Waislamu
wamekuwa na tabia ya kushambulia wakristo na kuwashutumu katika mambo mengi
likiwemo swala la mazishi hususani swala la kuzika na Sanduku linalofanywa na
wakristo,katika eneo hili tutakuwa tunajibu na kuchambua jinsi mazishi ya
kiislamu yanavyotofautiana na mazishi ya kikristo tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vitatu vifuatavyo;-
1. Mazishi
ya Kikristo yanavyokuwa.
2. Mazishi
ya Muhamad yalivyokuwa.
3. Mazishi
ya Kiislamu yanavyokuwa.
Mazishi ya Kikristo
yanavyokuwa.
Wakristo
wote tunafahamu kuwa muongozo wetu ni Biblia,Hivyo kila tunalolifanya
linatakiwa kuongozwa na Biblia neno la Mungu,Imani yetu imejengwa juu ya msingi
wa mitume na manabii naye Kristo ni jiwe kuu la Pembeni (Efeso 2;20). Hivyo tunajifunza kutoka kwao Maandiko hayatufundishi
popote kuwa Walipokufa mitume walikamuliwa kama wafanyavyo waislamu mfano
Ibrahimu alipokufa hatusomi kuwa alikamuliwa(Mwanzo 25;7),Isaka na yakobo pia walikufa na kuzikwa bila
kukamuliwa (Mwanzo 49;32,50;1-6). Ni
muhimu waislamu kutuambia kuwa maswala ya kukamuana wanajifunza kwa nani? Maana
quran imeagiza wajifunze kutoka kwa Wakristo na wayahudi kama wana shaka katika
jambo lolote {Surat Yunusi (Yona)
10;94)}
Kwa nini
Wakristo tunazika na Sanduku?
Swala la
kuzika na sanduku limekuwa likiwakera sana na kuwachanganya waislamu wamekuwa
wakihoji kuwa wakristo wamejifunza wapi Tabia ya kuzika na sanduku?wakati
mwingine wanafikiri tunaigiza utamaduni wa kizungu,kwa kawaida Wakristo
hatufanyi mambo kinyume na maandiko yanavyo tufundisha soma (Mwanzo 50;24).
“..Yusufu akawaambia nduguze,Mimi
nitakufa,Mungu atawajia ninyi bila shaka atawapandisha kutoka nchi hii mpaka
nchi aliyowaapia Ibrahimu;na Isaka na Yakobo,Yusufu akawaapisha wana wa
Israel akasema bila shaka Mungu atawajia
ninyi nanyi mtapandisha huko mifupa yangu.Basi Yusufu akafa,mwenye miaka mia na
kumi,WAKAMPAKA DAWA WAKAMTIA KATIKA SANDUKU HUKO MISRI.”
Tunajifunza
kutoka mfano wa Yusufu.baada ya kufariki alipakwa dawa kama wafanyavyo wengi
leo na pia akawekwa katika sanduku.hatuoni pia kuwa Yesu alikamuliwa alipokufa
bali aliviringishwa katika sanda akazikwa Hakukamuliwa.Vilevile tunaposoma
katika (Yohana 11;40-44).Pale Yesu
alipomfufua lazaro ambaye alikuwa maiti siku nne baada ya kumfufua Yesu
aliamuru “Mfungueni mkamuache aende zake”Ni wazi kuwa kama Lazaro hakuwa na
nguo zake ndani ya sanda ingekuwa vigumu Yesu kuamuru afunguliwe sanda aachwe
aende zake? Hivi ndivyo wakristo wafanyavyo hakuna ubaya mtu kuvalishwa nguo
zake kasha kufunikwa na sanda na kuagwa nk.
Mazishi ya Muhamad
yalivyokuwa.
Kifo na mazishi ya Muhamad ni tofauti kabisa na
waislamu wafanyavyo leo ,Habari za kifo na mazishi ya Muhamad yana patikana
katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhamad (SAW) kilichoandikwa na Shekh
Abdullah Saleh Farsy uk 79 ambapo kuna maelezo mengi nitanukuu baadhi.
“Baada ya kuoshwa lilichimbwa Kaburi
hukohukochumbani alikofia,chumba cha Bibi Aysha.na aliyesimama kutengeneza
mwandani ni Bwana Abu Tah wa Kiansar.Baada ya hapo wakamvua nguo za
kuoshea,wakamkafini(Wakamvisha).kwa nguo tatu nyeupe za Pamba.
Baada ya kufukiziwa udi.vyema na kutiliwa
manukato vizuri kasha akalazwa juu ya kitanda kwenye ukingo wa kaburi
akafunikwa nguo moja kwa moja,baadae wakapewa ruhusa watu kuingia kumuaga mtume
wao,yakawa makundi haya yanaingia haya yanatoka,mchana kutwa wa jumatatu,na
mchana kutwa wa jumanne na usiku kucha wa kuamkia jumatano.hata karibu na
alfajiri ya hii jumatano,mtume alishushwa kaburini mwake akazikwa.Mtume amekufa
mchana wa jumatatu mwezi wa 12 mfungo sita mwaka wa 11 A.H. yaani 8/6/632”
Kwa msingi huo
hapo juu tunajifunza kuwa ,Muhamad hakukamuliwa ,alizikwa kawaida kama wakristo
wanavyozika.Muhamad aliagwa kama wakristo wafanyavyo,Inashangaza kuona wafuasi
wake hawafanyi kama Mtume wao alivyofanyiwa je aina ya mazishi ya waislamu na
uchafu wa kukamuana wanatoa wapi? Utaniwia radhi kwani unapaswa kuwa mvumilivu
ninapoanza kuzungumzia namna mazishi ya waislamu yanavyokuwa tangu hatua za
kifo hata mwisho fuatana nami katika kipengele muhimu kifuatacho
Mazishi ya Kiislamu
yanavyokuwa.
Mwislamu
anapokuwa katika hatua za kufa ,Sharti aelekezwe kibla kama haiwezekani,yaani yu
mahututi,basi kitageuzwa kitanda nyayo zikiwa zimeelekea katika jiwe jeusi
(Hajar al aswad) huku akiwa amelazwa kichalichali,Wanasema ni lazima
kumuelekeza kibla ili weze kuwasiliana
na kile kilichopo makka.Baada ya kufa anawekewa mfano wa kitu kizito katika
tumbo lake kama tofali,Baada ya kuwekewa kitu kizito juu ya tumbo lake ndipo
wanapoianza shughuli yenyewe ya Maandalizi ya mazishi,kuna idara tatu ambazo ni
1.Uchimbaji wa kaburi,ambalo linakuwa na mwana ndani
ukubwa wa mwana ndani hutegemea urefu wa nyayo za marehemu ambazo hupimwa kwa
kamba.
2.Ushonaji wa Sanda.sanda ya mwanaume huandaliwa hivi;-
a].Shuka sita ambazo mojawapo
hupimwa ridhaa tatu ambayo ndiyo sanda ya mtu mzima baada ya kukamilisha
maandalizi ya sanda wahusika wataingia ndani kwa maiti watachukua shuka moja na
kumvalisha kama msuli
b]. Pia kutahitajika
mswaki,ambacho ni kipande cha sanda kinachopimwa usawa wa kiganja cha mtu
mzima.
c]. Zinatakiwa kamba tatu
ambazo hutumika kumfungia marehemu kichwani na tumboni na miguuni.
d]. Zinatakiwa groves za kuvaa
mikononi ambazo atazitumia mkamuaji, hizi hupimwa upana wa kiganja cha mkono na
kuchana mpaka chini, zinatakiwa tatu. Huwa zinashonwa mshazari kama vile
sambusa.
e]. Marashi,udi, mkeka,na
kitanda cha kamba.
Wakamuaji
wakiwea chumbani ambako ndiko shughuli yenyewe iliko,kwanza kabisa litachimbwa
shimo katikati ya chumba,shimo hukadiriwa kuwa na urefu wa futi moja na
nusu,baadae huchukuliwa kitanda cha kamba ambacho huwekwa katikati ya
shimo,baada ya hapo huletwa vifaa vitakavyotumika ikiwa ni pamoja na ndoo ya maji.
Kule ndani
ambako shughuli inafanyika kunakuwa na watu watatu wa kwanza anaitwa kigingi au
kiguzo,kazi yake ni baada ya Marehemu kukalishwa kwakuwa atakua amelegea,basi
yeye ataweka mguu wake wa kulia,goti likiwa limegusa uti wamgongo wa
marehemu.Na mikono yake akiwa amemshika mabega .Wapili kazi yake ni kuleta ndoo
za maji ambazo zina kuwa mbili na kazi yake ni kuyachanganya maji ya moto na
baridi na kumwagilia pindi yanapohitajika.Watatu kazi yake ni mbaya zaidi yeye
ndiye mwenye kushughulika zaidi naUkamuaji.
Kwanza
watamfunika marehemu shuka moja gubigubi, hili shuka ni moja kati ya yale
sita,atalazwa kitandani,atapakwa sabuni huku mtu wa maji anaendelea
kumwagilia,hapa ataogeshwa kwanza josho la kawaida,Baada ya kuogeshwa marehemu
litatolewa hilo shuka na kutumbukizwa ndani ya shimo,litachukuliwa shuka la
pili ataogeshwa tena.
Baada ya kuogeshwa josho la kawaida, litafuata josho
maalumu ambapo maiti atakalishwa kitakotako,Mkamuaji ataanza kumkamua ambapo
wanasema “Zada imrara-hatta yakhuruju
fibutuniha”yaani utazidi kukandamizwa mpaka utoke uchafu wote uliokuwa
ndani ya tumbo lake,utaendelea kukandamizwa mpaka mavi yoote yaishe
tumboni,Baada ya hapo litafuata tendo la kupima kama uchafu umekwisha au la.
Mkamuaji
atavaa gloves ya kwanza kati ya zile tatu,baada ya kuvaa atatumbukiza kidole
chake katika sehemu ya kutolea haja kubwa ya marehemu,na kuangalia uchafu
unaotoka ni wa rangi gani?ukitoka wa rangi ya manjano atajua bado uchafu
upo,hivyo shughuli ya ukamuaji itaendelea watakandamiza mpaka waone uchafu wa
rangi ya kijivukijivu,kama kijivu itakuwa imechanganyika na manjano watabadili
njia ya ukamuaji ambapo kiguzo atamwacha akiwa amekaa,watamwangalia ataegemea
upande gani? Lengo ni kuhakikisha anapata balance bila kuegemea upande wowote
na watasema “Faidhazada ilaa yaminihi,(endapo
atazidi upande wakulia) Kana najsa
yaminiha faidhazada ilaa yasarihi,kana Najsa fi yasarihi”yaani kama uchafu
uko upande wa kulia wataendelea na shughuli hali kadhalika upande wa kushoto,wakisha
kuikalisha ile maiti ikainama wanajua shughuli ya ukamuaji imekwisha na
mkamuliwaji amekwisha kuwa safi hana kitu tumboni,baada ya hapo watamlaza na
kumuogesha tena na watachukua shuka moja na kumfuta maji,ndipo litafuata tendo
la kumpigisha mswaki ambapo muoshaji hutumia kidole chake cha shahada na kuviringisha kipande cha nguo kwenye
kidole hicho,baada ya hapo kiguzo ata panua mdomo wa maiti ili meno yaonekane
ndipo mwoshaji atakapoanza shughuli ya kumsugua meno kushoto mara tatu,kulia mara
tatu,katikati mara tatu,Baadae yataletwa maji na maiti atapanuliwa
mdomo,atamiminiwa maji na atatikiswa kichwa chake kama nazi na watarudia hivyo
mara tatu.
Baada ya hapo
zitaletwa shuka tatu ya kwanza kwa mwanaume atavishwa msuli katikati, shuka ya
pili ambayo inakuwa imeshonwa kama kanzu atavishwa, nay a tatu ataviringishwa
mwili mzima, zitachukuliwa kamba tatu na zitafungwa moja kichwani, ingine
katikati na ingine miguuni na utaratibu wa kuzikwa utakuwa unasubiriwa.
Wakamuaji
watatoka nje tayari kwa kupata uji,wakati wakisubiri uji watakuwa wakinukuu
baadhi ya aya za quran na wataomba dua na baada ya duwa watatulia kusubiri uji
na maharagwe. Uji utakapoletwa ytawekwa kwenye zilezile ndoo zilizokuwa
zikitumika kwa shughuli za ukamuaji,mbaya zaidi ni kuwa wale watu watatu
waliokuwa wakamuaji ndiyo hupewa kipaumbele kunawa maji kwanza kasha maji hayo
hupewa wengine kunawa.
Baada ya
kunywa uji watamweka maiti kwenye jeneza tayari kwa kwenda msikitini
kumswalia,wimbo huu huimbwa wanapokua njiani “La ilaa haa ilaa ilah,la
ilaa haa ilaa ilah,la ilaa ilah Muhamad rasuru-ilah”yaani hapana mola ila
Allah na Muhamad ni mtume wake.wakifika msikitini hujipanga mstari wanaswali na
kuiswalia maiti na kuiombea dua kama hivi.
Allahuma aki
daru khayri min daarith-ewe
Alla mpe nyumba bora kuliko nyumba yake,
Allahuma ati
ahalal……..mina
ahaliha-mpe watu bora kuliko watu wake,
Allahuyma ati
zawji min zawjiha-mpe
wake bora kuliko wakeze.
Baada ya hapo watatoka msikitini wakiimba wimbo ule wa
kwanza na wanapofika makaburini
hubadilisha na kusema Allah-u-Akbar-Allah-u-Akbar
x3.
Kwa mujibu wa
dua hizo hapo juu mwanaume anapokufa huombewa apewe wanawake bora kuliko wakeze
lakini anapokufa mwanamke dua hii haisemwi! Hivyo katika uislamu wanawake
mtajiju.
Ndani ya
kaburi kutaingia watu wapatao watano ambao watamhifadhi marehemu wakati huo juu
ya kaburi kutakuwa kumefunikwa shuka ili watu wasione mambo yatakayotendeka
ndani maiti ya (kiislamu inafichwa sana). Watu waliopo ndani watampokea
marehemu na atatua juu ya magoti yao akiwa chali,baadae hushikwa ubavu
mmoja na kutumbukizwa ndani ya mwandani
ambapo huhakikisha uso wake umeelekea kibla (makka kwenye jiwe jeusi).endapo
maiti atakuwa mwembamba kuliko mwandani atawekewa nyasi ili awe sawasawa na
mwandani bila kupwaya, atawekewa mto ambao kwa kawaida huwa ni udongo. Baada ya
hapo kutaagizwa kisu ambacho kazi yak e ni kukata sanda eneo la sikio moja
kwani maiti huwa analazwa kiubavubavu,sikio hilo hubaki wazi ili liguse ardhi
wanaamini marehemu atatumia sikio hilo kusikia maswali atakayoulizwa humo
kaburini, kasha utaagizwa ubao ambao hufunikia eneo la juu la mwandani,endapo
ubao
utakua mwembamba yatachukuliwa majani ili kuziba eneo
lililobaki wazi kisha wataweka udongo ,shuka litatolewa na waliokuwemo kaburini
watatoka na wakati huo hata ukitazama huoni kitu ndani hivi ndivyo jinsi maiti
ya kiislamu inavyofichwa,kasha watu wataazna kufukia.Baada ya kumaliza kufukia
litafuata swala la kumuombea dua na kumfundisha marehemu kujibu
maswali.kunakuwepo kibirika chenye maji
wanamwagilia juu ya kaburi wanaamini kuwa yale maji yaliyo mwagwa juu ya kaburi
yanapenya udongo na kuingia kwenye sikio la juu na kutokea kwenye sikio la
chini,halafu mtu yule anafufuka ,baada ya kufufuka atakaa na kusema
alhamdulillahi kumbe nimekufa1! Hapo wanaamini kuwa ataanza kusikia. Sheikh
Anasoma kitabu kiitwacho Talakini l-mait yaani kitabu maalum cha kuzikia,
wanamfundisha kujibu maswali kwani wanaamini wasipomfundisha kujibu maswali
vitakuja viumbe kumuuliza maswali na endapo atashindwa kujibu atapigwa
marungu.katika kitabu hicho uk wa 104-105 atafundishwa hivi;-
“Yaa amalallah bint hawai,udh-uru l-ahad
khalajat,mindari dunia,I laa dar akhera wa huwa shahaadatan an laa ilaha
Muhammad rasur-Illah,wa ana jannat hakkon,wa anna nnara hakkon,waanna l-maut
hakkon, wa anna l-qabur hakkon,wa anna l-mu-nkara-nnakira hakon, wa anna suila
hakkon,wa anna l-jawaba hakkon.”
Tafasiri ya maneno hayo ni kama ifuatavyo;-
“Ewe mja wa
allah motto wa mwanamke kumbuka ahdi ambayo ulitolewa katika nyumba ya dunia
mpaka nyumba ya kuzimu nawe ni mwenye kushuhudia hakuna mola ila allah na
Muhamad ni mtume wake,kwa hakika pepo ni haki yako,kwa hakika kufa ni haki
yako,kwa hakika kaburi ni haki yako,kukujia viumbe viwili vyenye kutisha ni
haki yako na hivyo viumbe viwili kukuuliza maswali ni haki yako na wewe
kuwajibu ni haki yako”
“Ewe fulani bin fulan umetoka katika ulimwengu wa dunia
umeingia katika ulimwengu wa kuzimu,ukiwa kuzimu sema hakuna mola ila allah na
hakika Muhamad ni mtume wa allah, leo hii kupata pepo ni haki yako na leo hii
kuunguzwa moto ni haki yako,viumbe vyenye kutisha ni katika viumbe wa allah.
Yaa…..L 1-anna yattika,L-Karima,walaa yuvihibaka fainahumma khalaqu min – allat
llah.Faidhhhsaalaka. (Sisi tutakapoondoka Watakujia viumbe vya allah sw. hivyo
vitakuuliza maswali yafuatayo;-
Maaismuka…………………………...…Jina lako nani?........................................................................
Manni Rabbuka?.........................Mola
ni wako nani?............................................................................
Wa man
Nnabbiyyuka?...............Nabii
wako nani?...............................................................................
Wa maa
Imammuka?..................Kiongozi
wako nani?..........................................................................
Wa maa diynuka?........................Dini yako
ni nani?..............................................................................
Wa maa kibbilatuka?...................Kibla
(uelekeo) chako ni kipi?..........................................................
Wa maa I
khiwanuka?..................Ndugu
zako akina nani?...................................................................
Fukullu………………………………………Wewe utasema
kuwaambia…………………………….
Ismi…………………………………………...Jina
langu ni Fulani bin Fulani………...........................
Allahu Rabbi……………………………….Allah ndiye
Mola wangu……………………………......
Wa Muhamad
Nabii……………………Na
Muhamad ndiye nabii wangu……………………….......
Wal-qur-an
Imam……………………….Na
quran ndiyo kiongozi wangu…………………………...
Wal-qaaba
Kibrati………………….......Alkaaba
ndiyo kibla yangu………………………………....
Wal-Islama dini……………………………Na uislamu ndiyo dini
yangu…………………………….
Wal-muumun wal-muuminat kulumIkhiwani…Waisalamu/kike/kiume ndio ndugu zangu.
Faajibu hadha bi kauli dhabit………Wajibu
haya pasipo kutetemeka wala kuwa na woga
tena kwa lugha ya kiarabu.
Baada ya hapo itaombwa dua maalum kwa
ajili ya marehemu na baada ya dua hiyo watu wote hutawanyika.
Na kwa ajili ya hayo yatakuwepo marungu ya
chuma kila mara watakapotaka kutoka humo watarudishwa humohumo na kuambiwa
ionjeni adhabu.(Quran). Hivyo kuna adhabu ya marungu huko kaburini, tena
Muhammad analielezea rungu hilo kuwa ni zito sana kiasi kwamba hata kama watu
wote ulimwenguni kuanzia Adamu mpaka mtu wa mwisho kuzaliwa ulimwenguni tungejaribu kuliinua
tusingeliweza.
Hata hivyo mashehe hudanganya watu sana kwani
kwa mujibu wa quran maiti haisikii. Quran
12;106.(Ufafanuzi wa 106),35;22,
soma Biblia pia Mhubiri 6;4,Ebrania 9;25.
Je waislamu wamejifunza kwa nani kuwa maiti inasikia? Ni vizuri kuchagua leo
kudanganywa au kuiamini injili na pia mwili wako usikubali kuchezewa njoo kwa
Yesu Yeye nira yake ni laini.
Maoni 1 :
Wewe inaonekana huijui kabisa dini ya kiislam maneno unayoongea ni ya kizushi
Chapisha Maoni