Somo la pili.
Vijana na Uhusiano.
Katika
somo lile la kwanza sehemu ya pili somo lile la vijana na stadi za maisha
niligusia kuhusu uhusiano.Uhusiano ni
mojawapo ya swala la muhimu katika maisha ya mwanadamu,Hatukuumbwa tuwe peke
yetu,hivyo basi kukosekana kwa mahusiano kwa kweli kunaweza kusababisha fikira
potofu,upweke na kukosa kuelewa ukweli kuhusu maisha,si unajua kuwa
tunahitajiana ndio na si sisi tu ukweli ni kuwa tunahitaji mpaka viumbe vingine
visivyo vya aina yetu kama mimea wanyama,nk.lakini wanadamu tunahitajiana sana
na hilo ndilo ninalotaka kulizungumzia hapa.tunahitaji marafiki,ndugu,jamaa na
ushirika,tunahitaji marafiki hata wa jinsia tofauti na sisi.
Hitaji
la kuwa na marafiki.
Kama mtu angeniuliza swali leo kuwa ni
wakati gani katika maisha uliweza kuishi kwa furaha ningemjibu vema kwamba ni
wakati wa utotoni au wakati nilipokuwa ninasoma shule ya msingi na sekondari na
vyuo,baada ya hapo siwezi kueleza tena kama ninayafurahia maisha,na sababu
kubwa ni kuwa sasa nina marafiki wachache sana na ambao huwapata kwa muda mfupi
tu na wakati mwingi ninaishi maisha ya upweke nitakuelezea vizuri athari za
upweke tutakapofikia hatua hiyo lakini
ninachotaka kukazia hapa ni umuhimu wa kuwa na marafiki katika maisha
yetu kama wanadamu,Maisha ya kuwa mchungaji kama nilivyo leo yalinipunguzia
sana kuwa na marafiki sisemi kuwa kazi hii ni mbaya hapana lakini ni gharama
tunazolipa za kuwa watumishi wa Mungu hii ni pamoja na kuwa na vipindi tengefu
ambapo tunakuwa kama tumetengwa au tumejitenga. Ninahisi kuwa katika mazingira
Fulani vijana nao hupitia hali kama hizi kwa hiyo naona ni muhimu kuwa na
marafiki.
Je kila mtu anafaa kuwa rafiki?
Hata pamoja na umuhimu wa kuwa na
marafiki ni muhimu kufahamu kuwa si kila mtu anaweza kuwa rafiki,ni kweli kuwa
tunapaswa kuwa na amani na watu woote lakini si woote wafaao kuwa marafiki
hivyo ni lazima tuchague marafiki sawa na mapenzi ya kimungu. Si tunakumbuka
kuwa marafiki wana uwezo mkubwa wa kuchangia katika kujenga au kuharibu maisha
yako na tabia yako (Ikoritho 15;33).
Katika mstari huu Biblia inasema hivi “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya
huharibu tabia njema.” Ki msingi biblia hapa inazungumzia marafiki, na sio
mazungumzo tu, watafasiri wa biblia yetu ya Kiswahili walitumia neno mazungumzo
mabaya, ambalo katika biblia ya kiingereza hutumika hivi, “ Do
not be deceived; evil companionships corrupt good habits.” . Kwa
msingi huo kinachozungumzwa hapo ni zaidi ya mazungumza kama biblia ya
Kiswahili isemavyo, hapa panazungumzia marafiki!Unaona!. Hivyo kumbe kama
tutakuwa na marafiki waovu wanaweza kuchangia kuharibika kwa tabia zetu njema
tulizo nazo ni muhimu kufahamu kuwa tabia mbaya huambukiza kwa haraka kuliko
ilivyo kwa tabia njema.
Ninawezaja
kuchagua marafiki walio wema wema?.
Kabla ya kuzungumzia swala la kuchagua
marafiki nataka nikupe hadithi moja ya mnyama aliyeitwa ngamia,Siku moja
msafiri mmoja wa jangwani alikuwa na ngamia kadhaa waliokuwa wamembebesha
mizigo,Hata walipokuwa wakiendelea na safari jangwani ngamia mmoja aliugua na
kushindwa kuendelea na safari hivyo alizimia, msafiri alifungua mizigo na
kuibeba kwa ngamia mwingine kisha akamwacha jangwani akijua kuwa ngamia yule
amefariki baada ya muda Fulani ngamia yule alipata nguvu na kuamka akijikuta
peke yake jangwani,kwa bahati kulikuwa na majani mazuri mahali na hivyo aliweza
kuishi vizuri, Siku moja mfalme wa jangwa Simba na rafiki zake watatu
kicheche,fisi na chui walikuwa pamoja nae,Simba alishangaa kumuona mnyama huyo
wa kufugwa akiwa peke yake jangwani na alimuuliza kulikoni ngamia alimwelezea
simba yoote yaliyomkuta,Simba alimhakikishia Ngamia usalama na kumwambia kuwa
hakuna atakayemgusa na kuwa wataishi pamoja kwa amani hivyo ngamia alifurahi
sana .Siku moja Mfalme simba alijeruhiwa vitani huko nyikani katika vita
waliyopigana na tembo hivyo alizidiwa na kuishi pangoni rafiki zake walimletea
chakula cha mawindo kila siku hata hivyo wakati huu kulikuwa na hali ngumu ya
upatikanaji wa mawindo na hivyo ilikuwa kwamba mfalme alikuwa hashibi na hali
yake ya ugonjwa ilizidi kuwa mbaya, Siku moja fisi alitoa wazo kwamba ni vizuri
mmoja wao ajitoe kama chakula kwa mfalme ili kunusuru uhai wake fisi alitoa
wazo hili huku akijua kuwa kwa kuwa wao ni wanyama wa jamii moja hawawezi
kulana wao kwa wao lakini waliamua kuigiza ili kwamba wamle ngamia ambaye
alikuwa mkubwa na kingekuwa chakula cha kutosha kwa muda mrefu kiasi hivyo kicheche alianza kwa kujidai anajitoa
kwa mfalme hata hivyo mfalme alikataa kwa kuwa alidai kicheche alikua ni
mdogosana na asingeliwatosha wote,kabla mjadala haujaisha fisi alidakia mfalme
na anile mimi kwani fisi ni mdogo lakini kabla mfalme hajajibu chochote Chui
nae alidakia kuwa yeye alikuwa mkubwa kiasi cha kutosha na angelifaa kuliwa na
mfalme hata hivyo mfalme alikataa kujitoa kwa chui kwani woote hawa walikuwa
wanyama wa jamii moja na woote wanakula nyama na si majani na kwa kawaida
wanyama wa jinsi hii huwa hawalani,Ngamia alipoona kuwa kila mnyama aliyejitoa
ofa kwa mfalme mfalme alikataa ofa yake yeye naye alijipeleka na kumwambia
mfalme na anile mimi kwani wao ni wa jamii moja na ni wadogo wasingelimtosha
mfalme ndipo Mfalme aliposema nimekubali
ofa yako ee ngamia muungwana na mara akamrukia na kumla na rafiki zake hadithi
hii inatufundisha umuhimu wa kuchagua marafiki wa kweli.
Waswahili wana msemo usemao kuwa ndege wa
aina moja kwa kawaida huruka pamoja, msemo huu unaweza kuungwa mkono na maneno
ya nabii Amosi katika (Amosi 3;3)
ambapo Biblia inasema “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana?” hii ina maana
kuwa mara nyingi tunaweza kuvutwa na watu ambao tabia zao zinapatana na za
kwetu,kwa msingi huu lazima marafiki zetu wawe wale ambao kwa namna Fulani wana
tabia au mtazamo unaolingana na matakwa yetu, Vijana wengi ambao huvuta sigara
au bangi hupendelea kukaa vijiweni kwa wenzao ambao wanaweza kuvuta nao pamoja
kuwapatia moto au hata sigara ama bangi na viberiti vya kuwashia,kwa hivyo ni
muhimu kujua rafiki zako wana mtazamo gani na wewe unapendelea nini. Hiki ni
kipimo kizuri cha uchaguzi wa urafiki.
Aidha waswahili wana msemo mwingine
usemao akupendaye wakati wa dhiki huyo ndiye rafiki, msemo huu unaweza kuungwa
mkono kibiblia na ile mithali katika (
Mithali 17;17) ambapo biblia inasema “Rafiki
hupenda siku zote Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu” Ki msingi rafiki wa kweli ni yule ambaye
atakupenda siku zote hata wakati wa matatizo,rafiki wakweli hatakuacha uingie
pabaya kisha aseme nilijua tu utaingia
pabaya lakini niliogopa kukuambia,siku zote rafiki wa kweli ni yule ambaye
anakueleza ukweli hata pale ambapo hutapendezwa na anayokuambia maadam tu
anajua kua alilokuambia lina faida na ni la muhimu kwako.
Ni muhimu kuwa na rafiki ambaye kwako
atachangia uwe na tabia chanya kwa kadiri unavyoshirikiana naye unabadilika
kitabia anakupandikizia mambo mazuri na unafaidika kwa kuwa naye katika mtazamo
wenu, maana yake kama woote mmeokoka atakuwa kichocheo kikuu katika maswala
yote ya kumcha na kumtumikia Mungu, Jihadhari na rafiki yeyote anayeonekana
kuwa na tabia za kinafiki kama Yuda aliyeonekana akimbusu Yesu kumbe anatoa
ishara ya kukamatwa kwake,rafiki wa kweli atakuwa anakuwazia mema (Mithali 27;6) atahakikisha kuwa
anakulinda na madhara (1Samuel
18;1-4,20;1-4) atakuwa anatoa ushauri wenye kujenga na kukulinda,atakuwa ni
mtu muaminifu anayeweza kukushirikisha hisia zake au wewe kumshirikisha hisia
zako katika wakati woote huu kumbuka kuwa hakuna mwanadamu aliye mkamilifu
hivyo kutakuwa na mapungufu ambayo kwayo mtakuwa mkichukuliana.kumbuka kuwa
wewe pia sio mkamilifu.wakati woote huu
sheria ya dhahabu itakuwa ikipewa kipaumbele ile sheria husema hivi;-
“Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu
nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.”Wakati
wote huu ni muhimu pia kuwa na ujuzi kuwa biblia inatahadharisha kuwa na
urafiki na watu wenye mizaha (zaburi
1;1-6) au watu wenye ushawishi dhidi ya kutenda uovu (Mithali 1;10-19). Na kwa vijana waliokoka wanapaswa kuwa makini
kiimani kufungiwa nira na mtu asiyeamini (2koritho
6;14-18) hapa inazungumzia ushirika wa ndani sana na wale wasioamini sisemi kuwa hatupaswi kushirikiana
na watu wa dunia hii lakini ushirikiano wa mkristo na mtu asiyeamini ni wa
lazima au muhimu pale tu inapolazimu kwa kusudi la kujenga jamii au uchumi au
katika kuwaonyesha wasioamini njia ya wokovu,lakini si kibiashara,ndoa,uchumba
n.k.Hii ni kwa sababu kihistoria popote pale watu wa Mungu walipojisahau na
kujichanganya na watu wa duinia watu wa Mungu walivutwa duniani na kupoteza
maadili yao na wakati woote huu zingatia rafiki ambaye atakupa ushari ulio sawa
na imani yako na sio kinyume (2Samuel
13;1-5,16;21-22).
Swala
la urafiki na Jinsia tofauti.
Kimsingi urafiki wa watu wa jinsia tofauti
haupigwi vita katika biblia na kinyume chake tunayo mifano katika maandiko ya watu wanaume ambao
wamekuwa na marafiki wanawake (mf.Yesu katika Luka 10;38-39,Yohana 11;5,Paulo
mtume katika Warumi 16;1,3,6,12).Urafiki
huu ni urafiki wenye dhamiri safi,ni urafiki unaohitaji kuwa na fikira
adilifu,watu wengi hushindwa na aina hii ya urafiki na hujikuta wakiishia
pabaya ni muhhimu urafiki wa na jinsia tofauti ukajengwa katika misingi ya
uadilifu kama tutajifunza kufanya hivyo,urafiki na jinsia tofauti una raha zake
na unamuimarisha mwanadamu kisaikolojia,mwanamke hawezi kuwa mkamilifu bila
mwanaume halikadhalika mwanaume hawezi kuwa mkamilifu bila Mwanamke “Walakini
si mwanamke pasipo mwanamume,wala mwanamume pasipo mwanamke katika Bwana”(1Wakoritho 11;11)Hii ina maana kuwa
jinsia zote mbili zinahitajiana kimaumbile na kunahitilafu kubwa za kimaumbile
zinazoweza kujitokeza endapo binadamu atakua katika mazingira ya kuikosa jinsia
nyingine,Mtaalamu mmoja wa Saikolojia ya wanadamu alikuwa akihojiwa katika
television kuhusu kuwepo kwa tabia za ushoga na usagaji mataalamu huyu alisema
moja ya sababu kati ya nyingi zinazochangia tabia hii kujitokeza ni pamoja na
jinsia moja kukaa pekee katika mazingira Fulani kwa muda mrefu bila muingiliano
na jinsia nyingine mtaalamu huyu alitoa mfano wa Magerezani,Shule za bweni
n.k,alisema kimaumbile hali hizi hupelekea kuzaliwa kwa tabia hii aidha kwa
muda mfupi na wakati mwingine kwa muda mrefu. Hivyo wanawake na wanaume
wanahitajiana kimuingiliano katika jamii hata kama si katika mahusiano ya
kingono. Yako magonjwa ya kisaikolojia ambayo huwapata wanawake wanapokosa
muingiliano na wanaume kwa muda Fulani na wakati mwingine magonjwa hayo ya
kiakili huweza kufikiriwa kuwa ni pepo wabaya ,lakini pamoja na kuwepo kwa pepo
wabaya ni muhimu tukakubali kuwa tatizo hili lipo kama vile kulivyo na kifafa
cha kipepo na kifafa cha kawaida.kumbe basi kuna umuhimu wa kuwa na marafiki wa
jinsia tofauti.Lakini ni muhimu pia kukawepo na mambo ya kuyazingatia
tunapokuwa na marafiki wa jinsia tofauti ili kutulinda tusijiingize katika
mahusiano ya kingono.
Mambo
ya kuzingatia katika urafiki na watu wa jinsia tofauti.
Kama nilivyogusia awali kuwa kuna umuhimu
mkubwa kimaumbile kuwa na urafiki na jinsia tofauti kwa jamii nzima na kwa
wakristo pia, jambo la muhimu ni kujenga msingi wa kimaadili kwanza hii ina
maana ya kuwachukulia rafiki hawa kuwa kama kaka na dada akimshauri mchungaji
kijana Paulo mtume alimshauri Timotheo kuwaona wanawake wazee kama mama na
wanawake vijana kama ndugu wa kike katika usafi wote. (1Timo 5;2).kwa msingi huu ni muhimu kuwa na mijadala,mahubiri ya
pamoja,kusalimiana na kuwasaidia katika
mazingira ya kuhitaji msaada,Paulo mtume alifanya kazi ya injili na wanawake
wengi sana wakiwa ni wadau au watenda kazi pamoja naye soma wafilipi 4;3Biblia inasema hivi, “Naam
nataka na wewe pia mjoli wa kweli,uwasaidie wanawake hao kwa maana
waliishindania Injili pamoja nami,ambao majina yao yamo katika kitabu cha
uzima”Unaona!. Ni wazi kuwa Euodia na Sintike walifanya kazi ya injili pamoja
na mtume Paulo.Hivyo kuwa na marafiki wakike na wakiume inaewzekana lakini ni
lazima tuzingatie mambo ya msingi kwani kuna tatizo.
Tatizo kubwa la urafiki huu hasa kwa
vijana ni zile tamaa za ujanani na ule
ukuta wa fikira adilifu ambao haujajengeka miongoni mwa vijana,hii ni fikira
kuwamba kuwa na urafiki huu hupelekea watu kufanya ngono,(2Timoth 2;22). Hivyo ni lazima vijana wachukue tahadhari wanaporuhusu
urafiki wa jinsia tofauti kwa sababu ni kweli urafiki huu kiutafiti unaonekana
kufanikiwa kwa watu wachache na wengi huushindwa.
Utafiti wa hivi karibuni uligundua kuwa aina
hii ya urafiki hupelekea watu kuwa na upendo uliopumbazika,utafiti huu umebaini
kuwa 87% ya wasichana na 97% ya wavulana waliokuwa na urafiki wa jinsia tofauti
waliishia kufanyana ngono,hata hivyo 65% ya wasichana na 43% wavulana walikuwa
na urafiki na watu wa jinsia tofauti bila ya kufanya ngono.
- Mmoja ya wasichana aliyekuwa na urafiki na mtu wa jinsia tofauti akaishia kufanya ngono alitoa ushuhuda huu,Dada huyu aliyeitwa Loretta aliyekuwa na umri wa miaka 22 alisema tulivyoanza urafiki na mwanaume kadiri siku zilivyoendelea tulihisi kupendana na kuhusika kwa karibu kwa hisia za kila moja wetu,lakini hatimaye tulikuwa tuna kumbatiana,baadaye tuliona hakuleti msisimuko tena hivyo tulianza kupeana busu,pia baadaye tuliona ni jambo lisiloleta msisimko na tulianza kutomasanatomasana na ikafikia hata kutomasana sehemu za siri,wakati huu nilijihisi niko tayari kabisa kutoa penzi langu kwa mvulana yule kwani nilijihisi kuhemkwa na kuhitaji kutimiziwa hamu ya kingono na kama ujuavyo wavulana huwa wepesi kusimamisha uume na kuwa tayari kimapenzi tuliishia kupeana mapenzi.
Jaribu kuwaza matokeo
yaliyomtokea Loretta unahisi alikuwa na hali ya namna gani?Loretta aliishi
maisha ya wasiwasi sana alikuwa akiwaza kuwa walikuwa hawajapima damu zao,kwani
hawakuwa wachumba,hakuna aliyebeba kondom kwani hawakuwa wamejipanga kufanya
mapenzi walikuwa marafiki na hakujua kuwa amepokea ujauzito au la. Kwa kweli
kama vijana hawajaandaliwa vya kutosha kukabiliana na urafikiwa jinsia tofauti
wanaweza kujikuta wameishia kuharibu urafiki wao.
Ni kwa sababu hii Wachungaji wengi hubaki
wakifukuzana na vijana na kuwafikiri kuwa ni wazinifu na kuwawekea sheria kali
ambazo kwa kawaida hazisaidii kuzuia tamaa za mwili,na kunawajengea vijana
nidhamu ya woga, ni muhimu vijana wasibanwe kwa sheria za kifarisayo badala
yake wapewe mafundisho yatakayo wajenga katika uadilifu,ni muhimu kufanyika
kaka au dada halisi kwa kila msirika katika kanisa,tukiishi kama ndugu si
rahisi kufikia katika mawazo ya kingono, ni vizuri kina dada wakivaa kwa
kujistahi kama mtu afanyavyo mbele ya kaka yake kwa ni mvao unapeleka ujumbe na
unaweza kutongozwa kwa sababu ya muonekano tu (Mithali 11;16),Tafakarini gharama ya kufanya dhambi kwani dhambi ni
nzuri lakini inagharama,jifunze kutofautisha kati ya upendo na tama,shirikisha
rafiki zako namna unavyojisikia kihisia ili uweze kusaidiwa kwani kwa wakati
Fulani kila mwanadamu hushambuliwa na mawazo ya kingono wakiwemo viongozi wa
dini kwani wao sio malaika. Jifunze kuulinda moyo na mwelekeo wake(Yeremia 17;9). Jizoeze kuwa mwenye
dhamiri njema (Mdo 24;16),na
ikiwezekana kuweni katika mfumo wa timu inayozidi idadi ya kawaida ya
kugawana,kaeni katika mazingira yasiyo na mashaka msijifiche.
Vijana ni muhimu tu wakafahamu kuwa Mungu
alipofunua neema ya wokovu alikuwa anataka waliookolewa waishi kwa kiasi
angalia biblia inasema hivi “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote
imefunuliwa;nayo yatufundisha kukataa ubaya na tama zote za
kidunia;tupatekuishi kwa kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa”(
Tito 2;11-12),soma pia (Tito 2;6) “Vivyo hivyo na vijana
wanaume uwaonye kuwa na kiasi” Kwa
msingi huu nami nikuonye kama maandiko kuwa hakuna jambo zuri duniani kama kuwa
na marafiki wa jinsia tofauti lakini hakikisha haufunui,yaani haushiriki ngono
nahii itadumisha heshima na urafiki mwema,ukifunua utaharibu uhusiano hata huo
wa urafiki,mimi nami kama mtumishi wa Mungu sipendi vijana wabanwe na sheria
lakini nataka vijana kwa hiyari yao na kwa kuutambua wokovu na kuishi kwa kiasi bila kumvunjia Mungu
heshima kwa faida ya maisha yetu mungu akubariki.
Jinsi
ya kuchukuliana na watu tofauti tofauti
Kuna
wakati inatulazimu katika maisha kuvunja urafiki na baadhi ya watu kutokana na
kushindwa kuchukuliana nao au kushindwa kuwaelewa wewnzetu kuwa ni watu wa
namna gani na ni wa kundi gani katika tabia sehemu hii itatusaidia kufahamiana
na pia kijifahamu ili iwe rahisi kwako kuchukuliana na watu woote rafiki
aliyekomaa hawezi kupoteza marafiki kwani anawajua rafiki zake nguvu zao na
udhaifu wao Biblia ina tuambia kuna aina nne za watu ona (Mithali 30;11-14).jamii hizi kisaikolojia huitwa Melancholic (mst
11),Phlegimatic (mst 12),Sanguine (mst 13) na Colerich(mst 14). Jamii hizi zina
sifa na madhaifu, mbalimbali ambazo ni taa ya kutuonyesha sifa zao Sifa hizo ni
kama ifuatavyo;-
Melancholy
Kundi la watu wenye Nafsi inayoumia.
Kwa
kawaida hili ni kundi la watu makini, wenye kuweza kunyambulisha mambo,ni wenye
kupendelea ukamilifu,wana mpangilio wa mambo wana mawazo mazuri na wenye
kujitoa jamii hii ya watu wengi wamekuwa wanasayansi wasanii wanafalsafa na
wagunduzi wa kubwa pia ni wachoraji,Hata hivyo ni kundi la watu
wasiojichanganya na jamii wapweke na wanaoumia mioyo,wanatazamia mambo ya
kuumiza ni wabinafsi,hana ushirikiano anatunza visasi wanahitaji tunda la roho
la furaha na amani.
Phlegmatic.
Kundi la watu wenye Nafsi iliyotuliana taratibu.
Hili ni kundi la watu
wanaojiamini,wanaojitegemea na kujitosheleza na ni wapenda amani,kundi hili ni
la watu wasioweza kubadilika kwa haraka na hupenda kusanifu mambo,hata hivyo
kundi hili hupenda kujilinda ni waoga,wachoyo hawahamasiki na ni wavivu
wanapenda usingizi na mambo yao ni polepole na ni wachokozi chinichini hufanya
chochote wanachoshauriwa
Sanguine.
Kundi la watu wenye Nafsi Changamfu.
Kundi hili ni kundi la watu wachangamfu sana
wanaweza kufanya marafiki kwa haraka sana ni waigizaji wazuri na wasanii,ni
wasemaji sana ,wacheshi,ni marafikihawatulii na wasiojitegemea,hata hivyo
sanguini ni wadhaifu,wanaonekana kama hawana nidhamu waoga,wana haraka.
Choleric
.Kundi la watu wenye Nafsi Katili.
Kundi
hili ni kundi la watu jasiri,wanaojiamoni,ni viongozi hufanya mambo yatokee ni
watendaji wanaona mbali wanaweza kufanya maamuzi lakini ni wenye hasira
,hila,kujigamba,hana hisia za huruma,ni katili anajitoa sadaka kwa kufanya kazi
kupita kawaida.
Kuna uwezekano wa kujijua kuwa uko kundi gani
kwa kuangalia sifa za makundi hayo nzuri na dhaifu kisha unachukua idadi ya
sifa utakazozipata unazidisha kwa mia na kugawa kwa idadi ya sifa zote hapo
utajijua.
Mfano tunamjadili Kamote kujua
kuwa Yeye ni kundi gani hivi ndivyo tutakavyofanya
Melancholy
|
|
|
Phlegmatic
|
|
|
Sanguine
|
|
|
Choleric
|
|
|
Anauchungu
|
|
|
Anajiamini
|
|
|
Mcheshi
|
|
|
Ni
katili
|
|
|
Ana
jitoa
|
ü
|
ü
|
Mtaratibu
|
|
|
Msemaji
|
|
|
Anahasira
|
|
|
Ana
kipawa
|
ü
|
|
Anajitosheleza
|
|
|
Muigizaji
|
|
|
Jasiri
|
|
|
Ni
mkamilifu
|
|
|
Habadiliki
|
|
|
Anakelele
|
|
|
Mzalishaji
|
|
|
Mbunifu
|
|
|
Hahamasiki
|
|
|
Muoga
|
|
|
Mtendaji
|
|
|
Makini
|
|
|
Ana
sanifu
|
|
|
Muongo
|
|
|
Kiongozi
|
|
|
Hashirikiani
|
|
|
Mvivu
|
|
|
Muhamsishaji
|
|
|
Anaamua
|
|
|
Hanaharaka
|
|
|
Ana
choyo
|
|
|
Hana
aibu
|
|
|
Anakisasi
|
|
|
Mgunduzi
|
|
|
Hana
haraka
|
|
|
Si
mtendaji
|
|
|
Hujisifu
|
|
|
Mchoraji
|
|
|
Hujilinda
|
|
|
Kigeugeu
|
|
|
Ana
hila
|
|
|
hunyambulisha
|
ü
|
|
Hupendaamani
|
|
|
Ana
haraka
|
|
|
hajihurumii
|
|
|
Unaweza kuona kuwa alama za x
zinaonyesha sifa ambazo Kamote hana hivyo katika Melancholy Kamote hana alama
tatu na alama nane zilizo tupu ni sifa
alizo nazo sifa zitakazopatikana utazigawa kwa 12 sawa na jumla ya sifa zote za
kila sifa hivyo katika melancholy Kamote ana sifa nane na anakosa tatu hii ni
kusema kuwa katika melancholy na sifa nnyingine Kamote atakuwa na sifa
zifuatazo kwa kila moja ile itakayokuwa na asilimia kubwa zaidi ya wengine
ndiyo sifa ya mtu huyo mfano mzuri ni huo hapo chini
Melancholy
kwa Kamote ni = 8/12 X 100=66 %
Phlegmatic
kwa Kamote ni= 7/12X 100=58%
Sanguine
kwa Kamote ni=7/12X100=58%
Choleric
kwa Kamote ni = 12/12X100=100%
Hivyo Kamote ni Choleric kwa
asilimia 100 lakini anazo sifa nyingine kutoka katika makundi mengine na kwa
kawaida zile zinazojitokeza kwa wingi zaidi zile mbili hutabiri wazazi wa Kamote
kuwa mmoja ni Melacholy na mwingine ni Choleric na kwa kawaida Melancholy akioana na choleric melancholic
huumizwa hivyo mmoja wa wazazi wa Kamote katika ndoa alikuwa ni nafsi
iliyoumizwa na kitaalamu Yule anayeumia hufa haraka na ni kweli mzazi mmoja wa
Kamote yaani mama yangu alikufa mwaka wa 1984 hivyo chati hizi husaidia hata
kujua sifa za wazazi na taabu zao katika ndoa na kama mmoja yuko hai au l
Enye
Nguvu
|
Ana kisasi Ni katili
Ni
mwenye kujitoa Ana
hasira kali
Ana
kipawa Jasiri
Ni mkamilifu Ni mzalishaji
Ni mbunifu
Ni mtendaji
Ni makini Ni kiongozi
Hashirikiani Anamaamuzi
Ni mcheshi Anajiamini
Ni muigizaji Ni mtaratibu
Nimsemaji
sana Anajitosheleza
Ana kelele
Habadiliki
Ni muongo
Hahamasiki
Muoga
sana Ni mwenye sanifu
Anakigeugeu Mvivu sana
Hana nidhamu Ni
mwenye choyo
Dhaifu
Mchoro huu hapo juuna ule wa box pale juu
zaidi husaidia katika kufanya hesabu za
kujifahamu kuwa uko kundi gani kati ya hayo na sifa ulizonazo ,kwa kawaida kila
mwanadamu anasehemu zote hizo nne iliyo yake ni ile inayojitokeza kwa kiwango
kikubwa zaidi kwa asilimia ingawaje nyingine zinaweza kijitokeza kwa viwango
vingine tunapofanya hesabu hizo kusudi sio kwa ajili ya kumcheka mtu bali kujua
yuko kundi gani anahitaji matunda ya roho ya kiasi gani na watu watawezaje
kuchukuliana naye hivyo Hesabu hizi zisitumike kama kigezo cha kuchekana au
kusanifiana naamini utautumia kwa busara michoro hii hapo juu
(Michoro yoote Na hesabu Kwa niaba ya mwandishi wa somo hli Mchungaji
Innocent Kamote)
Maoni 1 :
IT IS HELP FULL TO ME THANKS SO MUCH
Chapisha Maoni