VIPENGELE VYA UDEREVA VYA KUJIHAMI.
Ili kutekeleza kanuni ya kuzuia
ajali, Dereva yeyote anatakiwa kuelewa vizuri mambo ya msingi yafuatayo;-
1.
Kujua
2.
Kuwa macho
3.
Kuangalia mbele
4.
Kuamua
KUJUA
Dereva anapaswa kuelewa michoro na alama za barabarani.
i.
Alama za barabarani na michoro inawakilisha
lugha, ambayo kila mtumiaji wa barabara anatakiwa kuijua vizuri, kuiheshimu na
kuitafasiri kama inavyotakiwa.
ii.
Kwa bahati nzuri inawakilishwa na vbitambulisho
vya vikundi vikuu vitatu
a.
Rangi Nyekundu, Nyeusi, Njano, Nyeupe, bluu,
kijani.
b.
Umbile Mviringo, Pembe tatu, Pembe nne na pembe
tano.
c.
Alama – Maandishi, Picha na Michoro.
iii.
Alama na michoro ya barabarani ni lazima ziwe na
sifa zifuatazo.
a.
Zilenge kuongeza ufanisi wa mtandao wa barabara.
b.
Zitoe ujumbe ambao ni wazi unaoeleweka kirahisi
kwa kila mtumiaji wa Barabara.
c.
Zizingatie sheria za usalama barabarani za kitaifa na kimataifa
d.
Ziwe na muundo wa alama moja kitaifa unaolingana
na makubaliano ya umoja wa kimataifa kwa alama za msingi.
e.
Ziwekwe sehemu ambazo ni lazima kuwepo, ili
zitoe ujumbe sahii kwa watumia Barabara,
f.
Ziwekwe umbali unaotakiwa kutoka sehemu husika
g.
Zifanyiwe matengenezo ya marakwa mara.
Mambo ya msingi ya kujiuliza kwanza
a. Alama
ni kiashirio kinachomuongoza mtu kwenye mambo na kumfanya afanye mambo vizuri.
b. Alama
za barabara ni uongozi uliowekwa kisheria
kutoa muongozo wa kisheria ili
kumuwezesha dereva aweze kufanya kazi
zake kirahisi na kwa ufanisi ili kwamba atumiapo barabara aweze kwenda kwa uysalama zaidi bila kupata
au kusababisha ajali.
c. Alama
za barabarani ni kitu ambacho hakitarajiwi kutokuweko
d. Wataalamu
waliamua kukaa na kutunga alama za usalama barabarani alama hizo zimegawanyika katika makundi makuu
matano
·
Alama za Amri
·
Alama za Onyo
·
Alama za taarifa
·
Alama za maelekezo
·
Alama za michoro chini ya barabara , taa za
kuongoza watumiaji wa barabara.
Alama za Amri
Alama hizi
zimegawanyika katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
-
Amri za kukataza.
-
Amri za kulazimisha au kuruhusu.
-
Amriza kutoa kipaumbele
Amri za kukataza ;-
Alama hizi zina waonyesha
watumiaji wa barabara sehenu ya barabara iliyokatazwa au mwisho wa sehemu
iliyokatazwa kufanya jambo Fulani kama itakavyoonyeshwa kwenye alama yenyewe alama hizi ni halali
·
Katika mwelekeo wa kawaida wa wanaotumia
barabara
·
Kutoka sehemu iliyopo hadi njia panda iliyo karibu
na alama husika .
Alama za amri ya kukataza zina
umbo la mviringo, mpaka mwekundu na picha au mchoro wenye rangi nyeusi,
nyekundu au bluu katika madhari
Alama au amri ya kukataza
zinawekwa karibu sana na sehemu husika
Alama za kulazimisha au kuruhusu
Ø
Hizi ni alma zinazzotumika kwa watumia
barabara kuelekea mwelekeo au njia
Fulani kati ya nyingi zilizopo kwenye
njia panda , pia alama hizi zinatumika kuwaongoza wanaotembea kwa miguu
na wapanda baiskeli kwenye njia moja kati ya njia zilizopo kwenye eneo husika
Ø
Amriza kulazimisha zina umbo la mviringo mpaka
mdogo mweupe na picha ai mchoro mweupe katika madhari nyuma bluu alama hizi
zinawekwa karibu sana na njia panda
Ø
Alama za kipaumbele na kupisha njia panda ni
sehemu yenye migogoro mingi kati ya watumia barabara kuliko sehemu nyingine yoyote
ile barabarani. Ili kurekebisha migogoro hiyo kati ya watumia barabara. Sheria ya
Usalama barabarani inatumika (toa
kipaumbele kwa madereva wa magari
wanaokaribia njia panda kutoka kulia ) lakini sehemu yenye magari mengi ambapo madereva hawawezi kutathimini vizuri
hatari iliyopo basi sehemu hiyo njia panda
sheria ya usalama barabarani haitatumika
tena badala yake zitatumika alama za kipaumbele
Ø
Alama hizi zina maumbo mbali mbali kulingana na
ujumbe au amri inayokusudiwa katika alama husika.
Alama za tahadhari au Onyo
Ø
Alama hizi zinawaonya madereva na watumia
barabara wengine juu yaq hatari iliyopo au inayoweza kuwepo mbele yao
Ø
Alama hizi zinawqekwa upande wa kushoto wa
barabara kati ya mita mia hadi mia mbili (100-200m) toka sehemu yenye hatari
Ø
Sehemu zenye njia panda nyingi hasa mjini umbali
huo hupungua hadi mita hamisini (50m)
Ø
Sehemu ya barabara yenye alama hizi dereva
anatakiwa kupunguza kasi ya gari lake.
Ø
Alama za tahadhariu au onyo zina umbo la pembe
tatu lenye kitako pembe mbili chini, mpaka mwekundu na picha au mchoro wa
hatari iliyopo au inayoweza kutokea mbele katika mandhari ya nyuma nyeupe.
Alama za Taarifa
Ø
Alama za taarifa huwataarifu madereva na
watrumia barabra wengine juu ya barabara , sehemu muhimu na sehemu senye huduma
mbalimbali ambazo ni muhimu kwao , kati ya alama hiziz zipo pia zenye uhusiano na sheria ya usalama
barabarani ambazo zinatoa masharti Fulani ambayo mtumiaji wa barabara akiamua kutumia sharti
afuate sheria na si vinginevyo Kwa
Tanzania ni hiari ya dereva kutumia barabara hiyo ,lakini akiamua ni lazima
aendeshe gari lake uelekeo ulioonyeshwa kwenye alama hiyo.
Ø
Alama za maeneo ya huduma, hizi ni taa ni alama
zinazowafahamisha madereva na watumia barabara wengine juu ya huduma mbalimbali
wanazoeweza kupata katika maeneo husika
Ø
Alama hizi zina umbo la pembe mraba nne, ulingo
wa Bluu picha nyausi au nyekundu katika madhari nyeupe nyuma
Alama za maelekezo
Ø
Hizi ni alama za kuwafahamisha madereva wa
magari sehemu maalumu nba muhimu
Ø
Alama hizi zina umbo la pembe nne Mstatili au
mraba ulingo wa bluu picha nyeupe au nyeusi madharri ya bluu au kijani nyuma.
Ø
Alama hizi zinawekwa kabla ya njia panda au kwenye njia panda ili kuwasaidia madereva na watumiaji wengine
wa barabara kuchagua barabara zinazofaa kuwafikisha waendako na kuwaongoza
kwenye mtanadao wa barabara kupita na hata kuzunguka kwenye maeneo ya makazi ya watu
Alama za michoro ya chini ya barabara na taa za barabarani
Ø
Michoro ya barabarani ni ni mmichoro iliyochorwa
kwa lengo la kurekebisha msongamano wa
magari pamoja na kuwaonya au kuwaongoza watumiaji wa barabara
Ø
Michoro hiyo ya barabarani imegawanyika katika
makundi makuu yafuatayo;-
Mistari ya Onyo
Mistari ya kukataza
Mistari inayogawa njia katikati ya barabara ya magari
Mistari inayogawa barabara
Mistari inayogawa njia ya magari ya abiria katika barabara
Mistari ya kutokea pembeni mwa barabara ya magari
Mistari ya kipaumbele
Mistari ya kusimama
Mistari hii pia huchoirwa karibiu na njia
panda sehemu ya barabara hii dereva
hatakiwi kuvuka njia kwa sababu ya hatari iliyopo ikiwa atavuka basi avuke kwa
tahadhari kubwa
Taa za kuongoza watumia barabara
Ø
Taa hizi zinalenga kuondoa migogoro kati ya watumia
barabara kwenye njia panda au barabara
zenye matumizi makubwa
Ø
Taa nyekundu humaanisha usiingie njia panda
simama
Ø
Nyekundu na njano usiiingie nja panda simama
Ø
Njano usiingie kwenye njia poanda simama
Ø
Kijani ingia kwenye njia panda endapo ni salama.
LIJUE
GARI LAKO.
Mfumo wagea Gea za Gari za aina mbali mbalizenye kutumia mfumo wa Manyo ( Manual)
CLUTCH ; Kazi yake
ni kuondoa gari na kutenganisha Engine
na Gearbox.
BRAKE ; Kazi yake ni kupunguza mwendo na
kusimamisha gari
ACCELERATOR; Kazi yake ni kuongeza
mwendo kasi wa gari na muungurumo na inapoachiwa kidogo mwendo hupungua,
inaongeza kasi ya uhcomwaji wa mafuta.
Ni Muhimu
Kukumbuka kuwa Unapotaka kusimama unatakiwaq kukanyaga Clutch na Brake kwa
pamoja ili gari lisizime linaposimama.
Kazi ya gea namba moja Ni kuondoa
gari na kupanda mlima mkali na wakati wa
kuteremka mlima mkali
Kazi ya gea namba mbili Ni
kuifanya gari kuwa nyepesi zaidi na kuongeza mwendo
Kazi ya gea namba tatu na nne Ni
kufanya gari kuendelea kuwa jepesi zaidi na kuongeza mwendo
Namna ya kupanga gea kutoka gea nzito kwenda gea nyepesi;
Kutoka
0-10 MPH Gea . No 1
Kutoka 10-20 MPH.
Gea . No 2
Kutoka 20-30 MPH.
Gea. No 3
Kutoka
30-40 MPH. Gea. No 4
Kutoka 40-50
MPH Gea. No 5
Kutoka
50-120 MPH. Mwendo utaendelea kuzaliswa na gia No 1 &
2
Jinsi ya kupangua gea kubwa kwenda gia
ndogo
Kama gari
lilikuwa linatembea kiasi cha mwendo
upatao 60MPh itakubidi upunguze mwendo hadi 50MPH au 40MPh ndipo uingize gia
nambari nne
Endapo
inatembea mwendo kiasi 40 MPH itakubidi upunguze mwendo hadi kufikia 30MPH
ndipo uingize gia nambari tatu
Kama gari
ilikuwa inatembea kiasi cha mwendo upatao 30MPH itakubidi upunguze mwendo hadi
kufikia 20MPH ndipo uingize gea nambari mbili
Dash board ni
chombo ambacho kinamjulisha na kumwezesha dereva kugundua hitilafu zinazoweza
kujitokeza anapoendesha gari barabarani kwa mfano
·
Kusoma speedmeter – hiki ni chombo ambacho hupima kasi au mwendo wa gari
·
Mail gauge – hiki ni chomboambacho hupima au
kuhesabu au kurekodi ni mwendo au umbali gani gari limetembea
·
Fuel gauge – ni kipimo cha kuonyesha ni kiasi
gani cha mafuta aidha Petrol au diesel iliyoko kwenye tank la gari
·
Oil gauge – ni kipimo chenye kufanya kazi ya
kuonyesha ni kiasi gani cha oil
kimebakia kwenye injini
·
Water temperature gauge ni kipimo ambacho kinaonyesha joto la injini
limepanda kiasi gani na pia kuonyesha
maji yamepata moto kiasi ghani kwenye radiator
·
Alternator gauge au alternator charge hiki ni
chombo cha kuonyesha kuwa kifua umeme katika gari hakifanyi kazi kwa msingi huo
maana yake ni kuwa haichaji na hivyo maana yake ni kuwa umeme haufuliwi
·
Right indicator – ni taa maalumu yenye mlio
Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda upande wa kulia
·
Left indicator – ni taa maalumu yenye mlio
Fulani kuashiria kuwa unakusudia kukata kwenda kushoto
Dash Board kama inavyoonekana katika mchoro
chini.
Katika Dash Board kunakuwa na maswala kadhaa yanayoweza kusoma mambo kadhaa yafuatayo
0 2 6 8 6 4
2
|
Water temp
|
Brake Light
|
Alternator
|
Fuel gauge
|
Right
|
Left indicator
|
Fuel
|
UTUNZAJI WA GARI
Katika utunzaji wa gari kwa
ujumla tunazungumzia ukaguzi wa gari.Ukitaka gari lako liwe katika hali nzuri
kila ulitumiapo/kuwa na uhakika wa usalama wako na wa gari lako liwapo
barabarani, ni muhimu sana kulikagua hari kila siku asubuhi kabala ya
kuliendesha na pia kuwa na utaratibu wa kulifanyia service kila linapotembea
kilomita kadhaa.
Ukaguzi wa gari
1. Kitu
cha kwanza kabisa ni kulikagua gari lako kwa nje, utafanya ukagfuzi wa matairi
kwa kuangalia
·
Upepo na nati kama zimelegea au la
·
Kashata za Matairi kama hazijaisha yaani ziko
kipara
Kisha utafungua
Bonet na hapa utaangalia
·
Maji kwenye rejeta (radiator) kama yapo
·
Oil kwenye injini kwa kutumia deep stick
-
Hakikisha unapopima oil gari liko katika
tambarare ili uweze kupata level halali ya oil
-
Oil inayotumika kwenye injini kwa kawaida ni
nambari 40
-
Deef oil nambari 140
-
Gear box ni oil nambari 90
·
Mafuta ya Brake (Brake fluid) na clutch
·
Maji ya betrii, yaani unafungua betrii na
kuangalia kama
-
Maji yamepungua unaongeza maji baridi Distrilled
water
-
Kama ni jipya umemwaga maji yote na kuweka Acid
maarufu kama maji makali HCI
-
Maji yakiisha ndani ya betrii , batrii itakufa
baada ya hapo
-
Unafunga tena bonet.
2. Sasa
unaingia ndani ya gari na unaaangalia
·
Kaa kwenye kiti chako na hakikisha kimekaa sawasawa
·
Kagua pedle zote
kama zinafanya kazi sawasawa yaani hapa tunazungumzia
-
Brake kama iko sawa na inafanya kazi
-
Clutch kama iko sawa na inafanya kazi
-
Acceletator kama iko sawa na inafanya kazi.
·
Kagua dashboard kama taa zote za vitu vyote
zinafanya kazi vema yaani
-
Water temperature gauge
-
Alitanatory charge
-
Oil gauge
-
Fuel gauge
-
Mail gauge .n.k.
·
Waipa kama zinafanya kazi vema
·
Hand brake kama inafanya kazi vema
·
Usukani kama umekaa vema
·
Mkanda
·
Taa zite kama zinafanya kazi Hususani indicator
·
Wema side mirror vema kukuwezesha kuona chochote kwa nyuma au
pembeni
·
Kioo cha kuangalia magari nyuma pia kiwekwe
kukuwezesha kuona
Ukimaliza yote
hayo sasa uko huru au salama kuendesha gari lako.
KUONDOA AU KUENDESHA GARI.
Unapokuwa umekagua gari lako na
kulikuta liko katika hali nzuri sasa unataka kuliendesha na kuanza safari na
gari lako, unapoingia kwenye gari na kuikuta iko katika gea namba moja basi
sasa unapaswa kufanya maswala yafuatayo.
i.
Weka switch/ yaani ufunguo wa gari katika sehemu
yake
ii.
Kanyaga clutch mpaka mwisho
iii.
Ondoa gea namba moja na kuliweka gari huru yaani
free
iv.
Ondoa mguu kwenye clutch
v.
Anza kuwasha ufunguo wa gari Satrt/Switch gari
vi.
Sikiliza muungurumo kidogo
vii.
Kanyaga clutch mpaka mwisho/pamoja na brake
kulisaidia gari lisiweze kurudi nyuma
viii.
Ondoa gari kutoka kwenye free mpaka kwenye
nambari moja gea hii mara nyingi
hujulikana kama gea ya kuondokea
ix.
Legeza mguu wa kwenye clutch mpaka unasikia gari
kama inaondoka hivi mlio unakuwa umebadilika na unakuwa constant
x.
Kumbuka kutoa handbrake
xi.
Ongeza mafuta kidogo na na kulegeza clutch na
gari litaanza kuondoka na linapoondoka
achia clutch, lakini usiachie ghafla, taratibu baada ya kuona baada ya
kuona gari liko kwenye mwendo wa kawaida
xii.
Lipe gari nguvu kwa kuongeza mafuta na badilisha
gea nambari moja kwenda nambari mbili,
unapobadilisha gea hakikisha kuwa unaachioa accelerator na kukanyaga
clutch na baada ya gea kuingia unaachoia
clutch na unakanyaga acceleretaor
xiii.
Utaendelea na safari kwa kubadilisha gea nambari
mbili mpaka tatu na kuendelea
Kumbuka gea nambari moja sio ya kutembelea hivyo
usiiache kwa muda mrefu bila ya kuibadilisha
Unapoendesha gari hakikisha kuwa una vyeti vyako ili
isiwe kero kwa traffic vyeti hivyo ni
a.
Leseni ya kuendeshea driving Licence – hakikisha
haijaisha na pia iwe ni daraja linalohusika
b.
Kadi ya njia (T.L.B)
c.
Kadi ya gari ambayo kwa kawaida huwa na
o
Jina la gari
o
Namba ya gari
o
Jina lako
o
Gari lilitengenezwa wapi
o
Limesajiliwa lini hapa nchini
o
Engine namber
o
Chases Nuimber n.k.
Vitu muhimu kuwa navyo unapoendesha gari ni
pamoja na
·
Spare tyre-tairi la akiba
·
Jeki
·
Na spana ya kuondoa tairi Wheel spanner
Safari ya mbali
·
Kisanduku cha huduma ya kwanza chenya panadol,
aspirin, spirit, iodine, bendeji, pamba, plaster, wembe mkasi, pini n,k.
·
Spana za dharula
·
Plaizi na Plier
·
Adjustable screw driver, plug spanner na sanduku
nzima ya spanner
·
Kamba
·
Fan belt
·
Petrol au diesel na kitu kingine chochote
utakachokiona muhimu katika gari lako kwa safari
Kuvumbua kasoro
1.
Kifaa au chombo kitakachokujulisha kuwa gari
lako lina kasoro ni Dash board.
2.
Pia kwenye mwili wako viungo vitakavyokufanya
uvumbue kasoro ni
o
Macho yako kwa kuona
o
Sikio lako kwa kusikia
o
Pua yako kwa kunusa
Unapogundua
chochote cha tofauti kwa kutumia vitu hivyo juu simamisha gari lako kagua na
kugundua hitilafu.
Kuna aina tano “5” za Taa;-
·
Full
Light Taa kubwa – Taa hizi zina mwanga mkali na hutumika wakati wa
usiku ili kuona masafa marefu, endapo
mbele hakuna kitu chochote chenye mwanga mfano gari linguine ua pikipiki au
baiskeli n.k
·
Deem Light
taa ndogo – Taa hizi hutumika kama mbele
yako kuna gari lililo kutangulia , pia kama mbele yako kuna gari lingine
linakuja unapaswa kutumia deem light au kama mbele yako kuna kitu chenye
mwanga mfano pikipiki au baiskeli au
hata gari linguine
Hakikisha kuwa mwendo wa gari hauzidi mwendo wa mwanga
wa gari kwa msingi huo nenda mwendo sawa na wa taa zako
·
Indicator
ziko mbili kwa kawaida
Indicator ya kulia ni kwaajili ya kuonyesha kuwa gari
linapinda kulia au kwaajili ya kuomba nafasi ya Njia wakati unapotaka kulipita
gari linguine Overtake au kumzuia dereva wa nyuma asi Overtake
Indicator ya kushoto ni kwaajili ya kuonyesha kuwa
gari linapinda kushoto, kuruhusu gari la nyuma liweze kupita Overtake na
kuonyesha kuwa gari linataka kusimama au kupaki kushoto
·
Parking
light – Hutumika wakati gari linapokuwa limepaki hususani wakati wa usiku,
au wakati wa ukungu ukungu mvua ua vumbi, pia mara giza linapoingia unashauriwa
kuwasha Parking light ni hatari kama
unapark gari usiku bila kuwasha parking light kwani dereva wa gari nyingine
anaweza asikuone na akakugonga
·
Brake
Light – Hutumika kumjulisha dereva
wa gari la nyuma kwamba
unapunguza mwendo au unasimama
UBADILISHAJI WA TAIRI
Utangulizi
Katika utaratibu wa kawaida
ubadilishaji wa tairi unaweza kufanyika katika njia kama mbili zifuatazo;-
·
Kuisha kwa tairi – yaani baada ya tairi kulika
limeisha linahitaji kubadilishwa
·
Pancha – wakati tairi linapopata pancha
(Punctuare)
Kulika au kwisha kwa tairi
Kwisha au kulika kwa tairi ni
jambo la kawaida kutokana na
msuguano wa tairi na ardhi, hivyo ni
vyema tairi linapokuwa limekwisha au liko kipara zibadilishwe na kuvalishwa ganda ama mpira mwingine mpya ili kwamba ;-
a. Kuepuka
usumbufu wa askari wa barabarani
b. Kulinda
maisha yako nay a watu wengine
c. Kuweka
usalama wa gari
d. Kuwa
na uhakika uwapo safarini na wakati wote unaposhughulika na gari
e. Kupita
sehemu yoyote bila ya kuwa na wasiwasi
Kwa msingi huo
basi ni muhimu kwa tairi za gari kuwa nzima wakati wote ili kupunguza matatizo
yaliyotajwa hapo juu.
Pancha (puncture)
Pancha hutokea wakati wowote na
kwa tairi yoyote hususani zile zilizolika kashata zake. Unapokuwa na pancha ni
vyema kuzingatia yafuatayo, iwapo utakuwa umekumbwa na pancha ni vyema
kuzingatia yafuatayo iwapo pancha imekupata kwenywe njia inayopitisha magari
wakato wote zingatia maswala muhimu yafuatayo;-
·
Egesha gari pembeni mwa barabara
·
Weka kibao au alama ya onyo kama unacho mbele na
nyuma ya gari kiasi cha mita 100 ili kuashiria tahadhari ya matengenezo au
uharibifuau marekebisho/Matatizo ya gari
·
Weka vigingi au mawe kwenye tairi la mbele na nyuma isipokuwa tairi lililopatwa na
pancha
·
Chukua wheel sperner na legeza nut za tairi
iliyopata pancha
·
Chukua jeki tafuta sehemu itakayostahimili uzito
wa gari kama vile kwenye chassis Frame nyuma ya aksel au kwenye kiti cha spring
piga jeki juu ili tairi iachane na ardhi
·
Chukua tena wheel spanner na malizia kufungua
nut za tairi ya pancha kisha ondoa tairi hiyo.
·
Chukua tairi ya tahadhari (Spare tyre) funga
sehemu ya tairi iliyopata pancha, Funga nut kwanza kwa mkono kisha nut mbili
zinazoelekeana zikaze kwa kutumia wheel spanner, rudia tena nut zote kwa wheel
spanner, rudia tena nut zote kwa kwa wheel spanner kwaajili ya kuzikaza
usitumie bomba kwani unaweza kulegeza au kukata stud.
·
Weka tairi lililopata pancha kwenye gari ondoa
mawe au vizuizi kwenye tairi, Ondoa vigingi ulivyoweka kwa kuashiria magari mengine kuwa kuna matengenezo au
matatizo barabarani
·
Washa gari kasha endelea na safari yako.
Ni muhimu kuhakikisha
kwamba unapopata matatizo ya pancha pitia kwa waziba pancha na kuziba tairi
lako, iwapo tairi uliyoifunga ina kipara rudishia tairi lenye kashata uliyoiziba
pancha na tairi zako zinapokuwa zimeisha kumbuka kufunga mipira mingine mipya
Vilevile kumbuka
kutumia viegemezi supports kusaidiana na jeki wakati wa kubadilishja tairi, ili
kwamba iwapo jeki itashindwa viegemezi vikusaidie kushika gari kuegemea chini
upande wa tairi iliyopata pancha au upande unaobadilishwa tairi
VITU MUHIMU KUELEWA NDANI YA GARI KWA DEREVA
MWANAFUNZI.
1. Rejeta
(radiator) – Kazi ya chombo hiki ni kuhifadhi maji ya kupooza Injini
2. Oil
– Kazi ya oil ni kulainisha vyuma vinavyokutana kwenye gari, Oili ni muhimu
sana kwenye injini. Kwani ukosefu wa oil unaweza kusababisha injini kufa au
kusimama (Knock)
3. Mafuta
ya brake (Brake Fluid).- Kazi yamafuta ya brake ni kusaidia gari liwe na
brake pamoja na clutch. Kwa hivyo
unatakiwa kuangalia mafuta ya brake wakati wote pamoja na Clutch, unatakiwa
kuangalia mafuta ya brake wakati wote yawepo kwenye kihifadhio chake.
4. Betrii
(Batery)- Kazi ya betrii ni kuhifadhi moto na kutoa moto kwa kusaidia shughuli
kama kuwasha taa, kuanza mwendo wa gari (Starting) kuwa kwenye Moto/mwendo na
kadhalika
5. Ignition
coil;- Kazi ya ignition coil ni kukuza moto utokao kwenye betrii na
kuingia kwenye distributor nayo inatoa
huo umeme kwenye plugs ukiwa umepoa, plugs ndizo zinatoa moto kwenye injini.
6. Distributor
– Kazi ya distributor ni kugawanya moto kwenye injini na kufanya gari liwe na
mlio mzuri na nguvu, chombo hiki kina waya tano na ukichomoa waya mmoja tu gari
linbakuwa lina miss.
7. Plugs;-
Kazi ya plug ni kuchoma Petrol kwenye injini, Pulug inaposhindwa kuchoma
inabidi uibadilishe ili kuepuka gari kuwa na miss.
8. Fuel
Pump – Kazi ya fuel Pump ni kuvuta mafuta kutoka kwenye tank na kyapeleka
kwenye Carburator
9. Carburator
– Kazi yake ni kupokea mafuta kutoka
kwenye fuel Pump na kuyachanganya na
hewa kwa kipimo maalumu kilichowekwa na kwenda kwenye injini
10. Alternator
– Kazi ya chombo hiki ni kuchaji betrii na kusaidiana na betrii ili kutoa moto
wa betrii na kusababisha betrii isipungue moto wakati wote gari linapokuwa
linatembea.
11. Self
start. – Kazi ya self start ni kuwasha gari wakati gari likiwa bovu na haliwezi
kuwaka lenyewe, chombo hiki hifanya kazi wakati gari linasukumwa na
kushituliwa.
12. Gear
box – kazi ya chombo hiki ni kubadilisha gea na kufanya gari liwe na mwendo wa kasi zaidi au kupunguza kasi
13. Differential
– kazi ya chombo hiki ni kugawa mwendo unaotoka kwenye injini na kuupeleka
kwenye matairi
14. Cut
Out – Kazi ya cut Out ni kufanya Marekebisho ya umeme kutoka kwenye Altarnator
na kwa kipimo cha volt 12 kiingiacho kwenye betri.
SIFA ZA DEREVA.
·
Ni lazima ajue Sheria za barabarani na kanuni
zake na kuzifuata
·
Anatakiwa asiwe mlevi wa Pombe au vilevi vya
aina nyingine
·
Anatakiwa kuwa mtu wa kulikagua gari lake mara
kwa mara
·
Awe mtu wa kuwajali watumiaji wengine wa barabara
·
Asiendeshe kwa mwendo kasi wa kupita kawaida
·
Ni lazima uwe mtu wa kujihami
·
Ni muhimu unaposikia usingizi au kuchoka
usiendeshe gari
·
Asiwe mtu wa mazungumzo yaliyokithiri kwenye
gari au wakati wa kuendesha
·
Awe mpole na mwenye huruma
·
Asitumie viburudisho wakati anaendesha
·
Unapopigiwa simu ya mkononi ni muhimu kupark
pembeni ndipo uipokee.
Ufahamu kuhusu injini.
Injini ni chombo au mashine
ambayo hubadilisha nguvu ya joto (Heat
energy) na kuwa nguvu ya mwendo (Mechanical Energy) kwa ujumla injini ina
sehemu kuu tatu zifuatazo;-
·
Cylinder Head; Ni sehemu ambayo huwa upande wa
juu wa injini
·
Engine block;
Ni sehemu ya katikati ya injini ambayo sehemu kubwa ni chuma
·
Coil Samp; Ni sehemu ambayo huwa inakaa chini ya
injini, hii ni sehemu ambayoOil ya
injini inakaa.
Spring;
Kwa kawaida spring katika magari
huwa ni za aina kuu mbili
·
Spring Bar – Hizi ni spiring za kawaida ambazo
huwa ni vipande bapa vya chuma
·
Coil spring – Hizi huwa zimepindana kwa kwenda
juu zimejikunjwa mfano wa dawa ya mbu ya kuchoma.
Grease;
Ni mafuta mazito ambayo kwa
kawaida hutumika kupunguza kulika kwa vyuma yaani kupunguza msuguano “Friction”
kwa kawaida Grease hupakwa sehemu yoyote ambapo chuma hukutana na chuma kingine
Unapotaka kuzima gari kumbuka;
·
Unapokuwa kwenye gia tahadhari usiachie clutch
kwani kuna uwezekano likazima ghafla,kwa hiyo zima ukiwa umakanyaga clutch na
brake halafu badilisha gia nambari moja, vuta hand brake kisha achia Clutch,
halafu achia Brake na mwisho ondoa ufunguo.
·
Au ukitaka kuachia clutch kwaajili ya kuzima unachofanya
ni kuweka gia huru free ndio uachie clutch, kanyaga tena clutch na badili gia
kuwa Nombari moja, vuta hand brake na endelea kama hapo juu.
Pichani baadhi ya vifaa vya gari kama vinavyoonekana Picha kwa hisani
ya Rev. Kamote home Bible Library. October 24, 2010.
UFAHAMU KUHUSU BIMA ZA MAGARI NA TARATIBU ZAKE.
Kwa kawaida sheria inaagiza kuwa
magari yote ni lazima yawe yamekatiwa Bima na kinyume cha hayo utakuwa umevunja
sheria ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini ni muhimu kufahamu kuhusu
bima
Zipo aina kuu mbili za Bima
1.
Third
Party
Bima hii ni bima
ambayo haitoi malipo gari linapokuwa limepata ajali , Bima hii hueleweka kama
bima ndogo, iwapo utapata ajali kati ya gari mbili atakayelipwa ni mwenzako
kama iwapo yeye anayo bima inayofanana na yako, iwapo atakuwa na bima ambayo ni
kubwa utalipwa kutokana na bima yake.
2.
Comprihensive
Bima hii ni bima
kubwa ambayo inakuwezesha kulipwa iwapo gari yako itapata ajali iwayoyote na
kwa kawaida utaratibu ufuatao huwa unafuatwa.
a.
Dereva awe na umri unaostahili kuwa dereva au
kufanya kazi hiyo ya udereva
b.
Leseni aliyokuwa nayo dereva kabla ya kupata
ajali ni daraja linalostahili kuendesha gari hilo
c.
Leseni ya
Derevahuyo lazima iwe halali na ameipata kwa kufuata utaratibu wa
kisheria, kinyume cha hayo Bima haiatalipwa wala haita husika na hasara itokanayo na ajali hiyo kabla ya
kupata ajali ni daraja
Iwapo katika gari yako kuna redio ni muhimu kuikatia Bima
yap eke yake ili uweze kulipwa iwapo ajali itaharibu Redio hiyo.
UTARATIBU WA KUWASHA NA KUENDESHA GARI.
Unapomaliza kucheki gari yako
unaingia ndani ya gari na kuiweka free gari au gea , halafu unaweka switch on
na kuangalia taa ya heater, ikilazimika unawasha gari na baada ya hapo unaweka
gea nambari moja kasha unaachia clutch
kidogo kidogo na utaona gari linaondoka utaangalia gari mpaka lizungushe tairi raundi moja au zaidi halafu utaachia
clutch kabisa.
Gari linapokuwa barabarani
unatakiwa uwe macho na kusoma alama za barabarani na uwe mwangalifu usitoe
macho tu unatakiwa kuwa makini kwa kila alama za barabarani.
Unapofika njia panda au keepleft
Hakikisha kwanza unasimama unaagalia kulia kwako kama kuna mwenye gari
anakuja na ameshafika unampisha
apite na ambaye alikwisha kuingia
kwenye mzunguko, halafu unawasha indicator na kuonyesha mwelekeo wa kule
unakokwenda, utawasha ya kushoto kama unaingia njia ya kwanza.
Njia panda au keep
left.
Kanuni za njia panda ua keep left.
·
Unapaswa kusimama na kuangalia kulia kwako kama
gari imeshafika unaipisha ipite hususani ile ambayo imeshaingia kwenye mzunguko
·
Hakikisha kuwa unapiga indicator ya kulia endapo hutaingia njia ya kwanza utabadilisha
indicator ya kuonyesha mwelekeo wa kuelekea unakokwenda
·
50
|
50
|
50
|
50
|
- Kibao cha namba
moja kimekataza usiende spidi zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba
mbili kimeruhusu kwamba unaweza kwenda zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba
tatu kimekataza kwenda zaidi ya spidi hamsini
- Kibao cha namba
nne kimeruhusu kwenda zaidi ya spidi hamsini.
Kanuni ya njia mbili Double Road kama hakuna keepleft unapaswa kubana upande wako kama umeshafika sehemu ya upande wako wa
kuchepukia wa kule unakokwenda
Kama kuna keep left utapaswa kwenda kama keep lefti za
kawaida .
Kama kuna barabara kuu na njia
panda unabana upande wako wa kushoto ambao ndio sauti yako halafu unaelekea
utakako.
1.
Barabara hii uendeshaji wake ni sawasawa na
uendeshaji wa barabara za kawaida za double road , kwenye uendeshaji unapofika
kwenye kuchepuka unabana upande wako ambao utaingia
2.
Barabara nyngine
hazina barabara kuu wala ndogo ,ukubwa wa barabara unategemea
taa ya kuongoza magari inapowaka
3.
Kisha barabara hii ina ukubwa sana kuliko ile ya
double road ya kawaida.
4.
Iwapo barabara hii inauwezo wa ku-ovaertake
pande zote ukiona hakuna hatari.
5.
Halafu bara bara hii inayoongozwa na taa inasema
hivi;-
a.
Taa nyekundu inazuia magari yasipite
b.
Taa ya njano inasema ujiandae na kuondoka
c.
Taa ya kijani inaruhusu kuondoka
d.
Taa yam shale wa kijani inanukuu kuondoka kwenda
mshale unakoelekeza hata kama taa nyingine zinawak
Rangi nyekundu maana yake simama
subiri nyuma ya mstari buliochorwa hapa chini ya bara bara
Nyekundu na njano pamoja maana
yake ni kusimama usipite mpaka rangi ya kijani imetokea
Rangi ya kijani maana yake
unaweza kupita lakini njia ikiwa ni salama na pia ni muhimu kufanya tahadhari
kwa watembea kwa miguu hususani unapokuwa unageukia kulia au kushoto
Mshale wa kijani maana yake
unaweza kwenda upande ulioelekezwa na mshale huo na unaweza kufanya hivyo haizuru hizo taa nyingine zinaonyesha nini
Rangi ya manjano maana yake
simama nyuma ya mstari ulioko hapo chini, unaweza kwenda ikiwa labda imekutokea iwapo ulikwisha kupita
huo mstari uliopo hapo chini hivyo au
labda ulikuwa karibu sana.
MASWALI YA KUJIULIZA KWA DEREVA (MASWALI YA MDOKO).
1. Wakati
unaendesha gari ikatokea imewaka moto utafanyaje?
2. Unapopata
ajali utafanyaje?
3. Ni
vitu gani vya kuangalia kabla ya kuendesha gari?
4. Eleza
namna ya kugeuza gari katika barabara kuu
5. Ni
wakati gani unaporuhusiwa kuipita gari iliyoko mbele zako?
6. Elezea
umuhimu wa kukagua gari yako kabla ya kuondoka
7. Kuna
hajka gani wakati wa kupinda kona kubadilisha gea?
8. Ni
vitu gani vinavyotumia barabara
9. Ishara
za barabara zina faida gani?
10. Taja
sehemu nne ambazo ni makosa kuegesha gari
11. Taja
sehemu tatu ambazo ni marufuku kupiga honi
12. Unatakiwa
kusimama umbali gani nyuma ya gari lililosimama?
13. Unatakiwa
kuwa umbali kiasi gani toka gari linalokwenda mbele yako?
14. Utamjulisha
vipi Dereva wa gari lilioko mbele yako kuwa unataka kulipita wakati wa usiku?
15. Taja
mambo manne unayotakiwa kujihadharisha unapoendesha gari
16. Utajuaje
kama unaingia mjini au unatoka mjini kwenda nje ya mji?
17. Ni
mwendo kiasi gani unatakiwa kuendeesha unapokuwa nje ya mji?
18. Taja
sifa anazotakiwa kuwa nazo Dereva?
19. Unatakiwa
ufdanye nini kabla ya kupinda kulia?
20. Ni
gari la upande gani lenye haki ya kupita kwenye kona au mzunguko?
21. Utafanaya
nini kama unataka kupinda kulia iwapo kuna gari linalokuja mbele yako ?
22. Taja
vyeti unavyotakiwa kuwa navyo unapoendesha gari
23. Ni
mambo gani yanaweza kusababisha ajali taja matatu
24. Utafanya
nini Kama gari litazima ukiwa mlimani?
25. Utaangalia
nini kabla ya kuondoa gari lako?
26. Alama
ya mstari mweupe ulionyooka barabarani inakuonyesha nini?
27. Alama
ya mstari mweupe ulioachana achana unakuonyesha nini?
28. Utafanya
nini kablaya kufika mahali unapotaka kupinda?
29. Utafanya
nini unapopita mahali penye shule pasipo na alama ya kivuko cha watoto wa
shule?
30. Ni
wakati gani unapotumia kioo cha kuangaliua nyuma unapoendesha gari?.
31. Unapaswa
kufanya nini unapoendesha gari wakati wa usiku?
32. Elezea
jinsi taa za magari zinavyofanya kazi?
33. Utafanya
nini iwapo gari lako limeharibika barabarani?
34. Ni
ishara gani utaiona kama mtu mashuhuri anapita na utafanya nini?
35. Mahali
gani unapaswa kuwapisha waendao kwa miguu?
36. Utafanya
nini kama unasikia usingizi unapoendesha gari?
37. Ni
sehemu gari za viungo zinatakiwa kuwa katika hali nzuri kabla ya kupata
lesseni?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA
ABIRIA:
1. Ukiwa
dereva unatakiwa uwe na tabia gani kwa abiria?
2. Je
dereva wa abiria anatakiwa kuvuta sigara katika gari anapoendesha kwa nini?
3. Unapaswa
ufanye nini ukiwa dereva wa gari la abiria wasafiri wanapopanda ndani ya gari?
4. Utampa
taarifa gani askari iwapo atakusimamamisha na kukuhoji?
5. Kama
gari yako inashukiwa kuwa ni mbovu na kukamatwa na askari utafanya nini?
6. Je
ukiwa ni dereva wa gari la abiria
unaruhusiwa kuzungungumza na mtu yoyote kwa nini?
7. Utaegesha
vipi gari kama abiria wanataka kuteremka?
8. Kabla
hujaendesha gari la abiria unatakiwa ufanye nini?
9. Utahakikishaje
kuwa abiria wote wamekaa sehemu zao kabla ya kuondoka ?
10. Ni
vitu gani visivyoruhusiwa kupakiwa katika gari la abiria?
11. Vitu
gani vinatakiwa kuwemo katika gari kwa tahadhari ya ajali au moto?
12. Unatakiwa
kwenda mwendo gani mjini na mwendo gani nje ya mji/
13. Kila
abiria anaruhusiwa kuchukua mzigo au uzito gani
14. Kuna
hatari gani iwapo gari litazidisha mzigo?
15. Ipo
haja ya kukimbizana ili uwahi abiria? Hatari zake ni zipi?
16. Je
abiria ana haki ya kutoa ushauri anapoona mambo yananyofanywa si sawa?
MASWALI KWA MADEREVA WA MAGARI YA
MIZIGO.
1. Gari
linalobeba mizigo au mafuta lazima liwe na vifaa gani?
2. Gari
linalobeba vifaa vya hatari kama baruti, sumu na gas linatakiwa kuwasha taa
ndogo?
3. Je
ni wakati gani unapotakiwa/Kuruhusiwa kuendesha gari lenye vifaa vya hatari?
4. Kabla
ya kuendesha gari lenye vitu vya hatari unapaswa kuangalia nini?
5. Iwapo
gari lako limeharibika katikati ya barabara unapaswa ufanye nini?
6. Sheria
inasema nini juu ya utumiaji wa taa ndogo au ni wakati gani unatakiwa kuwasha
taa ndogo
7. Abiria
wanagapi wanaoruhusiwa kupakia katika gari la mizigo?
8. Ni
barabara gani utakalopitisha gari la mizigo mjini
9. Ni
sehemu gani za muhimu za gari zinazotakiwa kuwa madhubuti kwa kubeba mizigo?
10. Eleza
jinsi unavyotumia taa za gari lako usiku kama kuna gari nyingine inakuja mbele
yako?
11. Ishara
gani utaitumia unapolipita au kupishana na gari lingine?
12. Utafanya
nini iwapo utakutana na gari lingine karibu ya daraja?
13. Utatoaje
ishara ya kusimama?
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA;
1.
Endesha
kistaarabu.
Ada ya mja
kunena , Muungwana ni kitendo, Basi kama ni hivyo onyesha uungwana wako kwa
kuendesha kistaarabu barabaraniUwe mpole na uwafikirie watumia barabara
wenzako, uwe mvumilivu, mtulivu, usiwe na papara lazima uwajali watu na
madereva wengine unapoendesha
barabarani.
2.
Fikiri
kabla ya kuteenda.
Fikiri sana
kabla ya kuamua, uwe na uhakika na kila hatua ya utekelezaji , usije ukadhani
kuwa ni kosa lako tu linaloweza kuleta hatari barabarani, Hapana uwe tayari pia
kuayamaliza na kuyaepuka makosa ya watumiaji wengine wa barabara
3.
Mkono dirishani.
Unapoendesha au
kuendeshwa usitoe mkono dirishani na kuuacha hapo hapo katika hali ya
kupumzika huku kisukusuku au kiwiko cha
mkono kikiwa kimejitokeza nje ya dirisha
4.
Watoto
,Vilema na wasiojiweza.
Ni muhimu
kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya watoto wadogo , vilema na ndugu wasiojiweza,
hususani unapokuwa barabarani, hao wanahitaji huruma zako, moyo , msaada na
uelewa wako wa dhati.
5.
Ishara
alama na michoro ya barabarani.
Zijue ishara
zinazotumika barabarani, jifunza zielewe ,uzimudu na kuziheshimu alama na
michoro yote ya barabarani.
6.
Michezo
Barabarani.
Wafundishe
watoto namna ya kuziheshimu barabara na hasa namna ya kuzivuka kwa usalama , uiswaruhusu watoto kucheza
barabarani au karibu na barabara, Aidha usiwaruhusu watoto wadogo kuvuka
barabara wakiwa peke yao bila kuongozwa.
7.
Dereva
akiwa kazini;
Lazima abiria
ajizuie kumyumbisha dereva mawazo yake
akiwa kazini,usibishane naye wala
kupiga gumzo naye wala kuimba kupiga kelele au kumshitusha na au kufanya kitendo
chochote kile kitakachoathiri mawazo yake anapoedesha.
8.
Takataka.
Usitupe vipande
vya sigara au takataka zozote barabarani
WAENDAJI BARABARANI.
a). Kutembea.
1. Kutembea barabarani;
Kila mara
tembea kwenye kijinjia cha waendaji kwa
miguu kama kipo, kama hakipo tembea nje ya barabara ili au ukingoni mwake upande wa kulia mwa barabara ili uyaone kwa
urahisi magari yanayokuja mbele yako,
ukifanya hivyo utapata nafasi kubwa ya kuyakwepa magari yanayojongea uliko.
2. Kutembea
na mtoto;
Usimwachie mtoto
aende kwa imani yake mwenyewe, mshike kwa mkono wako wa kulia na utembee kati
yake na barabara upande wa magari.
3. Maandamano
ya watu;
Kundi la watu
linapofanya maandamano barabarani lipite upande wa kushoto wa barabara , wawepo watu wa kutahadharisha
usalama na kuwatahadharisha watumia
bvarabara wengine .
4.Kuzuia njia ;
Usiwazuie
wenzako kwa kusimama katikati ya njia ya waendao kwa miguu kwa sababu yoyote
ile.
5. Kuzurula barabarani;
Usisimame, kuzubaa kuzurula au kutangatanga barabarani hasa kwenye kona na sehemu yoyote pofu au sehemu nyingine yeyote ya barabara
ambapo dereva hawezi kukuona kwa urahisi.
6. Kuelekea barabarani;
Uwe mwangalifu sana utapoelekea kwenye Barabara, angalia
kwa makini kuhakikisha kuwa hakuna gari linalojongea upande uliko kaa chonjo.
Kuvuka Barabara;
1. Kuvuka
barabara ;
Kabla ya kuvuka barabara simama kwenye ukingo
wa barabara kwanza halafu angalia kulia , kushoto , halafu kulia
tena kama hakuna gari vuka moja kwa moja
mpaka ukingo wa pili usivuke kimshazari.
2. Barabara
kwenya gema au kisiwa;
Kama barabara ina gema katikati simama hapo kwanza baada
ya kuvuka nusu ya kwanza ya barabara, hakikisha kuwa madereva wa upande wa pili
wa barabara wamekuona hasa kama kuna giza.
3. Kuvuka
kwa kukurupuka ;
Usivuke barabara kama mwizi au mwenda wazimu na hasa usivuke
mahali pengine popote kama kivuko cha waendao kwa miguu kipo karibu.
4. Kuvuka
kwenye kiyuo cha magari;
Usivuke barabara kwenye kituo cha kupandia au kuteremshia abiaria
na hasa mbele au nyuma ya gari, abiria anapoingia au kutoka kwenye gari.
Kivuko cha pundamilia
1. Kivuko
cha punda milia
Hiki ni kivuko
cha waendao kwa miguu. Usivuke kituo hicho mpaka umehakikisha kuwa abiria
wamekuona na wapo tayari kukupisha , unapovuka
pepesa macho kulia kushoto na kulia tena , kama tahadhari kwa madereva
ambao inawezekana wameshindwa kusimama,
chukua tahadhari wakati wote.
2. Kivuko
chenyae kisiwa
Kuna vivuko
vingine vya watembeaji kwa miguu vyenye visiwa katikati ya barabara , endapo
kisiwa kipo katikati ya kivuko cha punda milia , vuka kila nusu ya kivuko hicho
kama kivuko kamili kinachojitegemea.
Vivuko Vinavyoongozwa.
1. Vuvuko
vinavyoongozwa na taa.
Unapovuka mahali
panapoongozwa na taa fanya hivyo tu taa ya kuvuka ikiwaka
2. Kivuko
kinachoongozwa na askari.
Endapo Askari wa
kuongoza magari haya yupo ni muhimu kuvuka barabara tu askari akikutolea ishara .
Kupanda na kuteremka.
1. Kupanda
na kuteremka kwenye gari;
Usidandie gari
wala kuning’inia. Aidha usipande wala kushuka kwenye gari likiwa bado kwenye
Msururu wa magari ngojea hadi litakaposimama na kuegeshwa pazuri au kwenye
kituo kilichoidhinishwa.
2. Kuingia
na kutoka kwenye gari.
Hakikisha kuwa
unaingia na kutokea upande wa kushoto wa
gari,ikiwa mlango wa kutokea uko kulia , basi hakikisha usalama wako kwa kuangalia kulia na kushoto na ukitoka usivuke
barabara mara moja.
Usiku, vizuizi na Mkokoteni.
1.
Matembezi ya usiku.
Unapotembea
usiku;
Unapotembea
usiku au kwenye giza , haklikisha kuwa umevaa nguo nyeupe au zinazoonekana kwa urahisi gizani au shika
kitu kinachong’aa, hali hii ni muhimu zaidi kwa
barabara za vijijini.
2. Kuvuka
vihunzi.
Usivuke vihunzi
au vizuizi vyovyote vilivyojengeka , Pembeni mwa barabara ,unapotaka kuvuka.
3. Mikokoteni.
Wenye mikokoteni
pia hawana budi kuziheshimu sheria na kanuni zote za barabarani, sukuma
mkokoteni pembeni kabisa mwa upande wa kushoto wa Barabara , toa ishara shii au
kuvuka kwenye njia panda,
KWA MADEREVA WOTE;
Afya , usalama wako na wa gari;
1. Afya
ya dereva.
Usiendeshe gari
isipokuwa kama una uhakika wa afya yako ya mwili na akili yako , Ni lazima mwili
wako na fikira zako ziwe katika mtiririko mmoja ili kusababisha hali ya usalama
barabarani, ulevi wa pombe , madawa ya kulevya
na uchovu huathiri uwezo wa kufikiri kwa makini , kupanga , kuangalia na
kuamua sawia.
2. Hali
ya gari.
Hakikisha
kuwa gari lako lipo katika hali nzuri
kabla ya kuliweka Barabarani, ukaguzi wa marakwa mara wa Breki, usukani,
magurudumu na indiketa ni wa lazima ,
Aidha hakikisha kuwa kioo cha mbele ni
kisafi na vipanguso na Wepa navyo vinafanya kazi kila wakati.
3. Ubebaji
Mizigo.
Usipakie au
kubeba gari lako mizigo mingi na mizito kupita kiasi kinachokubalika kwa
wastani.
4. Shehena
kubwa.
Ukipakia mzigo
au shehena na ulio zagaa au kujipenyeza pembeni au nyuma unatakiwa kuwa mwanagalifu sana kwa mwendo. Na ni lazima pia kuweka alama za kuwaonya watumiaji wengine wa barabara kwa kufunga
kitambaa chekundu, kama ni mchana au taa nyekundu kama ni usiku.
5. Kofia
ya usalama.
Ni vizuri kuvaa
kofia ya Usalama kwaajili ya kujikinga
kichwa dhidi ya ajali ya kugongwa kichwa , kila unapoendesha chombo cha moto
kama pikipiki n.k.
MADEREVA WAPYA NA MANJU;
Usikimbilie kuendesha gari subiri
na kuhakikisha kuwa unafundishwa na mkufunzi aliye taalamika na aliyelimbikiza ujuzi na uzoefu wa kutosha.
Usianze kwa papara utaishia pabaya. kumbuka daima kuwa kuliendesha gari ni kitu
rahisi sana na karibu kila mytu anaweza
kama akitaka na akaweza katika siku chache
tu . Kinachofanya mafunzo yawe ni kitu muhimu
na cha lazima ni haja ya
kujifunza mbinu mbalimbali za kuthibiti barabara , mazingira na gari lenyewe, ni vizuri kujifunza kuanzia hatuia za awali, Tabia njema katika udereva ili hatimaye
ujuzi na uzoefu wako ujengwe juu ya msingi imara itakayokusaidia kuziepuka ajali za barabarani kwa urahisi
zaidi. Ili uweze kuwa dereva bora mwenye msimamo wa usalama barabarani, huna budi kuanza tangu mapema kujifunza na kuyazingatia kati ya mambo mengi muhimu yafuatayo;
1. Kuzijua
kanuni
Ni lazima uujue Udereva katika mapana na marefu yake
uzijue uzikariri na kuzizingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani
kujua huko kuambatane na makusudi ya kuzitekeleza kanuni hizo ipasavyo.
2. Uwe
dereva wa kujihami;
Ni vema
ikumbukwe kuwa hata Dereva bora, anayejulikana kwa ustadi wake anaweza
akasababishwa na watumiaji barabara wengine na akapata ajali.Falsafa ya dereva
wa kujihami inaelekeza kuwa dereva asiridhike na kujua kwake sheria na
kuzitekeleza kanuni tu, wala asifikiri kuwa madereva na watumiaji barabara
wengine wote wanazijua na wataziheshimu sheria ipasavyo.Ni lazima aendeshe huku
akiwa tayari kufidia na kurekebisha makosa yaw engine kwa sahihi za kuepusha
shari na kuleta hali ya maelewano na usalama barabarani.
3. usalama barabarani;
Dereva wa
kujihami, kamwe haendeshi kwa kuwakomoa wanaofanya makosa barabarani.Udereva wa
kujihami ni udereva wa kutumia akili.
4. heshima kwa wengine;
Ni wajibu kwa
dereva kuonyesha uungwana na kumheshimu kila mtumiaji barabara.Mwenye gari
ndogo au kubwa,pikipiki, baisk eli , mkokoteni,n.k mpishe mwenye haraka au
shida kila inapobidi, hata kama wewe ndiye mwenye haki ya njia.
5. ajali
za barabarani;
Jitahidi
kufahamu kuwa, ajali za barabarani hazitokei tu, bali husababishwa.Mara nyingi
hutokea ikiwa ajizi imefanywa dhidi ya misingi hiyo, jizoeze na jizatiti
kuibaini ukiwa barabarani.
6. lijue
gari lako;
Jitahidi na uwe
na dhamira ya kuliijua gari lako lilivyoundwa.Ijue mitambo iliyopo ndani ya
gari, viungo vyake na sehemu nyingine nyeti,zikiwa ni pamoja na maguridumu.
Hali hii itakuweaesha kuwa na staha ya aina Fulani kabla hujaamua kwenda kasi
Fulani na kuzuia uwezekano wa ajali hasa zile zenye asili ya kifundi.
UDEREVA WA KUJIHAMI;
Kila siku madereva wote hupambana na hatari ambazo haziwezi
zikamhakikishia dereva usalama wake na wa gari wakati wote.Hatari hizo
zinahusiana na hali ya gari, tabia na hulka ya waenda kwa miguu na hali ya
barabara yenyewe.Lakini tofauti ya elimu,tabia hulka na ujuzi wa madereva
wanapokuwa barabarani humpa mtihani mgumu sana Dereva bora na stadi.Azma ya
usalama barabarani,imejengwa juu ya mategemeo ya kuwa na dereva wa kujihami,
ambaye atahakikisha usalama barabarani,imefengwa juu ya mategemeo yakuwa na
dereva wa kujihami, ambaye atahakikisha usalama barabarani wakati wote.
Dereva wa kujihami (tazama maana yake hapo juu Ibara Na.2)
Ni mtaalam wa medani za barabarani na anazo mbinu kadhaa
anazozitumia katika kukwepa hatari na kujiokoa yeye gari lake na watumiaji
barabara. Kwa jumla dereva wa kujihami huzingatia mambo matatu kabla hali
haijamshinda, nayo ni;
a.
Hutambua
hatari-uwezo wake wa kuhisi na kutambuahatari kubwa.Haendeshi kwa kudhani au k Udhani
au kubahatisha, bali kwa kuwa na uhakika. Zing’amue hatari mapema na amua
kuziepa hatari na na vikwazo vya
barabarani.
b.
Huelewa mbinu za uzuiaji-atajitahidi kuepuka
hatari ama kuzuia janga kutokea.Jifunze mbinu mbali mbali na uzitumie kwa
wakati ufaao au zinapohitajika.
c.
Huchukuahatua –huendesha kwa kujikiri mbele
zaidi na akinusa tatizo huamua kutekeleza mara moja. Usingoje yatokee, epusha
shari, wala usidhani kuwa atasimama yeye.Simama wewe.
TAHADHARI KWA JUMLA;
Watoto wadogo
na hata wale wanaokwenda shule wamo hatarini zaidi kuliko watu wazima.
Walindeni na
wafundisheni juu ya usalama barabarani.Wazee na wakongwe nao ni wagumu kuwaza na kumaliza kasi ya
mwendo wa vyombo vya moto vinavyowajengea wafikirieni hao pia.
Kumbukeni hali
ya afya zao, udhaifu wa macho yao, uzito wa kutembea kwao.
Waendeshaji wa
vyombo nao wajione kuwa wazima wa afya kabla ya kuendesha.Aidha magari
yanayoendeshwa barabarani yawe mazima, katika hali nzuri na yakaguliwe mara kwa
mara ili yasisababishe ajali za barabarani.Taa,breki ,usukani, magurudumu na
viungo, vingine vithibitishwe kuwa vipo katika hali nzuri.
LESENI;
Leseni ni hali
ya kisheria inaokuruhusu mhusika kuthibiti au kuendesha vyombo vya moto katika
darafa lililoonyeshwa katika leseni.Kwa
hiyo pamoja na kuwa na leseni bado dereva anawajibika kujua mbinu mbalimbali za
uzuiaji na kujifunza, kuzikariri na kuzizingatia kanuni na sheria mbalimbali za
usalama barabarani.
Aidha ni vema
ikumbukwe nia yautahini wa udereva ni kuhakikisha kuwa, mtahiniwa anazifahamu
sheria za udereva bora na kwemba amefundishwa vya kutosha, amefanya mazoea ya
sheria kiasi cha kuinukia kuwa dereva bora ambaye siyo hatari kwakebinafsi na
kwa watumiaje barabara wengine.
STAHILI YA LESENI.
Chini ya miaka
16-Hapati leseni kabisa.
Miaka 18 hadi
20-Leseni za pikipiki na magari madogo na gari za biashara.Lakini siyo magari
ya abiria wala yale makubwa ya mizigo.Miaka 21 na zaidi –Leseni za pikipiki
gari ndogo magari makubwa ya mizigo nay a abiria.
KUMBUKUMBU
Mwombaji wa
leseni za kuendesha magari ya abiria au
magari makubwa ya abiria analazimika kwanza kupata cheti cha kuthibitisha uzima
wa macho yake kutoka kwa Daktari.
USALAMA WA GARI;
Usalama wa gari
unahusu yafuatayo;
i.
Kuibiwa
au kuharibiwa kwa gari.
ii.
Kuibiwa kwa baadhi ya vifaa vilivyo sehemu ya
gari hilo
iii.
Na wizi unaokuwa ndani ya gari hilo.
MAMBO
YA KUZINGATIA;
1. Usiache
swichi ndani ya gari lako na ufunge usukani unapotoka nje au kuegesha.
2. Funga
gari lako unapokuwa hulitumii k.m ukiliegesha.
3. Funga
vioo na milango kila unapoegesha au kutoka. Usiache nafasi yoyote.
4. Ondoa
vitu vyote vyenye thamani au vifungie kwenye buti japo utakuwa umefunga milango
na madirisha.
5. Vioo
vyote viandikwe namba ya gari.
6. Hakikisha
namba ya gari lako limewekewa bima.
7. Tunza
vizuri hati ya gari yako.kama hati ya kusajiliwa.Bima pamoja na anwani (jina)la
udereva.Hivi vinaweza kumwezesha mwizi kuuza gari lako kwa urahisi zaidi.
8. Watu
wanaotiliwa mashaka kutokana na tabia zao wasipewe leseni.
9. Tegeshea
mtambo wa kuzuia wezi kama gari linao kama huna unaweza kuuweka.
10. Weka
kumbukumbu namba za vitu vya gari lako , kama radio na kadhalika
11. Jihadhari
na watu wanaoonekana kuwa na nia mbaya na gari lako , ikiwezekana jihami kwa
kutoa taarifa polisi
12. Funga
tenki la mafuta kwa kifuniko imara ili wezi wasiyaibe au kuyaongeza mafuta katika gari lako linapokuwa limeibiwa
au kuporwa.
13. Usiwaache
watoto au watu wasiojiweza kwenye gari lililofungwa au lisiloingiza hewa
14. Usiku
egesha gari lako gereji au sehemu yenye mwanga wa kutosha utakaokuwezesha kuwaona wezi kwa urahisi zaidi, lifunge
vizuri.
15. Tafakari
juu ya usalama wa gari lako na usalama wako mwenyewe kabla hujatoka kwenye gari
lako.
DARAJA ZA
LESSEN.
Daraja
la A; Pikipiki za aina zote
Daraja
la B; Magari ya aina zote isipokuwa ya Biashara ya Mizigo naya abiria
Daraja
la C; Aina zote za magari Tazama kumbuka hapo juu na mizigo
Daraja
la D: Aina zote za magari sipokuwa magari ya mizigo na Abiria
Daraja
la E: Aina zote za magari isipokuwa ya abiria
Daraja
la F: Magari ya shughuli za ujenzi
Daraja
la G: Magari ya katika shughuli za migodi na mashamba
MATAYARISHO
YA UTAHINI:
Baada
ya kujifunza vema Udereva, kuzijua na kuzitafakari sheria, ukiambatana na
mazoezi mazito chini ya mkufunzi wa udereva, hatua ifuatayo ni ile ya kwenda
polisi kutahiniwa.
Uko
kwenye kituo cha utahini mtahiniwa
atawajibika kumthibitishia mtahini kuwa
anao uwezo wa kukiendesha chombo kwa uhakika na bila kubabaisha , Aidha
amthibitishie mtahini kuwa anazijua sheria na kanuni zote za usalama barabarani.
Katika
kuelekea huko kwenye kituo cha utahini mtahiniwa ajiandae na maswala yafuatayo.
a.
Lessen ya Muda (Provisional)
b.
Gari sahii kwa adaraja la lessen unayoiombea na
gari liwe zima lenye bima na lessen
hai ya njia
c.
Stakabadhi ya ada ya utahini kutoka katika ofisi
ya serikali ya mapato (Revenue). Na ada yoyote nyingine kama ipo
d.
Chunga muda na kituo ulichopangiwa kwa utahini
kwani ukichelewa utahini utaahirishwa.
UTAHINI;
Kumbuka daima
kuwa baadhi ya mambo ambayo mtahiniwa anatakiwa kuyathibitisha katika majaribio
au utahini ni kama yafuatayo;-
i.
Umahiri
wa kuliongoza gari katika barabara ya kawaida
na katika misururu ya magari mengine
ii.
Umahiri wa kuyapita magari mengine, utumiaji wa
aina mbalimbali za barabara na namna ya kutawala kasi ya mwendo.
iii.
Umahiri wa kona na uendeshaji wa kurudi
kinyumenyume.
iv.
Uendeshaji wa
magari ya aina mbalimbali
v.
Alama ya michoro ya barabarani pamoja na
sheria na kanuni za usalama Barabarani
Onyo kwa wanaotaka kujifunza udereva.
1. Hakikisha
kuwa unafundishwa na mkufunzi aliyetaalamika vya kutosha katika fani ya
udereva.
2. Usikubali
kufundishwa na dereva anayeendesha kwa kubahatisha na mwenye kuleta mbwembwe
njiani au asiyestaarabika.
3. Usikubali
kufundishwa kwenye mkweche wa gari yaani gari lisilokuwa katika hali nzuri.
Kumbuka kuendesha
gari si kitendo rahisi sana ,Lakini suala siyo mradi kuendesha bali muhimu ni
kujifunza mbinu mbalimbali
zitakazokuepusha na uwezekanao wa majanga uwapo barabarani.
UDEREVA BORA;
Dereva bora yeyote Yule lazima
awe amepitia mafunzo ya udereva kikamilifu kutoka kwa mkufunzi aliyetaalamika vilivyo
na mwenye ujuzi wa kutosha.
a. Dereva
bora ni lazima kwanza ajihusishe na gari
lake ipasavyo, katika azima hiyo ni lazima azingatie yafuatayo;-
1.
Kagua gari lako na hasa chunguza magurudumu,
honi, milango, maji,mafuta ,taa zote pamoja na
za ishara hii iwe tabia yako.
2.
Rekebisha chochote kibovu kabla ya kuendesha kwa
mfano kiti cha kukalia, vioo, milango n.k.
3.
Jaribu breki zako kama zinafaa na uwe na tabia
ya kufanya hivyo kabla ya kuendesha wakati wote.
4.
Uondokapo uhakikishe kuwa hakuna vizuizi mbele ,
nyuma na hata chini ya mvungu wa gari.
5.
Uendeshe tu ukiwa na uhakika na iwapo mgonjwa
jizuie sana kuendesha gari.
b. Kadhalika
dereva bora hana budi kuzingatia kanuni zifuatazo kwa usalama
wake na watumiaji wengine wa barabara ,
baadhi yake ni;-
1.
Tuliza akili na fikira zako.
2.
Jifunze zikariri na uziheshimu sheria na kanuni
za usalama barabarani.
3.
Mwili na fikira zako barabarani ziwe kitu kimoja
4.
Fikiria kwanza kabla ya kutenda
5.
Jizoeze kujizuia
na uwe mwanagalifu sana barabarani
6.
Uwe mwanagalifu na mwepesi kabla ya kufanya
uamuzi
7.
Uwe na ujuzi na uzoefu wa kutosha wa gari lako
8.
Uangalifu zaidi unahitajika unapoendesha gari
mpya au ambayo sio yako.
9.
Endesha kwa akili, nenda kwa kasi mahali
panapohitajika na panapo faa kwa wakati
unaofaa tu kumbuka kuwa mjinga yeyote
anaweza akaenda kasi na akapata ajali.
10.
Tumia honi kwa akili na toa ishara zinazoeleweka
tu.
11.
Uwe mwenye heshima na adabu kwa watumiaji wa
barabara wote.
12.
Usiendeshe gari bovu aslani.
c. Endesha kwa staha ;
1.
Kumbuka daima kuwa mjinga yeyote anaweza
kuiwasha gari , akaiendesha akaigeuza
lakini kwa dereva bora huwajibika kwa hayo tu.
2.
Endesha kwa juhudi, maarifa na uangalifu ili
kuepusha ajali, unapoelekea kwenye njia
panda , kipingamizi chochote au mzunguko keep left au kupita kwenye maeneo ya
shule, hospitali na mahali popote hatari
na ni muhimu kukumbuka yafuatayo;-
I.
Nenda kwa kasi ya kawaida itakayokuwezesha
kusimama ikitokea hatari.
II.
Toa ishara (Indicator) mapoema ili wenzako wajue
makusudio yako.
III.
Jua namna ya kuzitumia barabara za aina
mbalimbali kwa usalama na bila kujihatarisha mwenyewe au kuhatarisha wengine.
Kadhalika
unaweza kuepukana na ajali za barabarani ukizingatia vipengele vifuatavyo;-
a.
Zijue hatari zinazokukabili barabarani,
unapoelekea au ukifika kwenye hatari angalia kioo chako kwanza.
b.
Utoe ishara sahii kuwajulisha wengine
unachotegemea kufanya.
c.
Punguza mwendo kabla hujapiga breki , na tazama
kioo tena.
d.
Panga gia sahii, pita kwa uangalifu.
e.
Rekebisha kasi ya mwendo wako kwa kuchunguza
kasi ya mwendo wa magarai mengine
f.
Kama kuna watumiaji wengine wa barabara wengine
barabarani basi waonye kwa ustadi.
g.
Ukiisha kuipita hatari yoyote ile ondoka upesi
hapo kwenye sehemu hatari.
Kwa maelezo zaidi ya upitaji
salama kwenye sehemu za hatari kama
kwenye njia panda soma amelekezo kwenye kitabu cha medani za barabarani cha
H.B. Bantu ukurasa wa 37 hadi 42.
Dereva anbapaswa kuliweka gari
kwenye msimamo au mkao mzuri wa
barabarani anapoendesha gari lake kwa
kasi ya mwendo wa staha na akione
kipingamizi chochote barabarani kama
watu , mawe, n.k, apunguze mwendo na kuwa tayari kusimama
Ukiwa unaendesha swala la uangalifu
ni muhimu sana siku zote .Tumia macho yako wakati wote, Usilipite gari linguine
(Overtake) sehemu
a. Yenye
kona
b. Yenye
mlima
c. Yenye
kivuko cha punda milia au kwenye kivuko cha Reli
d. Kwenye
njia panda
e. Kwenye
daraja
f.
Kwenye barabara nyembamba.
Ukifanya ajizi utapata ajali na
kuhatarisha maisha yako nay a wengine aidha ni vema ukumbuke tena kuwa;-
a. Uwe
makini barabarani usiondoe macho yako barabarani
b. Kila mara pepesa macho kwenye kioo
c. Kila
mara waone watumiaji wengine wa barabara kama chanzo cha ajali hivyo chgunga
mienendo yao.
d. Penye
gari lililo simama mbele yako chunguza
kwa makini kama kuna anayevuka barabara
e. Chunga
sana watoto na wazee, wanaweza kuvuka barabara bila ya kuchukua tahadhari
f.
Unapoyapita
magari yaliyo pembeni mwa
barabara yapite kwa uangalifu sana
g. Usihisi tu kuwa dereva mwengine atakupa hali
ya njia au kukuruhusu upite Subiri mpaka afanye hivyo.
h. Usiendelee
na mwendo kama huoni mbele
i.
Pita kushoto Keep left unapoendesha gari bana
upande wa kushoto wa barabara ispipokuwa unapolipita gari linguine.
j.
Kulipita gari linguine Overtake kunaweza
kufanyika unapokuwa umahakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo na kuwa upeo wako
wa mchoni mkubwa na hakuna msururu wa magari au magari yanayongojea.
k. Nenda
polepole kama huoni mbele sawasawa au
huna uhakika na hali ya barabara na unapopitwa na magari mengine punguza mwendo na jitayarishe kusimama kila inapobidi.
l.
Jihadhari na kutaka kuwahi kwani kunaweza kusababisha
kuyavuka magari mengine na utajilazimisha kukatisha barabara kwa nia ya
kuyawahi magari mengine jambo ambalo linaweza kukusababishia usiyawahi.
m. Kubadili
njia kwenye barabara ya njia nyingine, usibadili kutoka njia moja kwenda njia
nyingine bila uangalifu , angalia kioo ,
toa ishara chunguza kwa macho.
UNAPOENDESHA INAKUPASA.
Inakupasa uwe
katika nafasi ambayo inakuwezesha kutumia na kuongoza gari lako ambavyo unaweza kuona sawasawa ,
barabara mbele na magari mengine n.k. Umpe heshima yule ambeye yuko katika
kivuko cha kuvukia barabra kwa miguu.
Angalia sheria
za barabara na ishara (Traffic Signs) Simama ukitakiwa na Ofisa wa Polisi kufanya hivyo, angalia
ngalia kama taa zako ndogo na za pembeni zinawaka wakati wa usiku, haikupasi
kuendesha bila tahadhari kwa mwendo ambao unaweza kuhatarisha watu, ukisimama inakulazimu kuzima
injini na breki kabla ya kuacha gari,
zima taa kunwa za mbele wakati wa usiku
lakini hakikisha kuwa taa ndogo zote za
nyuma na mbele zinawaka , Ikitakiwa na Polisi onyesha lessen yako ya kuendesha
na cheti cha bima Insurance kwa ukaguzi.
Inawezekana
kuvitoa popote kwenye kituo chochote cha pilisi unachopendaHaikulazimishi
kuendesha gari lako unapokaribia kivuko cha watembea kwa miguu , kusimamisha
moto wa gari linalokokotwa na gari
linguine penye “on waiting” yaani hakuna kungoja palipokatazwa kusimama au kusimamisha magari,
kupiga honi gari likisimama . aidha sheria inataka upatikanapo na hatari yoyote
ambayo ni hasara au jeraha kwa mtu yeyote au gari nyingine
au mnyama ni lazima kusimama na saidia kama kuna mtu aliyeumia na eleza
ripoti polisi bila subira, Kwa madereva wa pikipiki skuta na waendeshaji
wa baiskeli baada ya mengi yanayotakiwa
katika sheria zinazohusu madereva wa magari pamoja na zile zinazohusu vivuko vya waenda kwa miguu pia zuinakuhusu ,
haikulazimu kuchukua watu zaidi ya mmoja kwa mshine ya miguu miwili na abiria kuketi kwa kutambaza miguu juu anatakiwa ake sawa ashikwe sawa sawa.
Maoni 93 :
nimefurahia maelezo yako yanaeleweka
maelezo mazuri sana
nimejifunza kitu kizuri sana ila picha za dash board na za sehemu mbali zagari na ingini haionekani vizuri
nice
naam kiasi chake inafaa
naam kiasi chake inafaa
Nimependa sana kujifunza na kuelewa baadhi ya vitu ndani ya Maandalizi ya kuwpo mwanafunzi wa awali wa Udereva
Nimehamasika na hii kurasa. Nimejifunza mengi sana. Nawapa hongera kwa wale wote waliochangia kuunda huu ukurasa
alie fanya hii kazi mungu ambariki nimejifunza mengi nashukur sana
Asante Sana Maiko Ngalesoni mi ni Mchungaji niliweka tu taaluma hii ili kuwasaidia watu wemgi
Asante sana Macha Baraka Jina la Bwana libarikiwe
Thanks Charles Killenga
asante sana Mr. Emmanuel Edward
Amen nakushukuru jina la bwana libarikiwe
Asante sana
naomba kujua ni ishara gani natakiwa kuionyesha ninapotaka kuingia njia kuU (MAIN LOAD)
Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.
Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.
Gold silver
Nimeipenda sana hiyo elimu ya kukijua chombo cha moto.
Duuuu mungu azidi kukupa nguvu utuwezeshe wengi kuyafahamu haya mweeee
Sijawa kuendesha gari ila kwa muongozo huu umenifungua baadhi ya mambo.
nashukuru sana kwa aliye fanya kazi njema uliyofanya mungu akubark
Mungu akubariki sana Kaka yetu, nimefarijika sana kwa kupata ufahamu huu kuhusu maswala ya udereva. Mungu akubariki sana, na kama nikipata namba yako nitafurahi zaidi Brooh.
nameupenda ukurasa huu
Mungu akubariki sana
Kweli ukurasa huu nimejifunza mengi mno mungu akupe miaka mingi uendelee kutujuza zaidi
Saidi juma
Saidi juma
Naomba ungejibu na mwswali uliobyaacha
Umenifunza mengii japo kuna maswari nimeshindwa kuyajibuu ungetujibia namaswarii ingependezaa zaidii kujua jibu sahihi.
Safi sana, ubarikiwe na Mungu
Nimejifunz kitu hapo
Ramadhani msamzi
Naitaj kujiunga
Good
Good
Yaani hapa ni shule tosha endelea kutoa elimu watu wengi wataelimika
Nmejifunza vitu vingi sana kupitia ukurasa huu
Vicent
Mliki wa OnaZote.com nimependezwa na somo hili
Asante kwamaerezo mazuri
Kuna makundi mangapi ya askali barabrani
Kuna makundi mangapi ya askali barabrani
Kuna makundi mangapi ya askali barabrani
Nzuri sana imenisaidia baba mchungaji
Nimeupenda sana huu ukurasa muandaaji mungu ampe nguvu
Ni nzui kwakila dereva
Hili somo ni zuri sana kwa dereva yyt yule
Nimejifunza kitu hapa
Kwakusoma haya nimejua gari
Ahsa te
Asante
Ahsante kwa somo lako.
Nice lecture thanks
Iko poa sana umetusaidia wemgi
Namna ya kutumia H na L mkuu
Vincent sprian
Naomba kujiunga na mafunzo
Naomba kujiunga na mafunzo ya uendeshaji
Asante sana kwa maekekezo
Nimependa sana hii elimu, natarajia kuwa dereva na nimegain mambo mengi muhimu kutoka kwako. Ahsante Sana.
Asante sana nimepata uelewa mkubwa sana mungu akubariki
Somo zuri sana
Asante na mungu akutie nguvu mwandishi kiukwel imenisaidia sana
Ahsante
Ahsante sana, nitapataje pdf
Hiyo ni nzur
Mafundisho mazuri, tunashukuru Sana.
Changamoto tu ni kuwa michoro na baadhi ya alama hazionekani ila umegusa vitu vingi vya Msingi.
hii shule iko wpi
Uko vzr mkuu
Nimekuelewa vizuli lakini ada shingapi ya udeleva wa magali ya mizigo
Nimeelewa vizuri Sana
Mungu akubariki kwa kutupa somo hili
Nashukuru nimeelewa zaid
Ubarikiwe sana kwa somo zuri ndugu
Nimependa Sana
Nimeelewa Sana mubarikiwe.
Leonard
Nimefulahi Sana Kuna kitu nimejifunza ahsante Sana
Nimeipenda xana
Dah! nimejifunza niliyokuw siyajui so nimefurahi sana
Vizur san
Vizur san
Thanks aki tumejifunza 2cioyajua endelea ku2pa elimu ndugu
Chuo cha udereva wa maroli makubwa kwa dar es salama kinapatikana wapi
Naitaji kujifunza, kuendesha gar ndogo au yoyot mawasiliano 0621091274
Taa za barabara
Safi sana
Uko vzuri sana teacher
Nashukuru teacher uko vizur sana na nimekuerewa vizur2
Vizuri sana kwa posti nzuri hakika nimejifunza kitu
Mungu akubariki sana Mtumishi,, nimejifunza mengi sana kuhusu gari kupitia huu ukurasa.
Ubarikiwe....ilipotoa Mungu akuzidishie zaidi
Chapisha Maoni