Mstari wa msingi Mwanzo 19;16-17
“ Akakawiakawia nao wale watu wakamshika mkono na mkono wa mkewe na mkono wa
binti zake wawili , kwa jinsi Bwana
alivyomuhurumia , wakamtoa nje ya mji
ikawa walipomtoa nje mmoja alisema jiponye nafsi yako usitazame nyuma wala
usisimame katika hilo bonde popote ujiponye nafsi mlimani usije ukapotea “
Nguzo ya Chumvi
Wewe na mimi siku ile bwana
alivyotuokoa Yesu alituhurumia na kututoa
na kutuweka nje ya mji unaposoma Mwanzo
19;12-19, utaipata picha hii vizuri
kuokolewa ni kama Yesu ametutoa nje ya mji wa Sodoma na Gomora yaani
sawa na dunia hii ya watu watendao maovu ambayo wakati wowote itaanguka katika
hukumu ya Mungu Isaya 24;19-20, wakati wowote Mungu atauhukumu ulimwengu huu na
kelele za ulevi na uasherati havitasikika tena
wakati walimwengu watakapohukumiwa motoni lakini Lutu alionywa kuwa ajiokoe mwenyewe
kwa kutokugeuka nyuma
Mtu awaye yote aliyeokoka
anaonywa kuto kurudi nyuma Luka 9;62
Yesu akamwambia mtu aliyetia mkono wake kulima kisha akaangalia nyuma
hafai kwa ufalme wa Mungu Biblia inatuonya kuwa tusigeuke nyuma baada ya kuwa
tumeokolewa mkewe Lutu yeye baada ya wokovu mkuu aligeuka nyuma kwa kuipenda dunia Mwanzo 19;26 na tunasoma
kuwa akawa nguzo ya chumvi awaye yote ambaye ameokolewa kisha akaangalia nyuma
na kukumbuka maisha ya anasa za dunia hii uasherati, uvutaji wa sigara na
madawa ya kulevya kukumbuka sinema na dansi huyo anawezea kuharibiwa na
ulimwengu huu na kupoteza wokovu mkuu kiasi hiki.
NINI MAANA YA KUGEUKA NYUMA
·
Nikumsaliti bwana Yesu – mtu yeyote aliyeokolewa
anapoamua kurudi nyuma hana tofauti na Yuda kwani anamsaliti Bwana Yesu Luka 22;47-48
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu ni kumkana Bwana
Yesu na kudai kuwa hatumjui kama alivyofanya Petro Mathayo 26;71-72
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu kunakufanya uwe
nguzo ya chumvi Mwanzo 19;26 nchi yenye
chumvi ni nchi iliyolaaniwa hakuna kitu
kinaweza kustawi katika inchi ya chumvi hata maji yake hayanyweki wala kiumbe chochote hakiwezi kuishi Yeremia
17;5-6, Kumbukumbu 29;23
·
Kurudi nyuma na kuacha wokovu ni kujionyesha
kuwa wewe ni mkosaji mbele za Mungu na
wote wakaao mbinguni Mwanzo 11;3-8 kuacha wokovu ni kuyajenga tena yale
uliyoyabomoa ni kujionyesha jinsi ulivyo
mkosaji mbele za Mungu soma Wagalatia 2;18 siku ile ulipookoka mbingu
ilishangilia kwaajili yako sasa unaporudi nyuma ni aibu kule mbinguni ni huzuni
na kilio kikubwa na masikitiko na ibilisi na ufalme wake unashangilia
kukupatawewe tena huu ni ukosaji mkubwa
mbele za Mungu na majeshi yake huko mbinguni.
·
Kugeuka na kuacha wokovu ni kumtukama Mungu
Hesabu 15;30
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu ni kumkanyaga
mwana wa Mungu na kumfanyia jeuri Roho wa neema Waebrania 10;26-29
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu ni kumsulubisha mwana wa Mungu mara ya pili na
kumfedhehi kwa dhahiri Waebrania 6;4-6
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu kunakufanya uwe
nchi inayoota magugu na miiba soma
Waebrania 6;7-8, Yohana 15;1 Kutoka 16;4, Hosea 10;12
·
Kugeuka nyuma na kuacha wokovu ni sawa na mbwa
aliyerudia matapishi yake mwenyewe na nguruwe aliyeoshwa kurudi na kugaagaa
matopeni 2Petro 2;20-22, Mithali 26;11
TATIZO LA KURUDI NYUMA HUANZIA
MOYONI
Mtu aliyeokoka anaporudi nyuma jambo
hili huanzia moyoni Matendo 7;39 ziko
dalili kadhaa zinazoweza kuonyesha kwamba mtu Fulani amegeuka nyuma na kuacha
wokovu
Hatataka kulitii neno la Mungu
tena, Hofu ya Mungu ndani yake inakuwa haiko, hafurahii mafundisho ya neno la
Mungu na hufikia hatua ya kulikataa neno la Mungu na kukosoa kila aina ya mahubiri
na hakuna cha kumgusa, atalizoea neno la Mungu na kuliona la kawaida, haoni
umuhimu wa kukaa katika mafundisho, hufikia hatua ya kulidharau neno la Bwana Hesabu
15;31, Mithali 13;13 mtu wa aina hii
anaitwa mtu aliyeshiba njia zake mwenyewe Mithali 14;14 ageukaye moyoni hushiba
njia zake mwenyewe.
SABABU ZINAZOSABABISHA WATU WENGI
KURUDI NYUMA
·
Kukosa viongozi wanaofundisha kweli ya neno la
Mungu Kutoka 32;1 Waamuzi 2 18-19
·
Kuupenda ulimwengu huu wa sasa 2Timotheo 4;10
Mithali 24;1,23,17 Warumi 12;2 2Wafalme 17;15
·
Kukaa katika ushirika uliojaa maasi Mathayo
24;12
·
Kukosa mizizi na hivyo kuogopa dhiki na mateso
Luka 8;13 Mathayo 13;20-21,Luka 12;4-5 inatupasa kufahamu kuwa imetupasa
kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi Matendo 14;19-22
kwa msingi huo basi inatupasa kuendelea
kushikamana na wokovu kama mwanzo wa
uthabiti wetu Waebrania 3;14.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni