Ni mwaka juzi tu sio siku nyingi
wakati huo nilikuwa nasubiri kwenda kujiunga na chuo cha biashara, baada ya
kuapata nafasi pale, nilikuwa kwa kweli sina shughuli maalumu, nakumbuka hapo
jirani na nyumbani (Tandika) kulikuwa na jamaa mmoja ambaye alikuwa mnoko sana
yaani mkorofi sana , huyu jamaa alikuwa haelewani na mtu, anajifanya mjuaji na
anajifanya kasoma sana na anajifanya
kuwa ndsiye mwenye hela kuliko kila mtu.
Huyu ndiye Tabu aliyeshikisha mtu Adabu!
Alikuwa ni mtu mzima kidogo
mwenye umri kama wa miaka 50 kiumri, mkewe alikuwa na umrimdogo mwenye miaka
kama 22-23 huyo alikuwa ni mkewe wanne kwani kwa sababu ya ukorofi alikuwa
akikimbiwa na wanawake, siku moja nikiwa nimekaa nilisikia kelele hapo kwa huyo
jirani , ilibidi nitoke kwenda kushuhudia kulikoni tabia ambayo kwa kweli ni
umbeya mtupu, nilipofika pale nilimkuta Yule jirani akiwa amemkunja kijana
mmoja kwa kumkosea adabu. Nilipoona anataka kumpiga ilibidi niingilie kati na kujaribu kumsihi amuache nikimwambia kuwa
amekosa, Yule jamaa aliacha kumshughulikia Yule kijana na kunigeukia mimi na kuanza kunishambulia kwa maneno
nilishangaa kwa sababu nilichokuwa nakifanya mimi niliona ni kitendo cha
uungwana , alichambua kwamba najifanya nimesoma sana najiona msomi wa mtaa na
kwamba ati tunajifanya familia tajiri, kwa kweli sikumjibu kwa sababu nilikuwa
namfahamu vizuri kuwa ni mtu wa shari, nilichokifanya ni kuondoka na kurudi
nyumbani, umbea ulikuwa umenitokea puani. Lakini nilipofika nyumbani niliona
sikuwa nimejitendea haki kumwacha Yule jirani aniadhiri kiasi kile halafu aende
akiwa huru, Nilijiuliza maswali na kujipa majibu kwamba nilitakiwa kujibu
mashambulizi yale.
Niliamua kurudi tena
nikiwa nimepania kumfundisha adabu, Nilipofika pale kwa jirani
niliambiwa na mkewe kwamba alikuwa ameshaondoka, nilianza kumpa mkewe maagizo
ya kiamri kwamba mumewe akija amwambie kwamba
kunyamaza kwangu hakukutokana na kumuogopa na kumwambia kuwa ni lazima
ningemshikisha adabu, Yule mke wa jirani alibadilikia na kuniambia nimsubiri
mwenyewe akija niende nikamwambie yeye
(mke) hakuwa tarishi wangu, nilimwambia kwamba wenzake watatu wameshaoindoka
kwenye nyumba ile yeye pia hana nafasi ya kudumu Yule mke wa jirania alisema
kuwa hayo hayanihusu kwani hata mama yangu anaweza kuachika pia, alipomwingiza
mama yangu kwenye mabishanao hayo niliona kama amenivua nguo hadharani,
nilimwambia nitamshikisha adabu asipochunga mdomo wake. Nadhani alikuwa
amefundishwa tusi moja tu maishani mwake
linalohusu mama wa wengine kwani
aliniambia nimshikishe adabu mama yangu kwanza, Hapo sikuweza kuvumilia, nilimfuata
pale mlangoni alipokuwa amesimama,
nilipomfikia tu nilirusha kibao, lakini kwa ustadi wa ajabu sana alikidaka kile kibao changu na kunisukuma, niliyumba na
kurudi nyuma hatua kadhaa nilimfuata
nikiwa nimepania sana safari hii,
Nilimkata mtama, lakini
hakuanguka Badala yake alinishika na kunipinda ghafla kabla hajanitupa chini, niliinuka nikiwa
nimetahayari nilijua ule wakati wa kufedheheka umewadia nilipomfuata safari hii
nilijaribu kitu kingine, Nilimrushia ngumi za chapuchapu, lakini zote aliziona
na kuzikwepa, halafu nilihisi vitu kama mawe kimoja kikitua kwenye mbavu na
kingine chini ya jicho, zilikuwa ni ngumi za mwanamke, kabla sijakaa sawa
nilikuwa nimeenda chini yule mwanamke ambaye alikuwa mrefu mwembamba alinifuata
pale chini na kunikwida. Alianza kunisulubu kwa ngumi za usoni za haraka haraka.
Naomba kwanza niseme kwamba zile sifa za majina ambazo huwa zinaandikwa na
wataalamu wa utambuzi wakati mwingine ni kweli Yule mwanamke alikuwa anaitwa
Tabu, hivi karibuni nilisoma jina la tabu gazetini wakielezewa kuwa ni wanawake
wenye nguvu hasa wakiwa warefu wembamba,
Nilipojaribu kuinuka sikuweza,
ilibidi jirani waingilie kati waje
kuniamulia niliposimama nikiwa na nundu mbili na damu ikinichuruzika mdomoni
nilisema tutaona nimekwachia kwa sababu
u mwanamke, Bila shaka jirani zangu walikuwa na kila sababu ya kucheka kwani
walicheka baada ya mimi kusema maneno
yale, nilianza kuondoka polepole kinyonge, kwa aibu na kifedheha kuelekea
nyumbani, najua unataka kujua kama mume wa Yule mtesi wangu akiambiwa kuhusu
ugomvi ule na kama alikuja nyumbani kunitafuta kama nilivyoamuru, Utanisamehe
kwani tangu siku ile nilijifunza kuwa jambo baya kuliko kuliko yote duniani ni
umbeya, na kuingilia mambo ya watu
wengine, kwa hiyo naomba usiingilie mambo yangu. Au we mwandishi wa habari? Nyau
we!
Maoni 2 :
shukran sana yaan ni perfect ni nimejifunza mamb mengi kuhusu udereva
shukran sana nimejifunza mamb mengi kuhusu udereva
Chapisha Maoni