahitaji maziwa (1Petro 2;2)
kwa msingi huo yako maarifa ya muhimu ya
ufuatiliaji na hekima katika ufuatiliaji,mambo kadhaa yafuatayo ni muhimu
kuyazingatia.
Ø
Hatupaswi
kuwaharakisha (Mwanzo 33; 12-14).Si
vizuri kuwafundisha masomo magumu kama malipizi ya ndoa ,utatu wa Mungu,n.k
wakati wa uchanga wao kama amepokea muujiza mfundishe namna ya kuutunza muujiza
wake.
Ø
Tusiwahukumu
katika makosa wayafanyayo katika hatua za mwanzoni (Warumi 14;13) katika hatua
hii ya mwanzoni hata kama una shida na
unayemfuatilia ana uwezo jihadhari usimkope,Tumetumwa kufundisha tu (2Koritho 12;14-18,Isaya 65;13-14)
Ø
Tuwalinde
kwa kuwaombea kwani hawajui kuomba ili wakue kiroho (Maombolezo 2;1-4,18-19).
Mpangilio wa masomo ya mwanzo
ya wokovu.
Yako
masomo maalumu ya ufuatiliaji ambayo ni muhimu sana kwa watoto wa kiroho
kufundishwa wakati wa kuwafuatilia masomo mawili ni maalumu kwa watu waliofuata
maombezi na kuponywa au kuto kuponywa wakiwa hawajaokoka kama alikuja kwa
maombezi na hajapona tunamfundisha somo (Muujiza
mkubwa kwa watu wanaong’ang’ania) Kami ni mtu aliyepata muujiza wake lakini
hajaokoka tunamfundisha somo (Jinsi ya
kuutunza muujiza wako). Hali hizi zoote tunazigundua wakati tumefanya ule
utafiti wa mwanzo.katika utafiti ule wa mwanzo kama tumegundua kuwa
Tuliyemfuatilia ameokoka kabisa hawa sasa inatupasa kuanza kuwafundisha masomo
ya mwanzo ya wokovu ambayo yako kumi na tatu na tutayafundisha kwa kuzingatia
mpangilio ufuatao.
Namba
ya somo
|
Jina la somo husika
|
Aina
ya somo hilo
|
Siku
ya kulifundisha
|
Somo No 1
|
Furaha
baada ya kuokolewa
|
Somo
la utangulizi
|
Siku ya 1 ya ufuatiliaji
|
Somo No 2
|
Hakika
ya Wokovu
|
Somo
la kinga
|
Siku ya pili ya ufuatiliaji
|
Somo No 9
|
Mfahamu
adui shetani
|
Somo
la kinga
|
Siku
ya tatu
|
Somo No 8
|
Yeye
Ashindaye
|
Somo
la kinga
|
Siku
ya nne
|
Somo No 10
|
Kujaribiwa
kwa imani ya Mtu alliyeokoka
|
Somo
la kinga
|
Siku
ya tano na sita
|
Somo No 4
|
Tumaini
letu kuu
|
Mwongozo
|
Siku
ya saba
|
Somo No 7
|
Kuteswa kwa ajili ya Kristo
|
Kuimarisha
|
Siku
ya nane
|
Somo No 3
|
Furaha
katika wokovu
|
Maarifa
|
Siku
ya tisa
|
Somo No 5
|
Jinsi
ya kuukulia wokovu
|
Maarifa
|
Siku
ya kumi
|
Somo No 11
|
Jinsi
ya kuomba
|
Maarifa
|
Siku ya
kumi na moja
|
Somo No 12
|
Uwezekano
wa kukataliwa
|
Maarifa
|
Siku ya kumi na mbili
|
Somo No 6
|
Kugeuka
Nyuma na kuacha wokovu
|
Maarifa
|
Siku ya kumi na tatu
|
Somo No 13
|
Umuhimu
wa kuhudhuria Ibada zoote
|
Maarifa
|
Siku ya kumi na nne
|
Baada ya kuwa tumewafundisha masomo hayo pia tunaweza
kuwaimarisha kupitia masomo mengineyo mbalimbali tunayojifunza katika kanisa
letu kama misingi ya imani n.k
Jinsi na namna ya kuwafundisha.
Ni muhimu kukumbuka kuwa kuwafundisha ndio
kunyonyesha kwenyewe kwa hiyo kila tunapowatembelea tufundishe na tuache kupiga
story nyingine tusitoke katika lengo (Maombolezo
4;3-4),Sisi wenyewe ni muhimu kujifunza kujaa neno na ufahamu wakati
waufuatiliaji tutakutana na maswali mengi ni muhimu kujiandaa basi kabala ya
kwenda kufundihs hili litatuimarisha nasisi wenyewe” When you teaches you learn
twice” tumuombe Mungu atupake kabali aya kwenda kufundisha ili Mungu awabadilishe kwani maneno yetu tu
hayawezi kuleta mabadiliko (2Timoth
4;13,Matendo 6;4) Tukiwa na wanafunzi wengi wa ufuatiliaji tunaweza kuwa na
madarasa ya tirano (Matendo 19;8-10) Tuwahoji maswali ili kuelewa ufahamu
wao,tuwakumbushe kuhudhuria ibada,kuwahi ibada,kusikiliza kaseti za neno la
Mungu,Na kuwa mtu akisha okolewa mikutano ya injili kwake si ya muhimu kama
kujifunza neno katika mafundisho (Mathayo
28;19-20) Mtu aliyeokoka haitaji kuhubiriwa bali kujifunza neno.
Somo maalum shule
ya watenda kazi.
SOMO: KUSHUHUDIA KWA MANENO
MACHACHE
Mithali 11;30 Mwenye hekima huvuta roho za
watu, tunaweza tukawa ni watu tunaopenda sana kushuhudia lakini tukawa hatupati
matokeo yanayokusudiwa endapo hatutakuwa na hekima.Nyakati za kanisa la
kwanza waliposhuhudia walipata matokeo
mazuri zaidi na kuweza hata kuupindua ulimwengu (Matendo 17;5-6) Na nyakati zao ilikuwa ngumu sana kuifanya kazi ya
kuhubiri injili,ilikuwa usipo mkiri kaisari kuwa ni Bwana unauawa kwa kutupwa
kwenye matundu ya simba katika viwanja vya michezo ya Olympic sasa tutajifunza
somo hili kushuhudia kwa maneno machache kwa kuzingatia vipengele vinne
vifuatavyo;-
- Madhara ya kutokuwa washuhudiaji.
- Kushuhudia kwa maneno machache.
- Umuhimu wa kukwepa kutumia maandiko mengi wakati wa kushuhudia.
- Misingi minne ya kushuhudia kwa maneno machache.
Madahara ya kutokuwa
washuhudiaji.
(2Falme
6;24-33,7;1-9,Tito 1;15-16) Nyakati za Biblia wakoma wanne najisi waliamua
kupeleka habari njema kwa watu wa mji. Hawakuweza kuwasahau wengine pale Mungu
alipowafanyia wao muujiza kwa sababu ya njaa iliyokuwepo. Ikiwa watu hawa
najisi waliona si shani kufurahia wokovu wa Bwana peke yao kwani walijua kuna
madhara yatawapata sisi nasi tulikuwa najisi kabla ya kuokolewa na kwakuwa
Mungu ametuokoa hatuna budi kuwashirikisha habari njema hizi na wengine ili
waokolewe vinginevyo nasi madhara yatatupata tuwaalike wengine waje kula neno
la Mungu (Ezekiel 3;7-9).
Kushuhudia kwa maneno machache.
Kushuhudia kwetu mara nyingi kunapaswa
kuzingatia uhusiano wa mwanamke na mwanaume katika wokovu, kama ilivyokuwa kwa
Paulo (Matendo 12;3-4), kushuhudia
mtu wa jinsia tofauti wakati mwingine kunaleta matokeo bandia.Kushuhudia kwetu lazima kuzingatie kutumia maneno
machache, Paulo mtume alikuwa mtu hatari sana
katika ushuhudiaji wa maneno machache ilikuwa ukimpa nafasi tu anakugeuza kuwa mkristo (Matendo 26;27-28).Tusitumie maneno mengi wakati wa kushuhudia maneno yetu hayaokoi anayeokoa ni Roho wa
Mungu yeye atawashuhudia kwa habari ya haki, dhambi na hukumu.(Yohana 15;26-27,16;8,1Koritho 2;10),Tufahamu
kuwa watu tunaowashuhudia wana shughuli zao hivyo maneno mengi yanaweza
kuonekana kama unawapotezea wakati,Hivyo niu muhimu kutumia maneno machache
sana wakati huo.
Umuhimu
wa kukwepa kutumia maandiko mengi wakati wa kushuhudia.
Mtenda kazi anapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha kutofautisha kati ya
kuhubiri na kufundisha (Mathayo 28;19)
Tunaposhuhudia tunahubiri tu kwa lengo la kumleta mtu kwa Yesu au kutubu dhambi
zake na kuokolewa hapa tunahubiri watu kumuamini Yesu baada ya kuwa watu
wameamini ndipo mafundisho hufuata kwa
msingi huo basi wakati wa kushuhudia hatuna budi kukwepa kutumia ufundi mwingi
wa maandiko Yesu alikuwa akihubiri kwa kuyataja tu maandiko ingawa ulikuweko
wakati alipopaswa kufunua na kutafuta maandiko (Mathayo 5;21-27,38,Luka 4;16-17)
Misingi minne ya kushuhudia kwa
maneno machache.
Yako mambo machache ambayo ni ya msingi
kuyalenga wakati wa kushuhudia haya ndio kiini cha injili yetu wakati wa
kushuhudia misingi hii ya ushuhudiaji iko minne;-
Ø
Wote
tumefanya dhambi (Warumi 3 10-12,23, 5;12)
Ø
Hatuwezi
kuzishinda dhambi kwa nguvu zetu (Yohana
15;5)
Ø
Uwezo
wa kushinda dhambi unapatikana kwa Yesu tu (Waebrania 4;15)
Ø
Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa Bali yeye aziungamaye
na kuziacha atapata Rehema (Mithali 28;13;Luka
1;77,1Yohana 1;9-10)
Baada ya kuzingatia misingi hii minne
katika ushuhudiaji muongoze sala ya toba. Aidha ni Muhimu wakati wa ushuhudiaji
kutumia nneno TU badala ya U mfano woote TU mefanya dhambi badala ya Umefanya
hii inapunguza ukali wa maneno na kupunguza hali ya kujihesabia haki mitume
waliitumia wakijijumuisha na wao Mfano ktk Yakobo
3;2 1Yohana 1;8-9 twajikwaa,twatia n.k haya ni ya muhimu kwa ushuhudiaji
Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda.
Somo maalum shule
ya watendakazi.
Somo: MSAADA KWA MTU
ANAYESHUHUDIA
Msaada kwa mtu anayeshuhudia ni somo
maalumu lenye kutoa mwanga wa majibu husika kwa maswali au vikwazo
wanavyokutana navyo watu wanao kwenda kushuhudia Hapa tunatoa baadhi ya mistari
inayo faa kuwajibu wale wanaojificha katika kona za mambo kadhaa ili kukwepa
kumpokea Yesu ingawa kumpokea Kristo ni hiyari lakini mshuhudiaji anapokuwa na
uhodari wakujibu hoja hizo kwa kutumia maandiko inamweka mahali salama na
kumfanya kuwa na majibu ya kibiblia kwa kila kikwazo anachokutana nacho maswala
hayo ni kama ifuatavyo;-
- Nimekusikia vizuri lakini uamuzi wangu wa kuokoka nitautoa siku nyingine
JIBU; Walakini hamjui
yatakayokuwako kesho uzima wenu ni nini?…Mithali
27;1,Yakobo 4;14,2Koritho 6;2,Muhubiri 9;12.
- Nitaokoka ngoja nitengeneze pesa na nizidi kuhifahamu dunia
JIBU; Kujitayarisha kwa Mungu ni
jambo muhimu Luka 12; 15-21, Marko 8; 36
- Nitaokoka nikiwa mzee basi
JIBU; Mkumbuke muumba wako siku za
ujana wako Muhubiri 12; 1, 10; 14,
Mathayo 24; 42-44.
- Siwezi kuiacha dini ya Baba yangu.
JIBU; Baba hatabeba mzigo wa mwana
wala mwana hatabeba mzigo wa baba yake Eekieli
20;18, Marko 7;8-9 usiliache neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo
- Kwani kunywa Pombe ni dhambi?
JIBU;Mithali23;20
- Kwani kuvuta sigara,bangi,madawa ya kulevya,mirungi na ugolo vimeandikwa wapi katika Biblia?
JIBU; Isaya 55;2
- Mimi ni mtoto wa kikristo na nilibatizwa tangu utoto
JIBU; Tito 1;16,Luka
6;46,Warumi 10;13-14
- Mungu ni mmoja tu ni njia tu ndo zinatofautiana lakini woote tunaelekea huko
JIBU; Yakobo 2;19 1Timotheo 2;5 Yohana 15;23,1Yohana 2;23 Yohana 14;6, 10;7,9
- Haiwezekani kuokoka au kuwa mtakatifu ukiwa hapa duniani
JIBU; Yesu alikuja duniani ili
kuokoa,kama wokovu ni mbinguni hapa alikuja kufuata nini,Watakatifu walioko
duniani ndio waliobora …Luka
19;9-10,Yohana 5;34,Zaburi 16;3,Tito 2;11-12,Wafilipi 4;13,Tito 3;4-4
- Mimi naenda kanisani kila siku sikosi,naimba hata kwaya nimzee wa kanisa pia natoa sadaka sana
JIBU; Marko 7; 6, Amosi 5;21-22,Ezekiel 33;31-32
- Nikiokoka naona nitakuwa maskini
JIBU; Mathayo 27;57,.3Yohana 1;2 Hagai 2;8
- Muziki wa dansi umekatazwa wapi katika Biblia?
JIBU: Isaya 5;12-14
- Niliwahi kuokoka kisha nikaacha itakuwaje?
JIBU; 2Petro
2;20-22,Ufunuo 2;4-5 Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu....
- Bado nafikiria
JIBU Mithali 29;1.
- Mi mpaka nimuelezee mume wangu anielewe anikubalie
JIBU; Wagalatia 6;5 Luka 20;34-36 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe!
- Naogopa kuwa mnafiki wengi walijifanya wameokoka na tunawaona wakifanya dhambi
JIBU, Warumi 14;12 Zaburi 37;37 Kila mtu atatoa habari zake mwenyewe
mbele za Mungu
- Endelea kuniombea siku nikiamua ndo iatakuwa moja kwa moja bila unafiki
JIBU Warumi 9;16 Zekaria 4;6
- Maisha ya siku hizi unayajua sasa nitaisije na mshahara wa halali tu ikiwa nitaokoka
JIBU Mathayo 6;25-33,1Petro 5;6-7
- Mi sipendi kutanga tanga
JIBU
Mathayo 13; 45, Matendo 26;4-5,9-18 Mitume
waliacha madhehebu yao
- Mimi nauza pombe na nnaishi kwa hiyo na ninasomesha watoto sasa nikiokoka nitaishije?
JIBU Marko 9;43-48. mkono wako ukikukosesha ukate
- Mi baba yangu ni mchungaji na ni muhubiri mkubwa
JIBU: Ezekiel 14;14,16,20.
- Ninyi ndio wale manabii wa uongo waliosemwa watatokea
JIBU; “Manabii wa kweli wa Mungu ,husema yaliyo ya
Mungu yaani sawa na neno la Mungu 2Nyakati 18;13,Yohana 3;34,Hesabu
22;18,Ezekieli 2;7 Nabii wa uongo huwaambia watu amani tu wakati ni maangamizi
na hupoteza watu Ezekieli 13;9-10,
Hakuna amani kwa wabaya Isaya 48;22
- Kuokoka ni kwa watu maskini na mimi sina shida au nna shida gani?
JIBU;
Mathayo 27; 57, Matendo 17;12. Wanawake
wengi kwa wanaume wenye vyeo waliamini
- Kanisa let undo la kwanza na lina watu wengi sana duniani kote;
JIBU; Yohana 14;6 10;7,9,Mathayo 7;13-14,Luka 13;24-25.
- Hali ya uchumi ni ngumu inawezekanaje kuokoka katika hali hii
JIBU; Mathayo 19;25-26.
Kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu yote yawezekana
Somo maalum shule
ya watenda kazi.
Somo: WAJIBU WA KUTOA RIPOTI.
Mtu
awaye yoote ambaye ni mtenda kazi katika shamba la Mungu anawajibika kutoa
ripoti,Kwa msingi huu ni muhimu kwa kila mtenda kazi kuwa na ufahamu wa kutosha
kuhusiana na somo hili Wajibu wa kutoa
ripoti amablo tutajifunza kwa kuzingatia vipengele sita vifuatavyo;-
- Wajibu wa kila mtenda kazi kutoa ripoti.
- Mfano wa Yesu Kristo katika kutoa Ripoti
- Utoaji ripoti nyakati za kanisa la kwanza.
- Mfumo wa kutoa ripoti na utekelezaji wake
- Faida za kutoa ripoti.
Wajibu wa kila mtenda kazi kutoa ripoti.
Kila mtenda kazi ana wajibu wa kutoa
ripoti ;katika kazi ya Mungu ni muhimu kufahamu kuwa tumetumwa na hatujajituma
wenyewe,kwa kawaida mtu yeyeote aliyetumwa anaporudu huridi kwa aliyemtuma na
kutoa Ripoti.Kutoa ripoti kunaonyesha tabia ya uaminifu (Hesabu 13;1-3,17-20) watu hawa walitumwa na waliporudi walitoa
ripoti (Hesabu 13;25-27,Yoshua 2;1)
Wengine walitumwa wakati wa Yoshua pia walitoa ripoti (Yoshua 2;23-24,7;2-3,1471,) Yoshua alitoa ripoti kwa Musa,sisi nasi
kama watenda kazi tumetumwa(Isaya
6;8,Luka 9;2,Mathayo 28;19-20) Hao walitumwa (Yohana 17;18). Kama Yesu alivyotumwa na Babaye yeye naye ametutuma
sisi, ikiwa tu watumwa kwa Mungu inatupasa kujizoeza tabia ya kurudi na kutoa
ripoti (Luka 17;10).
Mfano
wa Yesu Kristo katika kutoa Ripoti
Yohana
8;42.Yesu alikuja duniani kama Mtumwa aliyetumwa na Baba (Warumi 8;3). Yesu alitumwa aje
kutukomboa (Galatia 4;4-5 1Yohana 4;9-10,14) Na alifanya kazi kama alivyotumwa
(Yohana 4;34) alipoikamilisha kazi
ile aliyotumwa alitoa ripoti (Yohana
17;1-4;6-8,12-14) Ikiwa Mungu Yesu Kristo alitoa ripoti sisi ni nani basi
tusitoe ripoti ni muhimu kujifunza kutoa ripoti ya kile tunachikifanya mara
baada ya kazi
Utoaji ripoti nyakati za kanisa
la kwanza.
(Mwanzo
8; 6-12). Mtu asiyetoa ripoti anafananishwa na kunguru aliyetumwa wakati wa
Nuhu na asirudi, Yeye aliyetoa ripoti anafananishwa na njiwa aliyerudi kutoa
ripoti.
Ø
Kutokutoa
ripoti ni udhalimu (Luka 16;10-12)
wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu (1Koritho
6;9a)
Ø
Kutokutoa
ripoti ni kumdarau aliyekutuma (Isaya
2;30) Tunaheshimika mbele za Mungu kwa kumtumikia (Hesabu 14;23,Isaya 1;4)
Ø
Mtu
asiyetoa ripoti ni kama amerudi nyuma
amefarakana na Mungu.
Ø
Kutokutoa
ripoti ni dalili ya kiburi na kujiona kuwa tu zaidi ya Bwana Yesu na mitume (Mithali 11;2) inatupasa kuwa
wanyenyekevu kutoa ripoti ni ishara ya utii na unyenyekevu (Mithali n16;18.29,23.Yeremia
30;29,31-32,Malaki 3;18,4;1)
Mfumo wa kutoa ripoti na utekelezaji wake
Kila mtenda kazi anapaswa kujitolea ripoti ya
kile anachokifanya kila siku kuhusu kazi ya Mungu na kutoa ripoti ya wiki au
mwezi au mwaka kulingana na mapatano ya kanisa husika maeneo ya muhimu
yanayopaswa kzingatiwa wakati wa utoaji ripoti ni pamoja na
Ø
Ushuhudiaji,Umeshuhudia
wapi,kina nani na matokeo yake
Ø
Ufuatiliaji,Umefuatilia
wapi,kina nani,wamehudhuria ibada au la na matokeo
Ø
Kusoma
neno,Umesoma wapi,umeelewaje kitabu gani sura gani mistari ipi
Ø
Kusikiliza
neno, Umehudhuria ibada?,Umejifunza nini,semina,mkutano n.k
Ø
Maombi
umeombea nini muda uliotumika matokeo n.k
Kila
mtenda kazi atajitolea ripoti katika maeneo hayo makuu matano Mungu atuwezeshe.
Faida za kutoa ripoti.
Ziko faida nyingi sana zinazoambatana na
wajibu wa kutoa ripoti baadhi ni kama zifuatazo;-
Ø
Zinatupa
changamoto ya kuishi maisha ya kukesha na kuomba (Mathayo 24;42-44)
Ø
Hufanya
mchungaji wako ajue vipawa ulivyo navyo karama
na ni namna ya kukusaidia ili kukupa msaada zaidi au kwa ajili ya
Utumishi wa juu (2Tomoth 1;6)
Ø
Inatusaidia
kujitiisha kwa kiongozi wa kanisa Yesu Kristo na kutufanya tuwajibike tuonywe
na kukemewa (Ebrania 12;5-13)
Ø Inamsaidia
mchungaji katika kulichunga kanisa.
Ø
Inatuzoeza
kuwa wanyenyekevu na watii
Bwana
na ampe neema kila mmoja wetu kuyazingatia haya tuliyojifunza na kuyafanyia
kazi na kuzidi katika jina la Yesu.
Somo maalum shule
ya watenda kazi.
SOMO: NGUVU KWA AJILI YA
UTUMISHI
Ni muhimu kufahamu kuwa pamoja na
mafundisho mazuritunayoyapata katika shule hii ya watenda kazi mafanikio yetu
katika mambo yoote tuliyojifunza hayawezi kufanikiwa endapo tutamweka Pembeni
Roho mtakatifu,Roho mtakatifu hutoa nguvu itakayotufanya kuwa mashahidi wazuri
na ndio maana pamoja na mafundisho mazuri aliyoyatoa Yesu Kristo kwa wanafunzi
wake kwa karibu zaidi miaka mitatu na nusu
Bado aliwasisitiza wanafunzi wake wasitoke mpaka wamevikwa uwezo utokao
juu, (Luka 24;49,Matendo 1;8) .Tutajifunza
somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-
- Umuhimu wa Nguvu za Roho Mtakatifu.
- Jinsi ya Kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.
Umuhimu wa Nguvu za Roho
Mtakatifu.
Roho mtakatifu ni wa muhimu sana
katika maisha na utumishi wa mkristo yeyote, Lakini ni wa muhimu zaidi sana kwa
watu wanaotaka kumtumikia,Kwa ufupi yeye hutoa nguvu kwa ajili ya
utumishi.Nyakati za kanisa la kwanza swala la mtu kujazwa Roho mtakatifu lilikuwa ni swali muhimu kwa
wakristo kama ilivyo wokovu au kuongoza mtu nsala ya toba (Mdo 8;14-17,19;1-7) kwa nini ni wa muhimu hivi ;-
Ø
Ni
suluhisho la maongozi (Mwanzo
41;38-40,Daniel5;5-12,Hesabu 11;10-17)
Ø
Ni
suluhisho la uonevu dhidi ya maadui (Waamuzi
14;5-6,15;3,14-16)
Ø
Ni
suluhisho la upinzani wa kidini (Matendo
6;8-10,7;55).
Ø
Ni
suluhisho dhidi ya Nguvu za giza (Kutoka
7;10-13,Daniel 5;7,Hesabu 23;7-8,22-23,Matendo 8;4-21,13;6-12)
Ø
Tatizo
la uonevu dhidi ya Ibilisi (Luka 4;18-19,Mdo
10;38)
Ø
Ni
suluhisho la kutupa hekima (1Falme
3;16-27,Mdo 15)
Kwa
msingi huo basi iwapo Mungu anatutuma kati ya watu wanaoonewa na wenye shida za
aina mbalimbali Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana ukilinganisha na uhitaji
ulioko wa matatizo ya watu tunaokwenda kuwahudumia ,Kila mtenda kazi ni lazima
ahakikishe amejazwa na Nguvu za Roho mtakatifu na anadumu katika nguvu hizi na
ndipo tutakapoweza kufanya huduma hii kwa ufanisi Mkubwa.
Jinsi ya Kupokea nguvu za Roho
Mtakatifu.
Roho mtakatifu ni Mtakatifu kwa msingi huo
kuwa mbalu na dhambi ni jambo la muhimu ili yeye akae ndani yetu.(Yohana 3;3-6).
Roho
mtakatifu ni ahadi ya Mungu kwetu hivyo ni lazima tuipokee kwa imani (Matendo 2;38-39). Wakati wa maombezi ya roho mtakatifu tusiogope kupokea
roho nyingine Mungu si dhalimu kile tuombacho ndicho atupacho (Luka 11;9-18)..Wakati wa maombi kuhusu
ujazo wa Roho mtakatifu inashauriwa watu waombe kwa sauti kubwa hii itasaidia
wewe kupokea lugha ya kimbinguni na kusikika ukinena kwa Lugha mpya usiyoijua,
(Luka 3;21-22) Tunaweza pia kupokea
Roho mtakatifu na nguvu zake kwa kuwekewa Mikono (Matendo 8;17).
Maoni 1 :
Ubarikiwe sana Kwa masomo yako
Chapisha Maoni